Thursday, 29 May 2014

KINANA AWASILI WILAYA YA BABATI VIJIJINI


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal JituSon mara baada ya kuwasili na kupokelewa katika Kata ya Mangara wilaya ya Babati Vijijini.Katibu Mkuu wa CCM yupo ziarani katika mkoa wa Manyara ambapo atafanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kukagua uhai wa chama.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa amezungukwa na wakazi wa Kata ya Mangara wilayani Babati Vijijini waliojitokeza kwa wingi kuwapokea mara baada ya kuwasili wilayani hapo .
 Wananchi wa Kata ya Mangara wakiwa na nyuso za furaha wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  ambaye ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kata ya Mangara kabla ya kukagua mradi wa ujenzi  wa wodi ya kituo cha afya cha Mama na Mtoto.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Ndugu Vrajilal JituSon mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa wodi ya kituo cha afya cha mama na mtoto.Katibu Mkuu wa CCM yupo ziarani katika mkoa wa Manyara ambapo atafanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na kukagua uhai wa chama.
 Wananchi wa Kijiji cha Mangara wakionyesh bango la kuomba msaada wa kusaidiwa kujengwa kwa daraja katika mto Mangara.
 Mto Mangara ambao wananchi wanaomba daraja lijengwe.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Magugu ambapo aliwapa usia vijana wenzake kwa kuwaambia Vijana wachape kazi na waachane na talalila za wanasiasa njaa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa  Magugu na kuwaambia viongozi wengi wa vijiji wamekuwa wakiingia mikataba bila kuwashirikisha wannchi hivyo kusababisha migogoro mikubwa ya ardhi na amewataka wananchi kuchagua viongozi makini,Katibu Mkuu wa CCM ameshtushwa na baadhi ya watu kumiliki sehemu kubwa ya ardhi na kuwakodishia wananchi kwa ajili ya kilimo cha mpunga.

Wednesday, 28 May 2014

KINANA ATINGISHA ENDASAK NA KATESH WIYALANI HANANG



 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi mjini Endasaki, Hanang, jana, Mei 27, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na njia sahihi ya kutatua kero hizo mkoani Manyara
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiongozana na Vijana wa Kibarbeig kuingia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ofisi ya CCM Kateshi, jana, Mei 28, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Ofisi ya CCM Katesh, mkoani Manyara
 Kinana akihutubia kwenye mkutano huo wa Katesh
 Mbunge wa Hanang, Mary Nagu akihutubia kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM jimboni mwake kwenye mkutano huo wa Katesh
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo
 Mkuu wa Wilaya ya Hanang Christina Mndeme akisalimia wananchi kwenye mkutano huo wa Katesh
 Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye na Mbunge wa Hanang Dk. Mary Nagu wakijadili jambo wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Katesh mkoani Manyara, Mei 27, 2014. Sumaye amewahi pia kuwa mbunge wa Hanang.
 Kinana akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Igembesabo iliyoibuka bingwa katika michuano ya Vijana wa jimbo la Hanang, wakati wa mkutano wa Katesh
Kinana na Nagu wakikabidhi mizinga ya nyuki kwa vikundi vya vijana Katesh
 Mwanachama wa Chadema akirudisha kadi yake kwa Kinana alipoamua kuhamia CCM kwenye mkutano wa Katesh
 Kinana akipiga mpira wakati Nagu akisubiri kuudaka, wakati wa ufunguzi mashindano ya vijana Endasaki
Endasaki
Kinana  na Sumaye wakishiriki ujenzi Ofisi ya CCM tawi la Qaroda,

Tuesday, 27 May 2014

MZIGO MPYA UMEWASILI KARIBU TRIPPLE A FASHION BARABARA YA UHURU MWANZA MKABALA NA VIZANO HOTEL

 Mkurugenzi wa Tripple A Fashion  Bi Aisha Abas anayofuraha kuwajulisha wateja wake wote na watu wengine wote kuwa mzigo mpya umewasili karibuni sana dukani kwake .

 Open shoes za kila aina utapata
 Mitindo tofauti tofauti
 Karibu sana Tripple A Fashion
 Jenz na suruali za aina tofauti utapata
 Mashati aina zote na za watu wa rika tofauti utapata
 Viatu nya kisasa vya wadada,wamama
 Urembo wa akina mama wa kila aina utapata
 Pochi za kila aina za ngozi utapata kwa bei nafuu,magauni ya kila aina utapata
 Duka hili lipo jijini Mwanza barabara ya uhuru mkabala na Vizano Hotel
kARIBUNI SANA KWA BIDHAA ZA VIWANGO NA UBORA

Monday, 26 May 2014

FELIX MULOKOZI FRANCE BWAHAMA MGENI RASMI KATIKA HARAMBEE YA UNUNUZI WA KINANDA CHA KWAYA PAROKIA YA NGOTE MULEBA

 Bw Felix Mulokozi ambae alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uchangiaji wa ununuzi wa kinanda katika parokia ya Ngote, kigango cha madalena wilaya ya Muleba akizungumza na waumini na kuamasisha watu mbalimbali kuthamini na kushiriki kusaidia katika mambo ya kiroho,Bw Felix Mulokozi  alieambatana na mkewe Bi Jesca Kokushoborora na mtoto wao na kumuwakilisha Dada yao Monica France Bwahama walichangia kiasi cha milioni moja,Mh Mbunge Prof Anna Tibaijuka kupitia kwa Mgeni rasmi alichangia shilingi laki mbili na nusu,na wadau mbalimbali ambao jumla yake ilfika milioni mbili na laki nne ambayo inakidhi ununuzi wa kinanda hicho,mbali na kinanda ,yapo mahitaji ya mwalimu wa kufundisha kwaya na kutengeneza albamu ya video na mahitaji ya gharama zote ni shilingi milioni kumi. Hivyo kupitia hotuba ya mgeni rasmi awewaomba watu mbalimbali kupitia vyombo vya habari kuguswa na jambo hili na kusaidia kwaya hii hili waweze kulitangaza neno la mungu.
 Wanakwaya wakisoma risara mbele ya mgeni rasmi
 Bi Jesca(mke wa mgeni rasmi) akiwa na mtoto wao Natasha.
 Mgeni rasmi akiongea na waumini wa  Parokia ya Ngote Karambi.
 Wakati wa harambee unatoa ulichonacho
 Anaonyesha dole gumba na ni muumini wa serikali mbili
 Baada ya kufikia malengo ya kinanda wakacheza kwa raha zao, ila bado mwalimu na fedha za kurekodi video ya albamu yao,wasaidie wanakwaya hawa.
Hapa Mgeni rasmi akiteta kitu na Padre.

PAPA FRANCIS AOMBEA UKUTA WA BETHLEHEMU.



Papa Francis akiombea ukuta wa Bethlehemu
Papa Francis ameombea ukuta wa saruji ambao Israel inajenga kulitenga eneo la ukingo wa Magharibi huko Bethlehem.
Aliweka kichwa chake juu ya juu ya ukuta huo, ambapo kumechorwa maneno" ipe uhuru Palestina".
Pande zote mbili zimekubali mwaliko.Papa ametoa mwaliko kwa Wa-Israili na Wapalestina waende Vatikani, kuomba mzozo wao umalizike.

Hapo awali Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani aliutaja mzozo kati ya Palestina na Israel kama usiokubalika huku akizitaka pande zote mbili kufanya maamuzi ya busara ili kuweka amani.
Akizungumza mjini Bethlehem ,papa Francis ametaka kubuniwa kwa taifa huru la Palestina pamoja na Israel.
Aidha alifanya maombi katika eneo ambalo Yesu anadaiwa kuzaliwa.
Akiwa katika ziara yake ya mji wa Bethlehem ,kiongozi huyo wa dini alisimama katika eneo ambalo Israel inajenga ukuta mkubwa pamoja na eneo la West bank ili kufanya maombi.
Maandishi yaliokuwa juu yake alipokuwa akiomba yalisema 'papa tunamtaka mtu atakayezungumzia kuhusu haki'.