Tuesday, 8 April 2014

CHUO CHA UALIMU ERA KINACHOFUNGULIWA MWEZI WA SABA MWAKA HUU CHAANZA UANDIKISHAJI WANAFUNZI, KUWA NA URAFIKI NA GLOBAL CITIZENS NETWORK YA MAREKANI

 Hatimae uandikishaji wa wanafunzi katika chuo cha ualimu ERA kinachotarajia kuanza mwezi wa saba mwaka huu,Akiongea na mmiliki wa Blog hii ,Mwanzilishi wa chuo cha ERA kilichoko Bukoba Manispaa, kata ya Kitendaguro nje kidogo ya mji wa Bukoba Ndugu Paskazia Barongo amesema maandalizi yanaendelea vizuri na taratibu zote zinaendelea vizuri, ikiwa ni pamoja na kuandikisha wanafunzi wanaotarajia kuanza masomo mwezi wa saba mwaka huu.Amesema Ndugu Paskazia Barongo kuwa ni matarajio yao kuwa wamejipanga vizuri kutoa Elimu Bora ili waalimu watakaohitimu katika chuo cha ERA waweze kutoa elimu bora katika shule za msingi popote Tanzania kwa Weredi na ufasaha mkubwa,Pia ameeleza kuwa ile kuboresha mahusiano na  vyuo vingine ndani na nje ya nchi chuo chao kimeanzisha urafiki na  Global Citizens network walioko Minneapolis Marekani ili waweze kushirikiana katika maswala ya Elimu kwa wanafunzi wa ERA kwenda Marekani na wa Marekani kuja ERA. Ndugu Paskazia Barongo ameitaka jamii kwa ujumla kuleta watoto wao waliomaliza kidato cha nne  na hawakuweza kupata nafasi wajiunge na chuo cha ERA na watajikomboa wao binafsi na kuwa Walimu wa mfano katika kutoa elimu bora nchini Tanzania.
 Mama Ashura( Fundi cherehani) akimpima Unifomu mmoja wa wanafunzi anaetarajia kuanza masomo  chuoni mwezi wa saba mwaka huu
 Vipimo vya Unifomu
 Bi Paskazia Barongo akiongea na wanafunzi wanaotarajia kujiunga na chuo, wakisubiri kupima Unifomu chuoni hapo
 Bi Linda Stuart (kushoto) Mkurugenzi wa Global citizens network ya Marekani akiwa na Mkurugenzi wa Cosad Ndugu Smart Baitani anaeishi  Marekani
 Wanachuo watarajiwa wanaoanza masoma mwezi wa saba mwaka huu
 bI Paskazia Barongo akiwakaribisha wageni
 Mkuu wa  Chuo cha ERA  Bi Paulina Ngina Musau akieleza namna walivyojipanga kutoa Elimu katika chuo cha ERA
 Mmoja ya wanachuo wanaojiunga akitoa neno la shukrani kwa kuanzisha chuo
 Mwanachuo mtarajiwa akipongeza uongozi kwa wazo zuri la kuanzisha chuo cha ualimu
 Mzazi akinukuu vifungu vya Biblia na kusema chuo cha ERA ni mkombozi kwa watoto wao
 Wakipata kifungua kinywa
 Mtoto wa Bi Linda Stuart akipata chai
 Mkuu wa chuo akimtembeza kumuonyesha mazingira ya chuo na sehemu ya mabweni, katika chuo cha ERA Godoro na kitanda unavikuta chuoni ili kumpunguzia gharama mzazi
 Ni vitanda imara na salama
 Vyoo vizuri kwa afya ya wanachuo
 Mazingira ya kupendeza
 Bi Paskazia akitoa maelezo
 Picha ya pamoja
Mkuu wa chuo Bi Paulina akiwa na mmoja wa wakurugenzi wa chuo ambae pia ni mwalimu katika chuo cha ERA Bw Ocham Collins wakiwa na mtoto wao

Sunday, 6 April 2014

YANGA YAIBANJUA JKT RUVU MABAO 5-1 UWANJA WA TAIFA


 Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva, akiruka kukwepa kwanja la beki wa JKT Ruvu, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1. Mabao matatu yalifungwa na Mrisho Ngassa, katika dakika ya 7, Dakika ya 15 na Dakika ya 48. 

Mabao mengine yalifungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 39 na bao la tano likafungwa na Hussein Javu katika dakika ya 51.  Kwa ushindi huo sasa Yanga imefikisha jumla ya Pointi 49 wakiwa nyumba ya Azam Fc wenye jumla ya Pointi 53 kwa tofauti ya 4. Bao la kufutia machozi la JKT Ruvu lilifungwa na Nashon Naftari, katika dakika ya 83.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia moja kati ya mabao matano yaliyofungwa katika mchezo huo leo.
 Sehemu ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
 Didier Kavumbagu (kulia) akichanja mbuga kumtoka mchezaji wa JKT Ruvu.
Kipa wa JKT Ruvu, akijaribu kuokoa moja kati ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake.
JKT Ruvu wanapata bao la kwanza kupitia Iddi Mbaga baada ya kazi nzuri ya krosi iliyopigwa na Sino Augustino.

RAIS JAKAYA APIGA KURA MSOGA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya mrisho Kikwete akisoma karatasi ya kupigia kura kabla ya kupia kura kumchagua Mbunge wa Jimbo la Chalinze kwenye kituo cha kupigia kura cha Zahanati Msoga.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye chumba cha kupigia kura wakati wa kupiga kura za kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura yake ya kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.
 Mama Salma Kikwete akiweka kura yake kwenye sanduku la kupigia kura kwenye kituo cha Zahanati Msoga.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha AFP Ndugu Ramadhani Mgaya akizungumza na waandishi wa habarai nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 1na kusema kuwa Chama chake kitakubali matokea yeyote na pia kama watashindwa watajipanga kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze Ndugu Mathayo Torongey akizungumza na baadhi ya mawakala alipotembelea kituo cha Ofisi Mtendaji Kata namba 1, Bwilingu.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete akihakiki taarifa zake kabla ya kupiga kura kwenye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 3 Bwilingu, Chalinze.
Aziza mtoto wa mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akimsaidia Baba yake kuweka kura kwenye sanduku la kura ,Ridhiwani alipigia kura yake kwenye kata ya Bwilingu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Chalinze Ndugu Samuel Salianga akizungumza na waandishi wa habari nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata Bwilingu na kutoa tathmini ya jinsi zoezi linavyoendelea na kufafanua mambo mbali mbali yanayohusu uhalali wa wagombea kupiga kura popote ndani ya jimbo la uchaguzi.