Monday, 31 March 2014

BUKOBA VETERAN WAZINDUA KATIBA NA KUKABIDHIWA JEZI KUTOKA UJERUMANI,HAFLA YADHAMINIWA NA KINYWAJI CHA CLIMAX

 Bukoba Veteran baada ya kukamilisha mchakato ulioanza siku nyingi zilizopita za kuandaa Katiba  hatimae wamezindua Katiba itakayowaongoza,lakini pia wamekabidhiwa Jezi kutoka Ujerumani, mgeni rasmi alikuwa  Sakina Sinda Wakili wa Serikali Mfawidhi wa Mkoa wa Kagera.
 Kapten akipokea jezi
 Wazee wa busara
 Chezea Climax weweeeeeee
 Hafla imedhaminiwa na kinywaji cha Climax
 MCJerry akichombeza
 Mgeni rasmi akiwasili ukumbi wa Lina's
 Katibu wa Bukoba Veteran Raksoni Kahabuka akiongerea mchakato wa Katiba ya Bukoba Veteran
 Climax ni kinywaji  bora viwango vya kimataifa
 Wakipata kinywaji cha Climax
 Mdau Didas Zimbile akiwa na Mainda E
 Optat Katibu
 Wanaveteran
 Bw Wily Kiroyera akieleza jinsi alivyofaamiana na  Fr Gerald Rugumila kupitia mtandao wa Facebook mpaka kuifaamu Bukoba Veteran na  sasa kuwa marafiki na timu kubwa  ya Mainz 05 inayocheza  BUNDESLIGA NA INAYOMILIKI  UWANJA  unaochukua watazamaji 34,036 huko  Ujeruman
 Fr Gerald Rugumila akieleza namna alivyoweza kuijua Bukoba Veteran kupitia kwa Bw Wily Kiroyera
 Mwenyekiti wa Bukoba Veteran Ernest Nyambo akiongea na wadau kuhusiana na siku muhimu na ya kihistoria katika umoja wa Bukoba Veteran
 Fr Mloso wa Ntungamo Seminary akitoa neno
 Bw Kagya Mratibu wa tamasha kubwa litakalofanyika siku ya pasaka Lina;s . Kapotive singles watawasha moto wakiwa na wasanii wa injili wakubwa Tanzania
 Katibu wa KRFA Salumu Chama akiongea na wana Bukoba Veterani
 Chezea Bukoba Veteran weweeee
 UZI wa Mainz 05
 Fr Gerald Rugumila mkazi wa manispaa ya Bukoba Nshamya anaehishi Ujerumani akikabidhi jezi  kwa kapten wa timu Mwinyi ,  Fr Gerald ni shabiki nguli wa Mainz 05 ya Ujerumani inayoshiriki ligi kuu ya BUNDESLIGA, Fr Gerald amekuwa na urafiki wa karibu na Bw Wily Kiroyera kupitia mtandao wa Facebook akiwa Ujeruman na sasa kuwa kiunganishi na Bukoba Veteran
 Baadhi ya wanakamati wa liofanikisha katiba kuwepo
 Mh Matete akifafanua vipengele vya katiba
 Hii ndio Katiba
 Fr Gerald Rugumila akivaa Tshirt aliyopewa kama  zawadi
 Mwenyekiti akieleza kwa ufupi jinsi T.shirt ya Bukoba Veteran itakavyowawakilisha ujerumani
 Mwenyekiti akiwa na Moses wakionyesha uwezo wa kusakata bolingo
 NI NGWASUMA KWA KWENDA MBELEEEE
 Afisa Utamaduni Manispaa ya Bukoba Rugeiyamu akimkaribisha mgeni rasmi
 Mgeni rasmi Sakina Sinda  Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Kagera akitoa neno katika uzinduzi wa katiba ya Bukoba Veterani katika ukumbi wa Lina's
 Mkurugenzi wa Lina's Mtensa akitabasamu na camera yetu
 Kijana mwiba akionyesha nembo ya Mainz 05 ya ujeruman akiwa na Capten Mwinyi wa Bukoba Veteran
 Rahimu akiwa na Kagya
 Mwenyekiti wa Bukoba Veteran Ernest Nyambo akiongea na wadau akisisitiza kutambua na kuthamini mchango mkubwa wa  kinywaji cha Climax kufanikisha hafla
 Bw Bube mkurugenzi wa shule ya watoto wadogo Leoleo akisoma katiba ya Bukoba Veteran kwa umakini mkubwa akiwa na Super Mkude  mkurugenzi wa shule ya Karume
 Bw Endrew Kagya akielezea ubora wa kinywaji cha Climax kwa niaba ya  wakala  wauzaji wa  Climax mkoa wa Kagera ambao ndio wamedhamini hafla hii
 Kwa raha zetuuuuu
 Hii ndio katiba ya Bukoba Veteran
Kushoto Fr Gerald Rugumila, Fr Mlosa na  mgeni rasmi Mh Sakina Sinda
 Mgeni  Rasmi akipata chakula
 FR Gerald Rugumila akipata chakula, kiunganishi kikuu kati ya Bukoba Veterani na  timu ya Mainz 05 ya Ujerumani kupitia kwa Wily Kiroyera
 Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama akipata chakula
 Wily Kiroyera akipata msosi
 Kamati ya T.shirts za Bukoba Veteran  umekuja mzigo mpya Popote ulipo duniani au Tanzania, Kagera  au Bukoba changia timu kwa kununua T.shirt kwa 20,000 tu .
 Kijana Rakson Kahabuka ndani ya uzi  wa Mainz 05 ya Ujeruman
Ongera Bukoba Veretan chini ya uongozi wa mwenyekiti Ernes Nyambo kwa hatua kubwa mliyopiga jamcobukoba.blogspot.com tunawatakia ufanisi zaidi.

Friday, 28 March 2014

CAMERA YETU PANDE ZA HAMUGEMBE LEO DARAJA LA KANONI,NI MWEZI MMOJA NA SIKU CHACHE TANGU LIFUNGULIWE BAADA YA UKARABATI KUKAMILIKA NA KUTUMIA ZAIDI YA MILIONI 300 NA SASA LINAFANYIWA TENA

 Nakumbuka siku hiyo takribani mwezi moja na siku kadhaa zimepita maeneo ya daraja hili la Kanoni barabara kuu inayounganisha manispaa ya Bukoba na  Mikoa mingine ilikuwa ni furaha, nderemo na vifijo, huku wananchi chini ya Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Fabian Massawe wakishuhudia kwa macho na taarifa iliyojaa matumaini na weredi mkubwa kuhusu ukamilishaji wa ukarabati wa daraja hili la Kanoni. Kipindi hicho daraja hili lilipofungwa ilitokea adha kubwa kwa magari kupitia njia zingine ambazo zilisababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi ,lakini pia kwa madereva na kusababisha ajali na watu kupoteza maisha.Kwa taarifa iliyotolewa siku hiyo kwa mbwembwe na umaili mkubwa mbele ya mkuu wa mkoa kwa kutumia mamilioni ya fedha, leo ndani ya mwezi mmoja na siku  hali iko hivi.Hapa yapo maswali ya msingi sana kujiuliza ,Lakini kikubwa ni watu kutambua kuwa wale waliobahatika kupewa dhanana ya kusimamia masrahi ya watu watambue pia wajibu wa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi, na zaidi ya hapo waende mbali zaidi kuwa Duniani  tunapita na kila kilichomo, ulichonacho , ulichokula, ulichokipata aidha kwa haki au vyoyote vile utaviacha na utahukumiwa kulingana na matendo yako.
 Ni  swala la kusubiri, maana hata pikipiki haiwezi kupishana na gari kutokana na ufinyo wa daraja kwa sasa
 Ni msongamano wa magari ambayo inabidi  yasubiri
 Hili ndio daraja ambalo upande mmoja  linafanyiwa ukarabati tena, na hali hii kusababisha msongamano

Thursday, 27 March 2014

UTIMIZA MIAKA 3 YA KLABU YA BONGO MOVIE ITAKAYOFANYIKA MEI 2


 Mwenyekiti wa Bongo Movie, Bw Steve Nyerere akiongea na waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade house Mikocheni.
 Steve Nyerere akinadi kinywaji cha Windhoek ambao ndio wadhamini wakuu wa sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movies, Sherehe itakayofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni jijini Dar Es Salaam Ijumaa ya tarehe 28.
Rais wa FM Academia Nyoshi Ali Sadat akiongea na wadau waliofika katika ukumbi wa East 24 wakati wa utambulisho wa wasanii na bendi zitakazotoa Burudani siku ya Sherehe ya Kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie itakayofanyika katika ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House ijumaa ya tarehe 28 Mwezi huu
 Meneja Masoko wa Kampuni ya Mabibo Beer, Bw Jerome Rugemalila akiongea na Waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa Bendi na wasanii watakaotoa burudani ya nguvu siku ya sherehe ya Kuzaliwa kwa Bongo Movie itakayofanyika tarehe 28 katika Ukumbi wa East 24 uliopo Arcade House Mikocheni Jijini Dar.
 Baadhi ya wasaniii wa Bongo Movies wakifuatilia kwa makini 
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer, Benadetha Rugemalira (aliyeshika kinywaji cha Climax) akifuatilia kwa makini matukio wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani siku ya ijumaa kwenye sherehe ya Kuazimisha miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movie
 Baadhi ya wadau waliohudhuria utambulisho huo uliofanyika katika ukumbi  wa East 24
 Mkurugenzi Mkuu wa Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalira (kulia) akijadiliana jambo na Meneja masoko wa Mabibo Beer, Jerome Rugemalira (pili kulia) na Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie, Bwa Steve Nyerere na Msanii wa bongo movie Adam Kuambiana
Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere akijadiliana jambo na Katibu wa Bongo Movie Mtitu wakati wa utambulisho wa Wasanii na bendi zitakazotoa burudani wakati wa sherehe za kutimiza miaka mitatu ya kuzaliwa kwa klabu ya Bongo Movie.

RIDHIWANI AENDELEA NA KAMPENI BWILINGU


 Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akihutubia wakazi wa kijiji cha Matuli Kata ya Bwilingu na kuwaambia CCM ni Chama pekee kinachoweza kuahidi na kutekeleza yale yalioahidiwa.
 Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia tiketi ya CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Martine Shigela  wakati wa mkutano wa kampeni za CCM kijiji cha Matuli kata ya Bwilingu.
 Mgombea Ubunge jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na wakina mama wa kimasai waliokuja kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni kijiji cha Matuli.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Nsugu Ridhiwani Kikwete akipandisha bendera baada ya kufungua shina la wakereketwa  la Msimamo.
 Msanii maarufu Dokiii akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakina Mama wa Kimasai wakati wa mkutano wa kampeni za Ubunge kupitia CCM kwenye kijiji cha Matuli
 Msanii Hafsa Kizinja akitumbuiza huku mgombea wa Ubunge CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete kijiji cha Matuli.