Wednesday, 26 March 2014

YALE MANENO YA KUFA KUFAANA YAMETIMIA UWANJA WA KAITABA BUKOBA KUFUATI UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA 2-5-2014

  Wa kale walinena  Kufa kufaana, maneno haya yametimia na kuleta faraja kwa wakazi wa manispaa ya Bukoba na Mkoa mzima wa Kagera kufuati ujio wa mbio za mwenge kitaifa zitakazozinduliwa rasmi 2-5-2014 katika uwanja wa Kaitaba.Yamekuwepo malalamiko ya muda mrefu sana kwa wapenzi wa soka kulalamikia ubovu wa majukwaa na miundo mbinu mbalimbali katika uwanja huu,Lakini kufuatia  tukio la uzinduzi wa mbio za mwenge yapo marekebisho makubwa yanaendelea katika uwanja huu, na Leo 26-3-2014 Mkuu wa Mkoa  wa Kagera Kanal Fabian Masawe alifika kujionea hali halizi ya maendeleo ya marekebisho ya uwanja nas kujionea  Wanafunzi  mia sita wa Halaiki wanaoendelea na mafunzo mbalimbali ya gwaride na nyimbo kwa ajili ya uzinduzi wa mbio za mwende Kitaifa Mkoani Kagera.
 Ni moja ya jukwaa ambalo linatengenezwa na litaezekwa juu kwa bati kumuwezesha mkaaji asipigwe na jua au kunyeshewa na mvua, na mbao zake zikiwa zimewekwa imara zaidi,
 Ukarabati ukiendelea
 Wanafunzi  mia sita wa shule za msingi katika baadhi ya shule Manispaa ya Bukoba wakiwa katika mafunzo ya Halaiki
 Kushoto ni Afisa Elimu shule za msingi Manispaa ya Bukoba Ndugu Fande akiwa na Afisa Utamaduni Manispaa Ndugu Rugeiyamu wakiratibu shughuli zote katika uwanja waKaitaba

 Ni Nesi akitoa huduma kwa wanafunzi wenye matatizo mbalimbali wanaoendelea na mafunzo ya Halaiki
 Muonekano wa Jukwaa

 Mkuu wa Mkoa Kagera Kanal Fabian Massawe akisalimiana na walimu wanaendelea kusimamia na kufundisha mafunza ya Halaiki wanafunzi
 Mwl J J Mugango(kulia) ni miongoni mwa walimu wanaofundisha na kushoto ni Ndugu Kilema Athuman Kambagwa mkufunzi wa Halaiki
 Mwl Alistidia ambae ni katibu  mkufunzi akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa
 Wanafunzi katika pozz tofauti
 Utapenda , vijana wanaweza
 Ni miongoni mwa alama ambazo wanafunzi wanafundishwa na wataonekana hivi
 Mwalimu anapokuwa kazini hakuna mchezo
 Ni manjonjo ya kila aina wanafunzi wa Halaiki haoo
 Hii ndio timu nzima

 Afisa utamaduni akimkaribisha Mkuu wa mkoa aongee na Walimu na wakufunzi

 Kanal  Fabian Massawe akiongea na wanafunzi kuwapa moyo na kuwataka pale kwenye mapungufu waongeze bidii

 Mkuu akikagua maeneo mengine
 Choo kipya kimejengwa katika uwanja wa kaitaba
 Hii ndio Kufa KUFAANA
 kAITABA inavyoo vya kufrash utapenda
 Jukwaa maarufu kama Jukwaa la Balimi nalo linaezekwa
 Jamcobukoba.blogspot.com tunatoa pongezi kwa uongozi wa kitaifa na mkoa kwa kuleta uzinduzi huu katika mkoa wetu,chini ya kapeti ziko habari kuwa uwanja huu hivi karibuni utawekewa nyasi bandia,yote ni heri kwa wana Kagera, ukizingatia Rais wa TFF NI...... Malizia mwenywe, Wahaya wanasema Eofisi etainamu wawe eikala ekomile. asante WAJINA.

Tuesday, 25 March 2014

MUAMKO JUU YA ULINZI SHIRIKISHI WASHIKA KASI ARUSHA TAARIFA ZAIDI ZA UHALIFU ZATOLEWA







Wananchi Mkoani hapa wameonekana kuwa na muamko zaidi wa Ulinzi Shirikishi baada ya kutoa taarifa mbili zilizofanikisha kukamata misokoto 1,038 ya madawa ya kulevya aina ya bangi pamoja na mirungi kilogramu 75.

Akizungumza na Waandishi wa habari ofisi kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema kwamba katika matukio mawili yaliyofanikisha ukamataji wa madawa hayo taarifa zake zilitolewa na raia wema.

Kaimu Kamanda Muroto alisema kwamba, tukio la kwanza lilitokea tarehe 18.02.2014 muda wa saa 1:30 asubuhi maeneo ya Kituo Kikuu cha mabasi jijini hapa ambapo mtu mmoja aitwaye Charles Ogaga Ayunga (38) raia wa Kenya na ni mkazi wa Taveta nchini humo, alikamatwa na misokoto 1,038 ya Madawa ya kulevya aina ya bangi iliyokuwa ndani ya boksi.

Akifafanua taarifa hiyo Kaimu Kamanda huyo alisema kwamba, siku ya tukio mtuhumiwa alikuwa anatokea maeneo ya Ngaramtoni akiwa kwenye Hiace na alipofika maeneo ya Kituo Kikuu cha Mabasi alishuka akiwa na boksi na kutaka kupanda basi linaloelekea Horiri wilayani Rombo lakini kabla hajapandisha boksi hilo kwenye basi hilo watu walimshuku na kutoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi, ambapo askari waliokuwa doria maeneo ya karibu walikwenda katika maeneo hayo na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa misokoto hiyo.

Mara baada ya mahojiano mtuhumiwa alikiri kuumiliki madawa hayo ya kulevya aina ya bangi na kueleza kwamba alikuwa anasafirisha kupeleka nchini Kenya.

Wakati huo huo mtu mmoja aitwaye Philipo Santolin (25) Mkazi wa Horiri wilayani Rombo alikamatwa na madawa ya kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa kilogramu 75 ambayo ilikuwa imehifadhiwa kwenye vifurushi tofauti tofauti7.

Akifafanua tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles Muroto alisema tukio hilo la ukamataji lilitokea tarehe 19/02/2014 muda wa saa 2:00 usiku maeneo ya Kaloleni jijini hapa.

Alisema siku ya tukio wananchi walitoa taarifa katika kituo kikuu cha Polisi kwamba, kuna mtu alikuwa anasafirisha madawa hayo katika gari aina ya Corolla lenye namba za usajili T 162 AYW toka mkoani Kilimanjaro kuja Arusha, ndipo askari walipoweka mtego maeneo ya Kwa Mrefu na mara baada ya gari hilo kusimamishwa halikusimama ndipo askari wakaamua kulifuatilia ambapo walifanikiwa kulikamata maeneo ya Kaloleni mara baada ya gari hilo la mtuhumiwa kupasuka tairi la mbele.

Kaimu Kamanda Muroto alisema mpaka hivi sasa watuhumiwa wote wawili wanahojiwa na watafikishwa makamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM YAFANYA KIKAO CHAKE CHA KWANZA LEO


 Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya Uongozi baada ya kuundwa leo. Kamati hiyo inayoundwa na wenyeviti wa Kamati za Bunge Maalum wote 12  pamoja na mambo mengine inajukumu la kaundaa ratiba ya Bunge Maalum. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge Maalum Yahya Khamis Hamad na aliyekaa kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samia Suluhu Hassan.
 Mhe. Sitta akiendelea kuongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi
 Naibu Katibu wa Bunge Maalum Dkt. Thomas Kashililah akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya Bunge Maalum kuhusu uwezo wa kutumika kupigia kura vifaa vya kielekroniki vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge wakati kamati hiyo ilipokutana jana.
 Mjumbe wa Kamati ya Uongozi Mhe. Anna Abdalah akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo.
 Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe..

Monday, 24 March 2014

WASHIRIKI 29 WA SHINDANO LA MAISHA PLUS 2014 WAINGIA RASMI KIJIJI

Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya) akiongea katka uzinduzi wa kijiji cha Maisha Plus, ambapo jana washiriki wapatao 29 waliingia kijijini kuanza kukabiliana na changamoto za kuweza kupata shilingi milioni 25 za kitanzania.
Wageni waalikwa waliofika kijijini cha Maisha Plus kuangalia uzinduzi.
Washiriki wa shindano la Mshindi wa Maisha Plus wakipewa maelekezo machache mara baada ya kuwasili kijijini kwao. 
Mmoja ya wawakilishi toka Oxfam ambao ni wadhamnini wa Maisha Plus 2014 akizungumza machache. Pembeni yake ni Afisa mtendaji wa Kampuni ya DMB ambao ni wamiliki wa Maisha Plus Masoud Ally (Masoud kipanya). 
Mkuu wa Kijiji Mwite Babu wa kaya akiwepo kuhakikisha wanakijiji wanakaribishwa kwa shangwe. 
Wageni waalikwa. 
Kazi ya kujenga nyumba za kuishi washirki wa maisha plus ikiendelea, ambapo washiriki hao walitakiwa kujenga nyumba zao za kuishi ndani ya masaa 48. 
Kila mmoja anawajibika kuhakikisha kazi ya kujenga nyumba inafanikiwa. 
Wadau kutoka Oxfam wakibadilisha mawazo mara baada ya kufika katika tukio la uzinduzi wa wawashiriki kuingia kijijini. 
Safari ya kuelekea kijiji cha Maisha Plus imeanza rasmi, washiriki wakiwa wamebeba mabegi yao ambapo kila mmoja alibeba mzigo wake mwenyewe kwa kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 1.5. 
Safari ikiendelea huku washiriki wakiwa wameshachoka, wengine walitamani kughairi kuendelea na safari. 
Wengine ilibidi wasaidiane kupeba mizigo. 
Hakuna kuchoka, kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe.
Wengine waliamua kulala ili waweze kunyoosha mgongo.

Sunday, 23 March 2014

Picha 15 za harusi ya Paul wa P Square na Anita Isama

1Baada ya pacha wake kufunga ndoa, hivi sasa ni zamu ya Paul Okoye ambaye amefunga ndoa ya kimila na mchumba wake wa muda mrefu Anita Isama.
Paul na Anita wana mtoto wa kiume na harusi yao imehudhuriwa na watu kama Omotola,D Banj,Naeto C,Banky W,Ini Edo,Iyanya na wengine wengi.
Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwenye harusi hiyo.
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15

MAGAZETI JUMAPILI



DSC 0068 93f54
DSC 0069 d399f
DSC 0070 a718b
DSC 0071 72547
DSC 0072 e22b2