Ni picha ya pamoja ya wafanyakazi wa jumuia ya Kasibante Redio waliondaa mlo wa mchana kwa ajili ya watoto yatima na walemavu wa viungo zaidi ya watoto 300 wakiwa na mliki wa Redio hiyo Balozi Kagasheki ambae alikuwa mgeni rasmi siku ya Valentine
Watoto kutoka Mugeza mseto, walemavu wa ngozi na macho
Matron wa watoto Mugeza mseto akiwa na mtoto mdogo mwenye umri wa mwaka mmoja mlemavu wa ngozi alieletwa na mama yake akiwa na umri wa miezi minne akamuacha shuleni hapo mpaka sasa mama huyo hakuwahi kurudi kumuona mtoto huyu , na hamjui mama yake , matroni huyu mtoto ndio anamtambua kama mama yake, mama wa mtoto huyu inasemekana anaishi Karangwe alimleta mtoto huyu kwa ajili ya kuokoa maisha yake asiuwawe,baada ya kumkabidhi ni miezi minane sasa hakuwahi kurudi .
Hawa ni watoto viziwi nao walishiriki mlo
Kikundi cha ngoma cha rugoloire kilitumbuiza watoto na wageni walioudhulia
Ni baadhi ya zawadi mbalimbali ambazo zimekusanywa na jumuia ya Kasibante Redio kutoka kwa wadau mbalimbali kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya watoto
Mcungaji James akiombea chakula
Mzee Rwangisa na mgeni rasmi wakipata chakula
Watoto wakipata chakula
Mtoto huyo ni mlemavu wa macho baada ya kushiba akapumzika kidogo
Mama na mwana
Mkurugenzi wa Kasibante Redio Richard Leo akitoa neno na madhumuni ya kuandaa mlo wa mchana na watoto yatima na walemavu,lakini pia alieleza kuwa utakuwa ni mwendelezo wa kila mwaka kusherekea valentaine kwa staili hii
Mdau Paschazia Barongo nae alishiriki
Mgeni rasmi Balozi Kagasheki akitoa neno la shukrani kwa wate waliochangia kwa hali na mali kuwakumbuka viumbe wa mwenyezi mungu wenye ulemavu wa viungo na watoto wanaoishi katika mazingira magumu,katoa wito kwa jamii nzima kuwajari na kusaidia watoto wenye mahitaji.
Bw Kabantega
Binti huyu hana mikono yake yote miwili, anakula kwa kutumia miguu
Cheza twist...
Chezeee Richard na Jane weweeee
Maka chiiiiniii Tofauuu
Kijana Bale
Picha ya pamoja
Balozi Kagasheki akiongea na watato wanaoishi katika mazingira magumu aliokutana nao nje ya jengo la Kasibante Redio wakati akiondoka eneo hilo
Sunday, 16 February 2014
BALOZI KAGASHEKI AKUTANA NA MACHINGA WA BUKOBA MANISPAA,AWATAKA VIONGOZI WALIOPEWA DHAMANA YA KUONGOZA WANANCHI WASIWE WEPESI WA KUJIBU MAJIBU MEPESE KATIKA MAMBO YA MSINGI YANAYOHUSU MAISHA YA WATU
Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini amekutana na wafanyabiashara ndogondogo(Machinga) wa Manispaa ya Bukoba baada ya kupeleka kilio chao katika ofisi za chama cha mapinduzi Bukoba kutakiwa na uongozi wa Manispaa ya Bukoba kutoka katika maeneo wanayofanyia biashara zao. Balozi Kagasheki akijibu risara yao iliyokuwa imesheheni buguza na adha wanayopata kutoka kwa mgambo na katibu Tarafa amesema ni vizuri viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza na kushughulikia matatizo ya wananchi wawe makini na waache tabia ya kuwa wanatoa majibu mepesi kwa vitu vinavyohitaji ufumbuzi wa tatizo, Mapema katika risara iliyosomwa na mwenyekiti wa umoja huo wa wamachinga walieleza na kuonyesha cheti cha usajili na kutambuliwa na manispaa ya Bukoba.,Balozi Kagasheki ndio akahoji unawezaje kirahisi kabisa kufukuza watu unaowatambua kisheria bila kuwatafutia eneo mbadala la kufanyia kazi,amewahaidi kulifanyia kazi na kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao, Amewasihi na kuwaomba kuwa watulivu na wasikivu wakati swala lao likifanyiwa kazi, amewachangia kiasi cha shilingi milioni kumi ili zitunishe mfuko wao na kuwahaaidi kuwaongezea mtaji zaidi kama watakuwa waaminifu katika kukopeshana na kurudisha katika umoja wao.
Mwenyekiti wa ccm Bukoba mjini Yusuf Ngaiza akieleza jinsi chama kilivyopokea malalamiko yao na sasa wanamkabidhi swala hilo mh mbunge alishughulikie
Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo akisoma risala kwa Mh mbunge
Wafanyabiashara wakimsikiliza mh Kagasheki katika uwanja wa kaitaba Bukoba.
Mh diwani Felician Bigambo kata ya Bakoba (CUF) akimsikiliza Mh Kagasheki
Mwenyekiti wa ccm Bukoba mjini Yusuf Ngaiza akieleza jinsi chama kilivyopokea malalamiko yao na sasa wanamkabidhi swala hilo mh mbunge alishughulikie
Mwenyekiti wa wafanyabiashara ndogondogo akisoma risala kwa Mh mbunge
Wafanyabiashara wakimsikiliza mh Kagasheki katika uwanja wa kaitaba Bukoba.
Mh diwani Felician Bigambo kata ya Bakoba (CUF) akimsikiliza Mh Kagasheki
Subscribe to:
Posts (Atom)