Hii ni picha ya marehemu Alinda aliefariki 13-1-2014 katika hospital ya kagondo akiwa na umri wa miaka 15, alikuwa anaingia kidato cha tatu katika shule ya sekondari Zakia Meghiji iliyoko chato, na tarehe anafariki ndio ilikuwa siku yake ya kurudi shule, Bwana ametwaa jina lako lihimiliwe
Jeni amepoteza mwanae wa kwanza
Lily Tigo akiwa na Bety msibani
Maua Daftari busy na simu msibani ,pembeni chui na London
Bi Zamda
Bw Wilson Mchunguzi akiwa msibani
Majirani wakiwa msibani
Kushoto ni mtoto pekee wa Jeni alibaki
Kulia ni Jeni aliefiwa na mwanae aliekuwa na umri wa miaka 15
Swaiba mkubwa wa Jeni(mfiwa) Bi Pelina
MC Baraka akiwasili eneo la msiba na Bw Yugin Kabendera
Azizi Kachwamba
Msibani maisha yakiendelea
Mmmmm jamani kazi ya mungu haina makosa
Moses Nyama msanii wa kakau Band(kushoto)akiwa na msanii Bk Sande(kulia) wakiwa eneo la msiba
Tuesday, 14 January 2014
RC AMTUMIA KILAINI KUMNASUA MEYA BUKOBA
Hatua hiyo inakuja wakati ambapo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Uttouh, akitarajiwa kuwasilisha ripoti ya ukaguzi wa miradi ya kifisadi katika manispaa hiyo wakati wowote.
Amani aliingia kwenye mgogoro na madiwani wake wakiwemo wanane wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na wenzao saba wa CHADEMA na CUF wakitaka kumwondoa kutokana na tuhuma za kuendesha miradi ya kifisadi.
Baada ya mgogoro huo kuwa mkubwa na CCM ngazi ya taifa kushindwa kuumaliza, hatimaye Kamati Kuu ya chama hicho ilimwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kupitia Wizara ya Tamisemi kufanya ukaguzi maalumu wa tuhuma hizo kupitia kwa CAG.
Oktoba 10, mwaka jana, CAG alianza ukaguzi huo na tayari amekamilisha ripoti yake akisubiri kuikabidhi, lakini kumekuwa na juhudi za makusudi za kutaka kuipotosha taarifa hiyo ili isiwasilishwe kwa madiwani.
Mkuu wa Mkoa ambaye amekuwa mtetezi mkubwa wa Meya Amani, jana aliitisha kikao cha dharura kati yake na madiwani wanane wa CCM wanaompinga Amani na kuwalainisha waondoe tofauti zao ili Baraza la Madiwani lianze vikao vyake.
Wakizungumza na gazeti hili kwa simu jana kutoka mjini Bukoba, baadhi ya madiwani hao walieleza kushangazwa na kitendo hicho cha Massawe ilhali wanasubiri ripoti ya CAG iwasilishwe ili wajue kile kilichobainishwa kwenye uchunguzi.
“Sisi tumemuuliza mkuu wa mkoa, wakati mgogoro huo ukiendelea hadi leo ambapo vikao havifanyiki, hao viongozi wa dini na wazee walikuwa wapi kutafuta muafaka hadi wangoje CAG amalize ukaguzi na ripoti inakaribia kutolewa ndipo waje kutusuluhisha?
“Kwanza, kama tungekubali huo mtego wao wananchi wetu wangetushangaa na kamwe wasingetuelewa kuona kile tulichokipigania kinakaribia kutolewa hadharani kujua ukweli halafu tunageuka,” alisema mmoja wao.
Tanzania Daima lilidokezwa kuwa Massawe alijaribu kuwasihi madiwani hao bila mafanikio akidai kuwa ripoti ya CAG haipo na kwamba kama itakuwepo huenda ikachelewa kwa muda wa miezi miwili, hivyo kuwataka waingie kwenye vikao vya baraza kupitisha bajeti.
“Baada ya kuona tumeshikilia msimamo wetu, Massawe alitumia ubabe kumwagiza Katibu Tawala aitishe vikao hivyo kwa nguvu ili tutakao kaidi tuchukuliwe hatua za kinidhamu za kuwajibishwa.
“Sasa tumemtaka atueleze kama yeye yuko juu ya Rais Jakaya Kikwete, maana baada ya yeye kushindwa kumaliza mgogoro wetu ndipo kupitia kwa Waziri Mkuu alimwagiza CAG aje kukagua. Sisi tumemwambia kwamba tunataka ripoti zote ile ya Abbas Kandoro na CAG na si vinginevyo,” alisema diwani mwingine.
Kikao cha jana kilihudhuriwa na Alexander Ngalinda wa Kata ya (Buhembe), ambaye pia ni Naibu Meya, Yusuf Ngaiza (Kashai), ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya, Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo), Richard Gaspar (Miembeni) na Murungi Kichwabuta wa Viti Maalumu.
Balozi Kagasheki na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo) hawakuweza kuhudhuria kikao hicho kutokana na kuwa katika majukumu mengine.
Miradi iliyokuwa inalalamikiwa ni upimaji wa viwanja 5,000 unaodaiwa mkopo wake wa sh bilioni 2.9 kutoka Mfuko wa Dhama ya Uwekezaji (UTT) haukufuata taratibu, na wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.
Ipo pia ujenzi wa soko ambapo meya anadaiwa kusitisha malipo ya ushuru na kutaka kuwaondoa wafanyabiashara bila kufuata utaratibu.
Anatuhumiwa pia kukopa sh milioni 200 kutoka Benki ya Uwekezaji (TIB) bila kibali cha Baraza la Madiwani. Vile vile alitoa taarifa kwenye kikao cha baraza hilo kuwa TIB iliwapa ruzuku ya sh milioni 90, lakini hakueleza misingi yake.
Upo pia mradi wa kuosha magari ambao unadaiwa kutumia kiasi cha sh milioni 297 zinazotiliwa shaka. Ameshindwa pia kutoa mchanganuo wa mapato na matumizi ya mradi kiasi cha sh milioni 134, za ujenzi wa kituo cha mabasi.
Sunday, 12 January 2014
MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAFANA
Rais wa Zanzibar
Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati akiingia
kwenye uwanja wa Amani na gari la wazi kwenye maadhimisho ya miaka 50
ya Mapinduzi.
Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi vya gwaride kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amani.
Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
Askari wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
Kikosi cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi.
Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi vya gwaride kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amani.
Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
Askari wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
Kikosi cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi.
ASKARI POLISI NA ASKARI MAGEREZA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA MBEYA
Mbele ni mshitakiwa wa nne Mbaruku Hamis akiingia mahakamani
Kutoka kushoto ni mshitakiwa wa pili Elinanzi Eliabu Mshana, Mshtakiwa wa nne Mbaruku Hamis, Mshita
kiwa
wa tatu Juma Mussa ambaye aliyekuwa Askari Magereza kwa Cheo cha Sajini
, Anaefuatia ni Mshtakiwa wa kwanza PC James aliyekuwa Askari Polisi
Wilaya ya Mbeya, na wa mwisho ni Mshitakiwa wa Tano Amri Kihenya .
Wa kwanza kushoto aliye vaa shati la Draft ni Dereva Ezekia Matatila (34) pamoja na wasikilizaji
Moja ya Gari lililotumika kufanya uharifu wa unyang'anyi wa kutumia silaha
Washitakiwa wanne kati ya watano kutoka kushoto juu hadi wa nne wakiwa wanatoka mahakamani chini ya ulinzi mkali.
Mwenye Jaketi la Njano ndiye Mshitakiwa namba moja PC James
Katikati ni Mke wa mshitakiwa wa tatu ambaye ni Askari Magereza Sajini Juma Mussa, Hata hivyo mwanamke huyo alizirai mahakamani wakati mumewe akiwa kizimbani.
**********************************
ASKARI
wawili wa jeshi la Polisi na Magereza pamoja na watu watatu ambao ni raia wa
kawaida wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbeya wakituhumiwa kwa
ujambazi wa kutumia silaha.
Watuhumiwa
hao watano kwa pamoja walifikishwa jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya
Wilaya ya Mbeya, Michael Mteite wakituhumiwa kwa kosa moja la unyang’anyi wa
kutumia Silaha kinyume cha Sheria kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Mshitakiwa namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302 wa
Wilaya ya Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada
ya kuhukumiwa kijeshi.
Aliwataja
wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela
Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B 500 Sajenti Juma Mussa(37) wa
Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa Iyela na Amri Kihenya(38)
Mkazi wa Iyela.
Akisoma
mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite, Mulisa
alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 3, Mwaka huu majira ya saa
11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya Mbeya Chunya.
Alisema
watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kulizuia gari aina ya Pick Up
lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34) Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya
ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sreedhar Pasupelet(38)
mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo mawili ambayo ni GX 100 Toyota
Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo lilikuwa na namba za Chesesi GX
6011832 AINA YA Grand Mark II.
Aliongeza
kuwa mbinu iliyotumika ni watuhumiwa ni watuhumiwa hao kutega magogo barabarani
huku wakiomba msaada kwa madai kuwa magari yao yameharibika na ndipo baada ya
wahanga kusimama waliwapora vitu vyao wakiwa na mapanga ambavyo ni pesa
shilingi Milioni 3.5, Mabegi matatu yenye nguo mbali mbali yenye nguo, Kompyuta
mpakato, simu aina ya Sumsung yenye thamani ya Shilingi Laki mbili pamoja na
simu ya Dereva aina ya Tekno ambayo aliitambua Mahakani na kutumika kama
kielelezo.
Hata
hivyo watuhumiwa wote kwa pamoja walikana kuhusika na matukio hayo ambapo
upande wa Mashtaka ulileta Shahidi mmoja ambaye ni Dereva wa Pick up Ezekia Matatira
ambaye aliwatambua washtakiwa wote watano na kuiambia mahakama kuwa siku hiyo
ya Tukio aliagizwa na Bosi wake kwamba awapeleke wageni Chunya na ndipo
alipotekwa katika eneo hilo huku watekaji wakiagizwa na Maaskari na yeye kufungwa pingu na kutishiwa na panga.
Aidha kutokana na kesi hiyo Hakimu Mteite aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 15, mwaka huu ambapo upande wa Mashtaka utaleta mashahidi wengine huku watuhumiwa wakirudishwa Rumande baada ya dhamana yao kufungwa.
Saturday, 11 January 2014
CAG KUANIKA UFISADI BUKOBA
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amesema wiki ijayo atakwenda mkoani Kagera kuweka wazi yaliyobainika katika ripoti ya ukaguzi wa tuhuma za ufisadi zinazoikabili Halmashauri ya Bukoba.
Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Utouh alisema ukaguzi huo umekamilika na wanakwenda Bukoba kuweka wazi kile waliochokibaini.
Alisema kwa utaratibu wa ukaguzi, lazima kifanyike kikao cha awali kabla na baada ya ukaguzi ili kuweka hadharani walichokibaini.
“Kabla ya kukabidhi ripoti hii ni lazima kwanza twende Bukoba kufanya kikao ili kuwaeleza tulichokibaini katika ripoti hiyo, na baada ya kumaliza kikao hicho ndiyo utaratibu wa kukabidhi utafuata.
“Hiyo inafanyika kwa utaratibu na sheria za ukaguzi zinavyohitaji,” alisema.
Katika uchunguzi huo timu ya wakaguzi ilifanya kazi kwa kuegemea hadidu 14 za rejea huku wakijikita kwenye maeneo husika kwa mwaka wa fedha 2010/11 hadi 2012/13.
Kwa mujibu wa Utouh, hadidu hizo ni kuchunguza usahihi wa utaratibu uliotumika kumpata mwekezaji wa kituo cha kuoshea magari, Kampuni ya ACE Chemicals Ltd.
Kuchunguza uhalali wa nyaraka na kiasi kilichowekezwa cha sh milioni 297 kwenye mradi huo, kuchunguza tatizo na sababu za viwanja 800 kutogawiwa kwa wananchi waliochangia gharama za upimaji, mradi wa upimaji wa viwanja 5,000, mradi wa ujenzi wa soko na mradi wa kujenga kitega uchumi.
Aliongeza kuwa nyingine ni mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi, ujenzi wa chuo cha ualimu, kituo cha maarifa na ujenzi wa bwawa kwa ajili ya utalii.
Yalikuwepo pia masuala mengine ya matumizi ya fedha yanayoashiria ubadhirifu na wizi au ufujaji wa mali za halmashauri na kutoa ushauri kwa serikali kuhusu namna bora ya kuimarisha usimamizi wa mapato katika halmashauri hiyo.
Ukaguzi huo pia umegusa mradi wa maji wa Benki ya Dunia kwa ajili ya Kata ya Nyanga, kiwanja cha Shule ya Msingi Kiteyagwa, barabara ya kupitia Kagondo Kaifu hadi Kagondo Karagulu, ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Bukoba na Ilani ya Uchaguzi.
Ofisi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda ilimuomba CAG kufanya uchunguzi wa halmashauri hiyo ili kumaliza mgogoro uliodumu miaka miwili hatua iliyosababisha wananchi wa halmashauri hiyo kushindwa kupata maendeleo.
Timu ya wakaguzi ilianza kazi Septemba 30, mwaka jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)













