Bw harusi akijiandaa kuelekea kwao na bi harusi kufunga ndoa
Pilau ya nguvu...
Msosi kwanza mengine yatafuata..
Kaka mkubwa Ernest katika hekaheka za kufanikisha sshughuli
Sudi Karatasi akiwa na Shafi
Wa mama walitokelezea
Bw harusi akiwapa zawadi kikundi cha kaswida
Mama mzazi wa Bi harusi
Kulia Shekhe Mustapha Sadick akiwa na Babu wa bibi harusi Mzee Galiatano
Baba wa bi harusi akitoa neno la shukrani
Bi zena katika pozz la mtandio
Hayawi hayawi leo yamekuwa
Sauda miaka 12 si mchezo , leo imekuwa
Vaa kofia mke wangu
Bw Ramadhani Kambuga akiwa na mkwewe Bi Sauda Sadick Galiatano baada ya kufunga ndoa
Ongereni sana maharusi wetu
Tuesday, 24 December 2013
Monday, 23 December 2013
HAPPY BIRTHDAY JAMAL KABIGUMILA KALUMUNA (JAMCO)
Ni siku ya kumshukuru sana mwenyezi mungu mwingi wa rehema na upendo mkubwa kwa viumbe wake, leo ni siku ya pekee katika maisha yangu, ni siku ambayo ilikuwa ni furaha kwa wazazi wangu Dauda Kalumuna na Khadija Elias Nasibu kwa kumpata mtoto wa kiume, Nawashukuru sana wazazi wangu kwa kunielea , kunisomesha na kunipa msingi wa maisha, Kipekee nitumie nafasi hii kumuombea mama yangu mzazi ambae ni marehemu mungu amlaze mahali pema peponi, Mama nilikupenda sana, nakukumbuka na kikubwa nazingatia uhusia na maelekezo yako yote kwa wadogo zangu, ndugu , jamaa , marafiki na Familia yangu,KWELI MUNGU NDIO KILA KITU, umenitendea mengi ambayo ni kama miujiza katika maisha yangu, Naishukuru kipekee familia yangu, wadogo zangu, jamaa wote na marafiki kwa msaada mkubwa walionipa katika maisha yangu ya kila siku mpaka naifikia tarehe ya leo 24-12-2013. asanteni sana.
BEN MULOKOZI AKIPENDEZA NDANI YA JAMCO BARBER SHOP
Ni gari ya Ben Mulokozi ikiwa nje ya likimsubiri akifanyiwa usafi ndani
Ben Mulokozi kiti cha kwanza kulia akifanyiwa usafi
Mahusiano na kufaamiana zaidi ni katika maeneo kama haya, kijana Ruta amelizingatia hilo
Karibu Jamco Barber shop kwa huduma nzuri, Uongozi wa Jamco Video Production na vitengo vyake inawatakia heri ya x-mas na mwaka mpya.
Ben Mulokozi kiti cha kwanza kulia akifanyiwa usafi
Mahusiano na kufaamiana zaidi ni katika maeneo kama haya, kijana Ruta amelizingatia hilo
Karibu Jamco Barber shop kwa huduma nzuri, Uongozi wa Jamco Video Production na vitengo vyake inawatakia heri ya x-mas na mwaka mpya.
Sunday, 22 December 2013
MSHINDI WA MANYWELE KIGOLI 2013 HUYU HAPA
MREMBO Suzie jana alishinda mpambano wa Manywele Kigoli 2013 uliofanyika ndani ya ukumbi wa Business Park uliopo Makumbusho jijini Dar alipowabwaga wenzake aliokuwa akichuana nao katika kukata viuno.
Suzan akiwa kwenye gari lake muda mfupi baada ya kutwaa taji hilo.
Msanii wa Bendi ya Malaika, Christian Bella, akitumbuiza kwenye mashindano hayo.
Ally ‘Nipashe’ akiserebuka na mrembo jukwaani baada ya kuombwa kutumbuiza mahali hapo.
Mshindi wa kwanza , wa pili na wa tatu wakiwa katika pozi.
Baadhi ya mashabiki wakishuhudia shindano hilo.
Vigoli wakiserebuka.
SOMA HOTUBA YA MH.ZITTO KABWE MJINI KIGOMA LEO
HOTUBA YA MH ZITTO Z. KABWE - KIGOMA – 21 DESEMBA 2013
Leo nina furaha kubwa sana kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbani kuwasalimu wananchi wenzangu! Na hii si salamu za kawaida bali nawasalimu kwa salaam za demokrasia, uadilifu, uzalendo na uwajibikaji. Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Na popote niendapo najivunia kujitambulisha kama Mtanzania; kama mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la Ujiji.
Tuna mengi ya kujivunia kama taifa lakini Ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika historia. Watu wa Ujiji mlipokea harakati za kudai uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya uhuru yalipoanza. Watu wa Ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Na Jimbo la Kigoma Mjini ilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kabisa kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995.
Kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994. Wakati Watanzania wengine wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyoanzishwa, watu wa Ujiji, watu wa Kigoma hamkusita kupokea mabadiliko. Wengi wamepoteza maisha yao, wengine kazi zao na wengine hata ndoa zao katika kupata mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu. Nawataka msichoke. Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha demokrasia katika nchi yetu haijaisha na inahitaji uvumilivu, kusameheana na kuaminiana.
Na nchi yetu Tanzania ni nchi inayoonyesha uwezo mkubwa katika kupendana, kuaminiana, kuvumiliana na hata kusameheana. Na haya si maneno tu ambayo ninayazungumza kama mwanasiasa. Hii ni hali halisi na maisha niliyoyaishi kwa mifano nilipokuwa ninakua na kusoma katika shule ya Msingi Kigoma na baadaye Shule ya Sekondari Kigoma. Malezi yangu yalikuwa yanaongozwa na jamii nzima ya Kigoma.
Nimekuwa nikiwaeleza rafiki zangu niliokutana nao kwenye masomo na kwenye siasa kwamba nimeanza kuvaa viatu kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la tatu. Viatu hivyo viliitwa 'asante Salim' vilivyokuwa vinatengenezwa na Kampuni ya Bora Shoes. Vililinunuliwa na mama Coretha Furugunya ambaye tulikuwa tunakaa mtaa mmoja wa Kisangani Mwanga.
Mama Coretha hakuninunulia viatu kwa sababu alikuwa ana uwezo mkubwa, la hasha! Alifurahishwa na matokeo yangu ya mitihani ya darasa la pili kwenda la tatu. Ninaamini kitendo cha mama huyu ni ushahidi wa uungwana, upendo na hata uwajibikaji ambao tunao sisi watanzania. Uwajibikaji kwani alichukua jukumu kunilea ingawa hakuwa mzazi wangu, lakini aliona kuwa kama mwanajamii ana nafasi kubwa katika kuwaendeleza watoto wote.
Jamii hii ya watu wa Kigoma ilinifunza kuwa nikijitahidi na kukazana kwa bidii kwenye masomo na majukumu, nitafanikiwa. Siwezi kusahau somo hili katika maisha yangu na ni somo hili ndilo limenifanya nijitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu kuwatumikia kwa uadilifu na mafanikio ya hali ya juu sana.
Nikiwa nimejaa matumaini haya kuhusu wananchi wenzangu, leo nataka niwakumbushe kwa nini kama jamii tulichagua kufuata njia ya demokrasia. Demokrasia ina maana pale ambapo inatumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wananchi. Maisha yanayotakiwa ni yale yanayomwezesha mwananchi kupata huduma zake stahili kama Elimu, Afya, Maji na miundombinu. Demokrasia haina maana pale wananchi wanakufa njaa kwa kukosa ajira na kukuza umasikini.
Demokrasia inahusu maendeleo. Tumejitahidi kwa upande wetu kuondoa mkoa wa Kigoma kutoka mikoa isiyo na miundombinu kabisa ya maendeleo mpaka kuwa mkoa unaotumika kama mfano kwa miradi mingi ya Maendeleo ikiwemo Daraja la Malagarasi, Uwanja wa ndege wa Gombe-Mahale, barabara za lami na upanuzi wa Bandari, ujenzi wa bandari ndogo mpya na ujenzi wa kituo cha Usafirishaji Mwandiga.
Asije mtu akasema yeye ndio kafanya haya. Haya ni matunda ya nyinyi watu wa Kigoma kupokea demokrasia na bila woga kuchagua viongozi wenu bila kujali vyama bali kwa kuangalia uwezo. Haya ni matunda ya viongozi wenu kupaza sauti yenu kwenye baraza la Taifa, Bunge. Haya ni matunda ya uvumilivu wenu na uamuzi wenu wa kutaka maendeleo. Juhudi hizi lazima ziendelezwe kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa nafasi ya mkoa wa Kigoma katika uchumi wa Tanzania inaonekana dhahiri na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa kituo cha biashara katika nchi za maziwa makuu.
Lakini tukumbuke pia kuwa Demokrasia ni Uwajibikaji. Katika kipindi cha utumishi wangu kwenu,kutokana na malezi niliyoyapata kutoka kwenu,nimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Serikali inawajibika kwa Wananchi. Nakumbuka wakati napambana kuhusu sheria mbovu ya madini kuna watu hapa nyumbani walisema 'sasa huyu kawa mbunge wa Taifa' lakini watu wengi zaidi wakasema tumemtuma Dodoma kusemea Watanzania wote na sio Kigoma tu. Tuliweza ndani ya miaka mitano kufanya mabadiliko makubwa sana kwenye sera ya Madini na sheria ya madini ambapo baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayafikiriki sasa yametungiwa sheria ikiwemo Serikali kuwa na hisa kwenye migodi, Tanzanite kumilikiwa na Watanzania sio chini ya asilimia 50 na kuzuia kabisa wageni kuchimba vito vya thamani. Uwajibikaji ulipelekea kumshinikiza Rais kufanya mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri kwa kuwafukuza mawaziri wanane mwaka jana.
Hii ilitokana sio tu na hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bali pia ushiriki mkubwa wa wananchi kupitia simu na mitandao ya kijamii ambapo wabunge walishinikizwa kuweka saini kwenye karatasi za kumtoa Waziri Mkuu. Toka wakati huo kumekuwa na utaratibu sasa ambapo wabunge hawaoni taabu kutaka uwajibikaji waziwazi ili kuzuia ubadhirifu wa fedha za Umma. Ni hivi jana tumeshuhudia mawaziri wanne wamejiuzulu na kufukuzwa kazi kutokana na kashfa ya operesheni Tokomeza ujangili iliyoibuliwa na ripoti ya kamati ya bunge. Mabadiliko haya ni hatua muhimu katika kuimarisha demokrasia yetu. Pamoja na matunda haya mengi mazuri lakini bado kuna changamoto katika juhudi zetu.
Changamoto kubwa tuliyonayo wananchi ni kukosekana kwa imani katika demokrasia yetu.
Kutoaminiana. Ni dhahiri kuwa kutoaminiana katika nchi yetu kumekuwa kwa kiasi kikubwa. Taarifa za kitafiti zinaonyesha kuwa katika kila Watanzania kumi, wanane hawaaminiani. Ni changamoto kubwa sana. Wananchi wameacha kutuamini wanasiasa na wanasiasa wameacha kuaminiana wenyewe kwa wenyewe. Hivi sasa uongo umegeuzwa kuwa ukweli na ukweli umekuwa ni uongo. Hivi sasa ukitaka kuwa mwanasiasa maarufu inabidi ujue kudanganya na ukitaka kuitwa mwanasiasa msaliti inabidi uwe msema kweli. Kukosekana kwa uaminifu na kuaminiana imekuwa ni kansa katika siasa zetu.
Itachukua muda mrefu sana kujenga demokrasia imara katika nchi yetu kama hatutapata jibu la changamoto hii ya kutoaminiana na kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo. Hivi sasa ukweli umekuwa unatengenezwa badala ya kutafutwa. Ni majanga! Juzi bungeni Mwanasheria Mkuu wa Serikali alielekeza shutuma kwangu kwamba sikushirikiana na kamati maalum iliyoundwa na Bunge kufuatilia mabilioni ya uswisi na kwamba chini ya kiapo nilisema sina majina ya watu wenye akaunti huko Uswisi. Huu ulikuwa ni uongo. Ni uongo kwa sababu niliitika wito wa kamati hata nilipokuwa katika mafunzo ya mgambo huko Tanga na nilikutana nao mara nne. Ni uongo kwa sababu niliwapa wajumbe wa Kamati Maalaum maelezo na taarifa nyingi sana kuhusu utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na umiliki wa mali nje ya nchi kinyumecha sheria.
Ni uongo kwa sababu mimi kutotaja majina haya haina maana sina majina, bali ni kwamba ninaheshimu utaratibu na nimeachia vyombo husika vikamilishe uchunguzi. Kwani mimi kama mtu binafsi nikianza kuchukua majukumu ya taasisi ninaweza kutia dosari harakati hizi muhimu na hata kupelekea mchakato mzima kuvurugika. Sitaingia mtego huu! Lakini hatua hii ya Mwanasheria Mkuu imenipelekea kujiuliza maswali mengi kwa mfano uongo kama huu ulifanywa kwa malengo gani? Na ninajikuta hata mimi ninaingia katika hali ninayoilalamikia ya KUTOAMINIANA.
Lakini mtambue pia kuwa kutoaminiana kunaleta kutovumiliana. Hivi sasa kuwa na mawazo tofauti katika vyama vya siasa au hata asasi za kijamii ni uhaini. Lakini bila kuenzi tofauti za mawazo hatuwezi kujenga vyama imara wala Taifa imara. Demokrasia imara ni zao la tofauti za mawazo na uhuru wa mawazo. Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyorutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo, tutajenga Taifa lenye watu wenye kuogopa na waliojaa woga. Wanachama wanapoogopa uongozi ni udikteta, lakini uongozi unapoogopa wanachama ni demokrasia. Bila demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa Taifa la kidikteta. Lazima vyama vya siasa, viongozwe kwa namna ile ile ambayo Taifa litaongozwa.
Demokrasia bila kuaminiana, demokrasia bila kuvumiliana sio demokrasia ya kweli.
Juzi nilipoingia Bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanayoendelea ndani ya chama chetu nilikaa pamoja na mbunge Tundu Lissu. Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo. Hii ni kwa sababu sina chuki na mtu yeyote yule. Mmenifunza kutojenga chuki na watu na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha. Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti na hatimaye kutafuta suluhu ya pamoja. Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tunasahau kwa maksudi. Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha ya wananchi na sio malumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa. Siasa si kuwekeana chuki na kuonyeshana ubabe.
Na hapo ni muhimu muelewa wanaKigoma mnapoambiwa kuwa eti ninapofuatilia mabilioni ya Uswisi ninatafuta umaarufu, ni uongo! Mnaposikia eti kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki na kujitafutia umaarufu, ni uongo! Kinachonisukuma kufanya vyote hivi ni ninyi. Ninasukuwa kila ninapowaona watoto bado wanatembea bila viatu;kila ninapoona akina mama wanapoteza maisha yao katika uzazi;kila ninapoona vijana ambao hawana uhakika wa kupata hata mlo moja kwa siku kwa kukosa kazi; ninapoona wazee wa Kigoma kukosa hata shilingi mia moja kununua chai asubuhi. Ninawaona si wanaKigoma bali mamilioni ya watanzania wakiishi katika hali hii. Alafu nalinganisha na taarifa tunazozipata kuhusu ufujaji na utoroshwaji wa pesa zetu.
Hebu sasa linganisheni na ukweli kuwa ripoti ya kimataifa iliyotolewa hivi karibuni imeonyesha kuwa mwaka 2010 pekee, jumla ya dola za kimarekani milioni 1315 (bilioni 1.3), yaani shilingi trilioni 2,113,930,000,000 (sh trilioni 2.1) zilitoroshwa kutoka nchini Tanzania. Mwaka 2011 kiasi cha dola za kimarekani milioni 817 yani shilingi za kitanzania zipatazo trilioni 1,315,370,000,000 (trilioni 1.3) zilitoroshwa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa jumla ya fedha za Watanzania zilizotoroshwa nje ya nchi katika miaka kumi iliyopita zilifikia dola za kimarekani milioni 4526 (bilioni 4.5) sawa na shilingi za kitanzania trilioni 7,286,860,000,000 (trilioni 7.3).
Nimewatajia hapa namba chungu nzima na matrilioni na mabilioni hayaleti maana. Lakini hii ina maana kwamba kiasi cha pesa zilizotoroshwa katika miaka 10 pesa - robo yake tuingeweza kujenga barabara ya lami ya kiwango cha juu kabisa kutoka Kigoma mpaka Dar-es-salaam! Pesa hizi zingeweza kuajiri na kuwalipa vizuri walimu, madaktari na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha tunapata huduma bora na kutengeneza ajira bora kwa vijana wetu. Pesa hizi zingeweza kununua madawa muhimu na kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama tunaowapoteza kila mwaka wakati wa uzazi. Pesa hizi zingeweza kuwanunulia watanzania wote si watoto tu angalau pea 10 ya viatu. Sasa nikitafakari haya siwezi kuchapa usingizi mnono na kufumbia macho utoroshwaji wa fedha au matumizi mabaya ya fedha za umma kwa njia ya sisi wabunge kujilipia posho! Hapana! Nafsi yangu hainiruhusu kukaa kimya kwa kuogopa kuitwa mbinafsi au msaliti!
Lakini naomba niwasihi kuwa katika nyakati kama hizi za changamoto za kisiasa jambo la msingi kuliko yote ni kutulia maana hakuna linalotokea bila sababu. Licha ya kwamba kuna watu wengi wanapaza sauti zao katika mambo haya lakini pia kuna wengi zaidi ambao wapo kimya lakini wana mawazo yao, ndani na nje ya chama chetu;ndani na nje ya Serikali na ndani nanje ya nchi yetu. Ndio maana lazima kuibadili nchi yetu ili kuweza kuhakikisha kila raia anakuwa na fursa ya kutoa mawazo na fikra zake zinakuwa huru.
Maisha ni mabadiliko; mabadiliko hayana ukomo; mabadiliko hayazuiliki kwa sababu bila mabadiliko hakuna ukuaji, bila mabadiliko hakuna maendeleo. Mabadiliko ni kiu kikubwa cha Tanzania kwa sababu mabadiliko huleta matumaini. Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu sisi vijana wa kizazi hiki kipya. Siasa za kizazi kipya cha viongozi ni siasa za majawabu ya kero za wananchi. Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha; ni siasa za kuaminiana na kuheshimiana hata pale mnapopingana kimawazo. Ninataka tujenge siasa mpya Tanzania;siasa za mabadiliko; siasa zinazojenga matumaini ya kweli;siasa zinazowajali na kuwajengea uwezo wananchi wa Tanzania. Mungu ibariki Tanzania.
LOWASSA ASHIRIKI TAMASHA LA WAENDESHA BODABODA JIJINI DAR
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akiwahutubia Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za
kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo
pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye
Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa alikuwa ni
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofana sana.
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza machache
kwenye Tamasha hilo kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Tamasha
hilo,Mh. Edward Lowassa (kulia).Katikati ni Kamanda wa Polisi Kitengo
cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga.
Kamanda
wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R.
Mpinga akizungumza akitoa hotuba yake mbele ya Vijana waliojiajiri kwa
kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda
wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la
Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe akisoma
Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani)
wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja
vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea
Risala ya Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Kutoka kwa
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael
Roewe.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Benki ya FNB kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa
Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Mfuko wa PSPF kwa kutoa Mchambo mkubwa
kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea
Zawadi Kutoka kwa Mwenyekiti wa Muda wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda
Mkoa wa Dar es Salaam,Said Magamba.
Salamu kwa waendesha Bodaboda.
Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya wanaounda kundi la KIBEGA,wakitoa Burudani mbele ya Waendesha Bodaboda hao.

Sehemu ya Waendesha Bodaboda hao wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi.
Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo mapema leo.
Mgeni
Rasmi katika Tamasha la Waendesha Bodaboda Mkowa wa Dar es Salaam,Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka
viwanjani hapo huku Vijana Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam
wakimsindikiza kwa shangwe.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwaaga
Vijana wa Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiondoka
viwanjani hapo huku shangwe zikitawala viwanjani hapo.
Vijana wa Bodaboda wakilisukuma gari la Mh. Lowassa ikiwa ni sehemu ya Furaha waliokuwa nayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)



















