Sunday, 1 December 2013

BUKOBA VETERAN WAFANYA BONAZA LA KUFUNGA MWAKA LEO KATIKA UFUKWE WA KIROYERA,WAZINDUA RASMI T,SHIRT ZAKE,BURUDANI ZATAWALA ,WADHAMINIWA NA TBL


                                                Ilikuwa na kujichanganya kila conner
                                                              Hawa nao kwa raha zao
                                     Upepo ziwa victoria ni raha kama ulaya au zaidi ya ulaya
 BW Sizya anawakilisha TBL ambao ndio wamedhamini Bonaza hili,kupitia bia ya safari Nani mtani jembe
 Mwenyekiti wa Bukoba Veteran Ernest Nyambo akiongea na watu wote waliofika katika Bonanza
                             Afisa utamaduni manispaa ya bukoba akipongeza wana Veterani
                            Mwenyekiti akimkabidhi T,shirt mgeni alitokea wizara ya utamaduni na michezo
                                Bonanza mpaka kuogera, Willy Kiroyera kwa raha zake
                                                     Chezee Willy weweee
                                                                 Wazee wa Gas
                             Ikafunguliwa shampein kuzindua rasmi Tshirts za Bukoba Veteran
                                                     Mama Mwebesa akiyarudi mayenuu

                                                        Sued Kagasheki katika pozz
                                  Baada ya kula na kushiba sasa ni wakati wa TBL
                                    Mtoto tangu utoto mweke karibu na raha jamaani
                                                                            Wazee wa busara
                                                            Matete na bia yake mkononi
                                               Muziki mkubwa wa TBL, watu wakiserebuka
                              Mwarabu maeneo kama haya achezi mbali na hasa kama wamekaa jinsia ile......
                                    Mtu na mkodomi wake au mtu na shemeji yake
                          Ongereni wana Veteran Bukoba kwa Bonanza la kufunga mwa 2013

INTER COLLEGE BASH BUKOBA YAFANA,WANACHUO WA WAONYESHA UWEZO WAO KATIKA KUIMBA NA FASHION SHOW, WALKGURD HOTEL ILIKUWA SHANGWE

                      Mmoja ya wasanii kutoka chuo cha saut akionyesha uwezo wake
 Kamanda mstaaf kanda ya Dar  Kamanda Tibaigana wa pili kulia nae alikuwepo
                                                                Wakutubi katika pozz
                                                                          Full shangwe.....
 Bw SIZYA kulia na Bw Kahabuka wakiwakilisha TBL kama wadhamini kupitia bia ya safari
                                Bonge la jukwaa la TBL, kila kitu kilifanyika hapo
                                   Ma Mc walioendesha shughuli nzima, si mchezo walimudu
                                                                             Mmmmmm
                                                 Ni wakati wa kuonyesha mavazi tofauti
                                                    Kama kawaida bloggers tulikuwepo
                                                Nani mtani jembe walitoa zawadi kibao
                                                                Mmmm wanachuo noma
                                                                     Ilikuwa poa sana

                                                                         Vi mwanaaaa
                                                     Wanaonyesha vazi la harusi
                                                  Washiriki wote wa mavazi picha ya pamoja
                                                          Nani mtani jembe, utajaza mwenyewe























Friday, 29 November 2013

FIFA WAFUNGUKA BAADA YA UWANJA WA KOMBE LA DUNIA KUPOROMOKA BRAZIL



SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) imesema halina mpango wa kuhamisha michuano ya Fainali ya Kombe la Dunia 2014 kutoka nchini Brazil ingawa nchi hiyo imepata changamoto katika maandalizi ya michuano hiyo.
Wafanyakazi wawili walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na nguzo ambazo ziliharibu uwanja wa Corithians ulio mjini Sao Paulo.
Timu ya taifa ya Brazil inatarajiwa kucheza mechi ya ufunguzi ya Kombe la dunia katika uwanja huo wenye uwezo wa kuwa na watazamaji 65,000.
Vyanzo vya habari vya juu ndani ya Shirikisho hilo vimeendelea kusisitiza kuwa hakuna mbadala kutokana na kutokea kwa ajali hiyo.
Brazil ilikiri kuwa inafanya jitihada za kumaliza ujenzi wa viwanja 12 kwa ajili ya michuano hiyo, sita kati ya hivyo ipo tayari kwa ajili ya michuano ya kombe la shirikisho.
Ajali iliyotokea siku ya Jumatano ni ya tatu kusababisha kifo katika viwanja vitakavyopigiwa kipute cha kombe la dunia. Wafanyakazi wengine wawili walipoteza maisha kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Uchunguzi umeanza hii leo kubaini chanzo cha ajali mjini Sao Paulo.

Wednesday, 27 November 2013

MAITI HUFUKULIWA MAKABURINI ILI KUBADILISHWA NGUO HUKO INDONESIA


Pichani ni baadhi ya wafu waliofukuliwa kaburini na kuvishwa nguo Indonesia.

KILA mwaka huko Tana Toraja, Indonesia, wafu (au maiti) hufukuliwa kutoka makaburini ili kubadilishwa nguo. Watu wa eneo hilo wa kabila la Toraja wana mila za ajabu kuhusu vifo na maisha yanayofuata baada ya mtu kufa.
Wao mtu akifa hutakiwa kuzikwa katika eneo alilozaliwa na si lazima azikwe katika eneo alilofia.
Idadi kubwa ya watu wa eneo hilo ni Wakristo, wanaofuata ni Waislam na wengine ni Wapagani ambao wanajulikana kwa imani au madhehebu ya Aluk To Dolo yaani “Njia ya Mababu”.
Torajan huishi katika maeneo ya milimani na hawataki kujulikana sana katika jamii, japokuwa wana mila na desturi zao zilizoenea katika jimbo la Sulawesi.

Tuesday, 26 November 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA NCHI WANACHAMA WA SHIRIKISHO LA VIWANDA VYA UTENGENEZAJI NGUO KWA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA (CAPA)


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Nchi Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji Nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika,lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jarida la Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika (CAPA Journal), wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha. Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya CAPA,John Kondoro.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya Kinyago kutoka kwa Makamu wa Mwenyekiti wa CAPA wa Kanda ya Afrika Magharibi, Prof. Daniel Nyarko, baada ya kufungua rasmi Kongamano la Nchi Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji Nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika,lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa nne kushoto), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya CAPA,John Kondoro (kushoto kwa Makamu) na baadhi ya viongozi wa CAPA, wakifurahia kwa pamoja baada ya kuzindua rasmi Jarida la Wanachama wa Shirikisho la Viwanda vya Utengenezaji nguo kwa nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola Barani Afrika (CAPA Journal), wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo lililoanza leo katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakiwa makini kumsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akisoma hotuba ya ufunguzi.

Monday, 25 November 2013

CHUJI, CANNAVARO, MSUVA NA JERRY TEGETE WAONGEZA MIKATABA YANGA - KUBAKI JANGWANI MPAKA 2016


Wachezaji watano wa timu ya Young Africans wameongeza mikataba ya muda mrefu ambapo sasa wataendelea kuitumikia klabu yenye maskani yake mitaa ya Twiga/Jangwani mpaka mwaka 2016, hili limefanywa na uongozi kwa mapendekezo ya benchi la ufundi.

Wachezaji ambao mpaka sasa wameshaongeza mikataba ya kuitumikia klabu ya Young Africans ni walinzi Kelvin Yondani (2014-2016), Nadir Haroub "Cannavaro" (2014-2016), kiungo Athuman Idd (2014-2016), mshambuliaji Saimon Msuva (2014-2016) na Jerson Tegete (2014-2016).

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya Young Africans Abdallah Bin Kleb amesema hao ni baadhi tu ya wachezaji ambao wameshamaliza taratibu zote na kusaini mikataba mipya itakayowafanya waitumikie Yanga mpaka mwaka 2016.

"Tupo katika mazungumzo ya mwisho na wachezaji wetu wengine, mazungumzo yanaendelea vizuri na tunaamini muda si mrefu nao tutakua tumeshamalizana nao ili waweze kuendelea kuitumika Yanga tena kwa muda mrefu "alisema Bin Kleb.

Wakati huo huo kikosi cha Young Africans leo kimeanza mazoezi asubuhi katika uwanja wa Bora - Mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo wa hisani dhidi ya Simba SC Disemba 14, 2013, mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.