Monday, 11 November 2013

AFISA USALAMA FEKI ANASWA KWENYE MSAFARA WA RAIS MJINI GEITA



GEITA: Katika hali ambayo inazidisha mashaka juu ya Usalama wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Mtu mmoja ambaye hajatambulika nia yake, amefanikiwa kujipenyeza katika msafara wa Rais na kujifanya miongoni mwa walinzi wa msafara.
Mtu huyo ambaye baada ya kunaswa amekutwa na vitambulisho bandia, alifanikiwa kujipenyeza katika mkutano wa kwanza wa ziara ya Rais wilayani Bukombe mkoani Geita, ambapo kulikuwa na sherehe za uzinduzi wa barabara ya Lami ya Bwanga hadi Uyovu Lunzewe yenye urefu wa km 45 ambayo ujenzi wake ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete siku hiyo Novemba 9 mwaka huu.
Akiwa kama afisa usalama alikuwa akizuia baadhi ya watu kufika maeneo maalum yaliyoandaliwa mahususi kwa ulinzi, lakini pia alikuwa akipitapita kukagua baadhi wa watu wakiwamo na waandishi wa habari huku akiwapanga namna ya kukaa vyema kabla msafara wa Rais kuwasili eneo la tukio.
Katika mkutano huo wa kwanza alifanikiwa kupita salama kwani baada ya mkutano huo kumalizika, aliweza kupata usafiri na kuondoka na msafara umbali wa km 53 na kufika Ikulu ndogo ya Bukombe, ambako msafara uliitulia kwa muda na wageni kupata chakula, kisha kuelekea katika mkutano wa pili wa hadhara mjini Ushirombo.
Hata hivyo, huko hakuweza kufanikiwa, Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa shirikiana na Maofisa Usalama wa Taifa, lilifanikiwa kumtia mbaroni mtu huyo kama inavyoonyesha (Pichani Juu) akiwa ameshikwa chini na Ulinzi wa Askari polisi na afisa usalama akitolewa katika ya mkutano wa Rais Kikwete uliofanyika katika Uwanja wa Kituo cha mabasi Ushirombo.
Mtu huyo ametambulika kwa jina la Kwamani Juma anakadiriwa kuwa na umri kati ya 43-46, alikamatwa Novemba 9 mwaka huu, eneo la Ushirombo katika mkutano wa hadhara akiwa amejipanga kama maaofisa Usalama karibu na jukwaa kuu alilokuwa amekaa Rais Jakaya Kilwete.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Leonard Paul amethibitisha kukamatwa kwa afisa huyo bandia, alisema "Ndiyo… amekamatwa, si umeona kwenye mkutano kilichotokea, sasa unataka nieleze nini zaidi," alielza Kamanda Paul



Kukamatwa kwake kulifanya wanaomjua kuanza kueleza wasifu wake na mmoja wapo akiwa ni Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Bukombe, Julius Kambarage ambaye kutokana na kumfahamu mtu huyo alistajaabu kumuona akiwa amejipenyeza jukwaani hali ambayo ilimfanya kutoa taarifa kwa wahusika.
"Mimi nilikuwa MC, pale kwenye uzinduzi wa Barabara (Lunzewe) nilipomuona niliwaeleza watu wa usalama, sikujua walifanyiaje kazi, lakini nlistajaabu amefika tena Ushirombo, ila safari hii nilimuona wakati akikamatwa, naona atakuwa Tapeli huyu" alieleza Afisa utamaduni huyo.
Mtu huyo mpaka akikamatwa alionekana akiwa mtanashati, aliyevalia Kaunda Suti, miwani na kuonekana nadhifu, ina anadaiwa katika ukaguzi kitambulisho alichokutwa nacho kilikuwa kimeandikwa jina lake na huku kikuonyesha kuwa na Muhuri unaosomeka ‘Ulinzi na Usalama wa Taifa’.
Naye Diwani wa Kata ya Uyovu Yusufu Fungameza (Chadema), alieleza kumtambua mtu huyo na kudai ni mkazi wa Kata yake lakini amekuwa akitajwa na kulalamikiwa kuhusika na matukio ya utapeli kwa wananchi.
"Huyu bwana namfahamu sana, ni mkazi Kata yangu lakini amekuwa akinihusisha na vote do vya utapeli, yapo matukio kadhaa ya kulalamikiwa kutapeli watu pale Uyovu amewahi kumtapeli mfanyabiashara mmoja," alieleza.

MH. LOWASSA AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE YA AWALI YA KANISA LA KKKT,KIJITONYAMA JIJINI DAR,ZAIDI YA SH. MIL 600 ZAPATIKANA


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama,muda mfupi kabla ya kuanza kwa Harambee Maalum ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Awali katika kanisa hiyo.Ambapo zaidi ya Sh. Mil. 600 zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika Kanisani hapo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama,muda mfupi kabla ya kuanza kwa Harambee Maalum ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Awali katika kanisa hiyo.Ambapo zaidi ya Sh. Mil. 600 zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika Kanisani hapo.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga akimuunga Mkono Mgeni Rasmi,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa katika Harambee ya Uchangishaji Fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Awali ya Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama,iliyofanyika leo Novemba 10,2013,jijini Dar es Salaam.zaidi ya Sh. Mil. 600 zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika Kanisani hapo.
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Idd Azzan akimuunga Mkono Mgeni Rasmi,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa katika Harambee ya Uchangishaji Fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Awali ya Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama,iliyofanyika leo Novemba 10,2013,jijini Dar es Salaam.zaidi ya Sh. Mil. 600 zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika Kanisani hapo.
 Mwenyekiti wa Harambee Maalum ya Kuchangisha fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Awali katika kanisa KKKT Usharika wa Kijitonyama jijini Dar es Salaam,Mzee Kamugisha akifanya mnada wa Picha ya Jengo la Shule hiyo ya awali,Wakati wa Harambee iliyofanyika leo kwenye Kanisa la KKKT,Kijiyonyama jijini Dar leo.
 Mchungaji wa Kanisa hilo akinungumza machache.

 Kwanya ilitumbuiza wakati wa Harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiangalia kitu kupitia simu ya Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Makongoro Mahanga.Kushoto ni Bw. Sadock Magay.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa na Wajuu zake,Angelica (kulia) na Edward mara baada ya Ibada katika Kanisa hilo la KKKT,Kijitonyama leo.

Harambee ikiendelea.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimkabidhi Muigizaji wa Filamu Nchini,Jacqueline Wolper moja ya bidhaa zilizokuwa zikinadiwa kwenye Harambee ya Uchangiaji wa Fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Awali katika Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama,Jijini Dar es Salaam.zaidi ya Sh. Mil. 600 zilipatikana katika harambee hiyo iliyofanyika Kanisani hapo.

Sunday, 10 November 2013

SEND OFF YA HAPPY MWALAMI YAFANA


                                            Bi harusi mtarajiwa (kulia) akiwa na matroni wake
                                                             pozz na mama mzazi
                                                                   picha za ndugu na jamaa
                                                                                   mapozzz
                                                              wapambembe ,usipimeee
                                                       ni siku ya ukumbusho
                                                                 happy na dada mpendwa
                                Mr & Mrs martin watarajiwa 30-11-2013 wanafunga ndoa huko Nairobi
                                                                       iko poa three sisters
                                                       mama mzazi wa happy(mama shani)
              mwenyekiti wa kamati bw Asiel akifungua sherehe katika ukumbi wa bukoba club
                                                                        love u a lot
                                                   bw Nyamukama muda wote huwa yuko smart
                                                                           picha ya pamoja
                                   mama mzaa chema akiwa amepewa zawadi za kumpongeza na marafiki

                                                          twende  wakuone mme wangu mtarajiwa
                                               mweonekano wa keki iliyotengenezwa na mama semeo
                                                                 bw harusi mtarajiwa  martin
                             happy akikata keki,anatarajia kufunga ndo huko Nairobi 30-11-2013
                                                                 matukio ni muhimu yanatafutwa
                                                                         happy akimpa mama keki
                                                                  dadaa na mumewe
                                                                               kabendera family
                                                        bw ngirwa akifungua shampein
                                                                filo na rafiki yake kipenzi
                                                                                      mapozzz
                                                                       wageni wakiwa katika furaha
                                          mama mzazi wa happy (mama shani) akitoa neno
                                               happy akiwa na bwna harusi mtarajiwa bw martin
                                                        bety akiwa na mama mdogo
                                      bety kushoto akiwa na mama mlezi wa happy bi Filomena
                                                 Happy akiwa na mama mzazi na matroni wake
                                                      Happy akiwa ufukwe wa spice beach