Wednesday, 30 October 2013

RAIS WA CAF AMPONGEZA MALINZI



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Issa Hayatou amempongeza Jamal Malinzi kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.
Katika salamu zake kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya CAF na familia ya mpira wa miguu Afrika, Rais Hayatou amesema uchaguzi huo unampa Rais Malinzi fursa ya kuupeleka mbele mpira wa miguu nchini Tanzania.
Amesema CAF ina imani uwezo wake katika uongozi, uzoefu na ujuzi katika mpira wa miguu havitausaidia mpira wa miguu Tanzania pekee bali Afrika kwa ujumla, na kuongeza kuwa ataendeleza ushirikiano uliopo ili kuwanufaisha zaidi vijana wa bara hili.
Rais Hayatou amemtakia Rais Malinzi kila la kheri katika kipindi chake cha uongozi na kumhakikishia kuwa CAF iko pamoja naye katika kusukuma mbele gurudumu la kuendeleza mpira wa miguu.
PAMBANO LA YANGA, MGAMBO SHOOTING LAINGIZA MIL 37/-
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting lililochezwa jana (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 37,915,000.
Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 46 iliyomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 walikuwa 6,515 ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 5,783,644.07, gharama za kuchapa tiketi sh. 3,145,790 wakati kila klabu ilipata sh. 8,550,741.95.
Wamiliki wa uwanja walipata sh. 4,347,834.89, gharama za mchezo sh. 2,608,700.93, Bodi ya Ligi sh. 2,608,700.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,304,350.47, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,014,494.81.
SIMBA, KAGERA SUGAR KUUMANA KESHO.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaanza raundi ya 12 kesho (Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Viingilio katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv kupitia TBC 1 vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A.
Nayo Yanga itashuka uwanjani Novemba Mosi mwaka huu katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya JKT Ruvu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS, DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KUJADILI MTANDAO WA MAJI KWA NCHI WANACHAMA WA SADC LILILOANDALIWA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua rasmi kongamano la kujadili Mtandao wa maji kwa Nchi Wanachama wa SADC, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leoJijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua rasmi kongamano la kujadili Mtandao wa maji kwa Nchi Wanachama wa SADC, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leoJijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa 'local Organizing Commitee', Prof. Mtalo Felix, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo.
  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
   Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
   Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo baada ya kufungua rasmi
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Bashir Mrindoko, wakati akiondoka baada ya picha ya pamoja na kufungua Kongamano la kujadili Mtandao wa maji kwa Nchi Wanachama wa SADC, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leoJijini dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano huo, Prof. Mtalo Felix, wakati akiondoka baada ya picha ya pamoja na kufungua Kongamano la kujadili Mtandao wa maji kwa Nchi Wanachama wa SADC, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leoJijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SERIKALI ZA MITAA KUJADILI MABADILIKO YA TABIANCHI


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua rasmi kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Picha Zote na OMR
 Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi huo, kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, leo.
  Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi huo, kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, leo.
 Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi, akizungumza kutoa mada yake wakati wa kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, lililofunguliwa na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika moja ya Banda la maonyesho baada ya kufungua rasmi kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.

ALHAJI CHUCHU APOKELEWA BUKOBA KWA SHANGWE, BAADA YA KUMALIZA IBADA YAKE YA HIJA

                                                        bw hasan akiwa na mkewe
                                                                 bw hasani akiwa na wake wake
 Alhaji chuchu akipokelewa maeneo ya kibeta ,amekuja kwa njia ya barabara kutokea Dar-es-salaam
                             Machozi ya furaha yakimtoka alhaji chuchu baada ya kuonana na mkewe
                                             alhaji chuchu akipokewa kwa shangwe
                                mapokezi ya alhaji chuchu  maeneo ya kibeta bukoba
                                                   gari lililombeba alhaji chuchu kutokea Dar
                                               msafara wa mapokezi ya alhaji chuchu
 alhaji chuchu akiwa msikiti wa bilele akiswali kumshukuru mwenyezi mungu kwa kumfikisha salama na kumaliza ibada ya hija na kurejea nyumbani salama
                                                        alhaji chuchu na shekhe kakweke
                                        shekhe kichwabuta na alhaji Abubakari kagasheki
                   bw hasan TRA, Alhaji chuchu, mke wa hasan na bw nasoro sadru wakifurahia
                                       shekhe haruna kichwabuta akiwa na alhaji chuchu
                   wadau,haruna goronga, hamis na majid kichwabuta wakimsikiliza alhaji chuchu
                         alhaji chuchu akiomba dua na kueleza safari yake ilivyokwenda mpaka kurudi
                                                                       furaha ...
                                         picha ya pamoja alhaji chuchu akiwa na mkewe na wanae

Monday, 28 October 2013

SIMBA YAPOKEA KICHAPO CHA BAO 2-1




Azam waliendelea kulisakama lango la Simba na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Kipre Tchetche dakika ya 45 akimalizia krosi safi ya Erasto Nyoni na kufanya timu zote kwenye mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu kwa bao 1-1.  

 Mpaka mwisho wa mchezo Simba imepokea kichapo cha kwanza tokea ligi kuu ya Vodacom baada ya kulala kwa Timu ya Azam Fc baada ya kufungwa bao 2-1 katika mchezo uliochezwa leo uwanja wa Taifa jijini Dar.

*RAIS KIKWETE AITAKA JAMII KUJENGA TABIA YA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  na mkewe Mama Salma Kikwete wakimpongeza mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi kwa ahadi ya kuichangia shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama Jumla ya Shilingi milioni mia mbili kila mwaka kwa miaka mitano,wakati mahafali ya kwanza ya shule hiyo iliyofanyika katika kijiji cha Nyamisati,wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Mishoni mwa Wiki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA NakayMA ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau akimkabidhi tuzo Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake wa kuimarisha elimu nchini wakati wa mhafali ya kwanza ya Shule ya Sekondari ya WAMA Nakayama iliyofanyika huko.Nyamisati, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani Mwishoni mwa wiki.Kuliua ni Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete. Picha naFredy Maro
************************************************************
 NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS  Jakaya Kikwete ameitaka   jamii  kuwa na tabia  ya  kuwafadhili  watoto yatima na wanaoishi katika  mazingira magumu   katika kuwapatia elimu, chakula na malazi ili waweze kuendesha maisha yao kwa kujiajiri au kujariwa kwani kwa kufanya hivyo nguvu kazi  ya taifa  haitaweza kupotea.

Kauli hiyo ilitolewa jana (juzi) na Rais Kikwete  wakati wa mahafali  ya  kwanza ya kidato cha nne ya Shule ya Sekondari  ya  Wama Nakayama iliyoko  Nyamisati , wilayani Rufiji , mkoani Pwani yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Shule hiyo  inayoendeshwa  na Taasisi ya Wanawake  na  Maendeleo(WAMA)  ,ambapo Mwenyekiti wa taasisi hiyo ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. 

Rais Kikwete aliwashukuru watu mbalimbali walichangia shule hiyo kwa moyo wao wa upendo na huruma  ili watoto wa kike yatima na wanaoishi katika mazingira magumu  waweze kupata elimu, huku akisema  kama wasi wafadhili  hao isingekuwa rahisi watoto hao kuwezeshwa kusoma shuleni hapo.

“ Mtapata fadhila  kwa Mwenyezi Mungu  kwa kila mtoto atakayesoma hapa…Mkopesheni Mwenyezi Mungu atawapa fadhila zake,”alisema Rais Kikwete.
 Kauli hiyo pia iliungwa na  mkono na Mama Salma Kikwete ambaye alisema bila juhudi za pamoja kati ya  Serikali, jamii na sekta  binafsi  watoto  wengi wa kundi hilo  watakosa elimu.

Mama Kikwete alisema nchi ina Watanzania milioni 44.9 kama wapo wenye uwezo wapatao milioni tano kila mmoja akimchukua mtoto mmoja. 

“ Tanzania   isiyokuwa  na watoto wasio matumaini inawezekana,”alisema Mama Kikwete  huku akisema kwa kufanya hivyo kuwasaidia kujikwamua katika hali ya umasikini.
    
 Rais   Kikwete   aliwataka wanafunzi  hao  kuwa na malengo ya kupata elimu  ya juu ili waweze kukabiliana na changamoto mbalimbali na kulisaidia taifa, huku akisisitiza  wawe jasiri kusoma fani  ambazo wanawake wengi wanaogopa kuzisoma   ambazo zitawawezesha kuwa mabingwa mafano udaktari, wahandisi na wanasheria.

 “ Hamna budi kushukuru na kujipongeza ombi langu ni kuweni watoto wema heshima na mabalozi wa shule hii.  Shule hii itakapokamilika huduma zitakuwa bora.Shule hii ina kila sababu ya kuwa shule bora,” alisema Rais Kikwete.

Aidha  Rais Kikwete  alizitaka  halmashauri nchini  kuendelea kushishirikiana  na Maendeleo(WAMA) kuwatambua watoto yatima na wanaoishi katika  mazingira  magumu  ili  waweze kupata elimu kwa malengo ya  taasisi hiyo.

Katika mahafali hayo Mwenyekiti wa  kammpuni  za IPP, Reginald Mengi  aliahidi kuchangia shule hiyo Sh. milioni 200 kwa kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano na Umoja wa Wanawake Tanzania  wa Chama  cha Mapinduzi (UWT)uliahidi kutoa Sh. milioni 10  yakiwemo mashirika mbalimbali yaliyoahidi kutoa michango  kadhaa.

Rais  Kikwete katika mahafali hayo aliwatunuku vyeti wanafunzi 67 na kutoa zawadi za vyeti na fedha tasilimu kwa wanafunzi na walimu waliofanya vizuri, ambapo mwanafunzi  aliibuka mshindi baada ya kufanya vema  kwenye masomo ya biashara, historia na Kiingereza.Mwanafunzi aliyefanya vizuri kila somo alipata Sh. 100,000 na mwalimu Sh. 500,000.  

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATOA POLE KWA MJANE NA FAMILIA YA BALOZI ISAAC SEPETU LEO


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa wanafamilia wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana  jijini Dar es salaam.
 Mke wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimfariji mjane wa Balozi Isaac Sepetu alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kufuatia msiba Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  alipokwenda  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole. Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
 Mama Salma Kikwete  akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa Balozi Isaac Sepetu  nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam. . Marehemu Sepetu aliyefariki jana katika jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji  mjane wa Balozi Isaac Sepetu, Mama Miriam Sepetu, alipokwenda na Mama Salma nyumbani kwa marehemu Sinza Mori, Dar es salaam, kutoa pole kwa mjane huyo na familia ya Marehemu Sepetu aliyefariki jana jijini Dar es salaam.

HOTUBA YA KWANZA YA JAMAL MALINZI,RAISI MPYA WA TFF


 Hatimaye Tumechagua Mabadiliko,
Salamu kwa wanafamilia wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Salamu kwa wapenda michezo wa ndani na nje ya nchi yetu Tanzania.

Naanza kwa kumshukuru Mungu kwa hekima, busara, akili, vipaji na uwezo aliotujaalia kutuwezesha kutenda yote haya kwa amani na utulivu.

Shukrani za dhati zimwendee Bw. Leodegar Tenga, rais wa TFF 2005 - 2013 anayekabidhi madaraka kwa rais mpya wa TFF. Yeye na timu yake kwa hakika wanastahili pongezi kwa mengi mazuri waliyofanya.

Shukrani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi 2013 kwa kunikubali, mimi Jamal E. Malinzi niwe Rais wa TFF kwa kipindi kijacho cha miaka minne.

Kweli dunia imekuwa kijiji, kwani kipindi cha masaa 72 baada ya kuzindua ilani yangu ya uchaguzi, nimepokea salamu, maoni na mapendekezo toka ndani na nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Burundi, Ivory Coast, Denmark na NewZealand.

Kupitia www.jamalmalinzi.com, twitter @jamalmalinzi, Jamii Forum, Facebook na mitandao mingine, naomba tuendelee kuwasiliana, kutoa maoni, kukosoa na kuchangia mijadala yenye tija na ufanisi ili Tanzania yote ipate neema ya mpira wa miguu.

Safari ni ndefu na wasafiri ni wengi kwenye vyombo vichache vya usafiri. Kwa wale ambao tayari wana ramani ya safari yetu, sote bila kujali tofauti zetu hasa wakati wa kuwania uongozi, tutoe mchango wake ili Tanzania isonge mbele katika ulimwengu wa soka.

Naam, kuna msemo wa Kiswahili unaosema 'kukata tamaa ukingali unaishi ni dhambi'. Naomba msemo huu na utuongoze kila tunapojikwaa tunanyuke na kuendelea na safari hadi tufike tulipopakusudia.

Historia imeshaanza kuandikwa, mwaka 2013 ni Tumechagua Malinzi, Tumechagua Mabadiliko na sasa tunasonga mbele.
Jamal E. Malinzi
Oktoba 27, 2013

JAMAL MALINZI AVUNJA KAMATI ZOTE ZA TFF - ATOA MSAMAHA KWA WALIOFUNGIWA



Jamal Emil Malinzi ndiye Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Malinzi ameshinda wadhifa huo katika uchaguzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF uliofanyika juzi (Oktoba 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Aliibuka na ushindi wa kura 73 dhidi ya mpinzani wake pekee Athuman Jumanne Nyamlani aliyepata kura 52. Nafasi ya Makamu wa Rais imetwaliwa na Wallace Peter Karia aliyepata kura 67 na kuwashinda Ramadhan Omari Nassib kura 52 huku Imani Omari Madega akipata kura sita.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Rais Malinzi ametaka ushirikiano kutoka kwa wadau wote akiwemo mpinzani wake Nyamlani katika kuhakikisha mpira wa miguu nchini unasonga mbele.
Pia ametoa msamaha kwa watu wote waliokuwa wamefungiwa kuanzia ngazi ya wilaya, mkoa na TFF. Msamaha huo hauwahusu wale waliofungiwa kwa makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile msamaha huo hauhusu adhabu zilizotolewa katika ngazi ya klabu.
Rais Malinzi pia amevunja kamati zote za TFF ambapo ataziunda upya kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.
Kwa upande wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji walioshinda ni Kalilo Samson (Kanda namba 1- Geita na Kagera) aliyepata kura 102 za ndiyo na 17 za hapana. Kanda namba 2- Mara na Mwanza, mshindi ni Vedastus Lufano aliyepata kura 51 dhidi ya Jumbe Odessa Magati (11), Mugisha Galibona (24), na Samwel Nyalla (39).
Epaphra Swai ndiye mshindi wa Kanda namba 3- Shinyanga na Simiyu kwa kura 63 dhidi ya Mbasha Matutu aliyepata 61. Kanda namba 4- Arusha na Manyara mshindi ni  Omali Walii Ali aliyepata kura 53 dhidi Elley Mbise (51), Ally Mtumwa (19).
Kanda namba 4- Kigoma na Tabora, mshindi ni Ahmed Idd Mgoyi aliyepata kura 92 dhidi ya 28 za Hamisi Yusuf Kitumbo.
Ayubu Nyaulingo na Blassy Mghube Kiondo ameshinda Kanda namba 6- Katavi na Rukwa kwa kura 73 dhidi ya Ayubu Nyaulingo aliyepata 52. Ayoub Shaibu Nyenzi ndiye mshindi wa Kanda namba 7- Iringa na Mbeya kwa kupata kura 59 na kuwapiku David Samson Lugenge (8), John Exavery Kiteve (12) na Lusekelo Elias Mwanjala (46).
Kanda namba 8- Njombe na Ruvuma inawakilishwa na James Patrick Mhagama aliyepata kura 93 dhidi ya 31 za Kapteni mstaafu Stanley William Lugenge. Athuman Kingombe Kambi ndiye mshindi wa Kanda namba 9- Lindi na Mtwara kwa kura 84 akiwazidi Francis Kumba Ndulane (30) na Zafarani Mzee Damoder (11).
Hussein Zuberi Mwamba ametetea ujumbe wa Kanda namba 10- Dodoma na Singida kwa kura 63 akiwapiku Stewart Masima (58) na Charles Komba (4). Geofrey Irick Nyange ameshinda Kanda namba 11- Morogoro na Pwani akipata kura 78 dhidi ya Juma Pinto (26), Farid Nahdi (14), Riziki Juma Majala (5) na Twahil Twaha Njoki (2).
Kanda namba 12- Kilimanjaro na Pwani, Khalid Abdallah Mohamed ndiye aliyeibuka kidedea kwa kura 69 dhidi ya 54 za mpinzani wake Davis Elisa Mosha. Kidao Wilfred Mzigama ameshinda Kanda namba 13- Dar es Salaam kwa kupata kura 60 dhidi ya wapinzani wake Muhsin Said Balhabou (50), Omar Isack Abdulkadir (10) na Alex