Monday, 16 September 2013

TEC yataka Kamishna wa Polisi Z’bar afukuzwe kazi


Padri Joseph Magamba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Machui Zanzibar aliyemwagiwa tindikali akisaidiwa kushuka kwenye ndege na Padri Thomas Assenga(kushoto) wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Zanzibar baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana kuelekea katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi
  • Yadai ameshindwa kuwakamata watuhumiwa wanaowamwagia  tindikali viongozi wa dini.

Dar es Salaam. Tukio la kumwagiwa tindikali  Padri wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Joseph Mwang’amba huko Zanzibar limechukua sura mpya baada ya  Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) kumtaka Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa kufukuzwa kazi.
Makamu  Rais wa TEC, Askofu Severine Niwemugizi aliliambia gazeti hili jana kuwa anapaswa kuondolewa kwa sababu ya kukithiri kwa matukio hayo visiwani.
Askofu Niwemugizi alisema kamanda huyo anapaswa kuchukuliwa hatua kwa kuwa ameshindwa kukamata watu wanaofanya vitendo viovu dhidi ya viongozi wa dini.
Kwa upande wake Kamishna Mussa alisisitiza hawezi kujiuzulu na kwamba anayestahili kulaumiwa ni Mkurugugenzi wa Mashitaka (DPP) kwa sababu kwa upande wake alishawakamata watuhumiwa wa matukio hayo.
“Kazi yangu mimi ni kupeleleza na kukamata watuhumiwa,ila kazi ya kushitaki watu ni ya DPP hivyo mimi siyo wa kulaumiwa’Alisema .
Hili ni tukio la nne la uhalifu dhidi ya viongozi wa dini huko Zanzibar baada ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wakati Padri Ambrose Mkenda alipigwa risasi na Katibu wa Mufti, Sheikh Fadhili Soraga alimwagiwa tindikali.
  Katika hatua nyingine, Askofu Niwemugizi alisema kuwa matukio hayo kwa sasa yamekuwa wazi kwamba ni mpango wa kuangamiza Ukristo na Wakristo kwa ujumla katika Visiwa vya Zanzibar.
“Uchochezi umefanywa wa kuhamasisha chuki dhidi ya Ukristo unasikitisha. Tulikaa kama Wakristo tukaiambia Serikali mambo ambayo inaweza kufanya kukomesha vitendo hivi, lakini hadi sasa hakuna lililotekelezwa,” alisema na kuongeza: 
“Awali ilielezwa kwamba siyo sababu ya kidini,  watu wa Kikundi cha Uamsho ndiyo walioanzisha moto huo na wanauendeleza, hali inatisha zaidi kwamba hata jamii ya Wazanzibar haionyeshi nia ya kushiriki kukomesha ukatili huu, kama huyu Padri Mwang’amba amemwagiwa kwenye kituo cha intaneti ni eneo ambao lina watu mbona mhusika hajakamatwa? alihoji.
Wakati huohuo, Mwenyekiti wa Kamati ya Haki na Maadili kwa Jamii kwa Viongozi wa Dini ya Kikristo, Mchungaji William Mwamalanga alisema kuwa Kamishna huyo wa Polisi anatakiwa kufukuzwa kazi kwa kuwa anaichafua Zanzibar kwa kushindwa kudhibiti matukio hayo ya uhalifu kwa makusudi, pia amejaa udini.

WASHIRIKI WA MISS TANZANIA WATEMBELEA KAMPUNI YA TANZANIA DISTILLERIES LIMITED 'KONYAGI'


Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' David Mgwassa akizungumza na waandishi wa habari baada ya warembo wanaowania taji la Miss Tanzania kufanya zihara katika Kampuni hiyo mwishoni juzi ambayo imedhamini mashindano hayo kupitia kinywaji chake cha Zanzi 
Baahi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakichukua chakula wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' juzi   ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi
Baahi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakiwa kwenye pozi wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi'  juzi  Konyagi  ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi
Meneja masoko  ya ndani na nje wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' ,Vimal Vaghmaria kushoto na meneja masoko wa ksampuni hiyo Joseph Chibhee wakigonganisha grass na Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania walipotembelea kiwandani  juzi Konyagi ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi
Meneja masoko  ya ndani na nje wa Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi' ,Vimal Vaghmariakatikati akiwa katika pozi na baadi ya washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania walipotembelea kiwandani  juzi konyagi  ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi
 Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakiwa kwenye pozi wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi'  juzi konyagi ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi

Baahi ya Warembo wanaowania taji la Miss Tanzania wakipata chakula wakati walipotembelea Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited 'konyagi'    ambao ni wadhamini kupitia kinywaji cha Zanzi

MALKIA WA ZOUK TANZANIA HAFSA KAZINJA AMUENZI MUHIDIN MAALIM GURUMO KWA KUIMBA WIMBO WA "NIMUOKOE NANI"

 Malkia wa Zouk nchini Hafsa Kazinja akiwa na Omari Mkali (kushoto) na Abdul Salvador baada ya kukamilisha kurekodi wimbo wa 'NIMUOKEOE NANI' katika Studio za OM Productions jijini Dar es salaam wikiendi hii.
 Baada ya ukimya wa muda mrefu,   Malkia wa Zouk Tanzania,  Hafsa Kazinja,  anaibuka upya katika fani akiwa na ingizo lake la kwanza kati  ya kumi aliyoandaa kwa kuimba wimbo maarufu wa NUTA Jazz Band uitwao “NIMUOKOE NANI”  anauouleta hewani katika mahadhi ya Zouk.
Hafsa Kazinja anasema ameamua kurudi ulingoni kwa kutoa wimbo huo ili kumuenzi Mzee Muhidin Maalim Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani ya muziki baada ya kufanya kazi hiyo akiwa na bendi mbalimbali tokea mwaka wa 1960.
“Nimeamua kuimba wimbo huu wa “NIMUOKOE NANI” ili  kumuenzi gwiji huyu wa muziki kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo naibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda”, anasema Hafsa ambaye alitoka kwa wimbo wake wa “PRESHA” aliomshirikisha Banana Zorro.
Hafsa ameandaa wimbo huo wa “NIMUOKOE NANI” katika studio za OM Productions ya jijini Dar es salaam chini ya wanamuziki nguli, Abdul Salvador na Omari Mkali.
“Nafurahi kwamba wimbo wa NIMUOKOE NANI nimeuimba baada ya kupata Baraka zote toka kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe.
“Haikuwa rahisi kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya kwenda kumuona nyumbani kwake alinifanyisha mtihani wa kuuimba wote kabla ya kuridhika maana alisema asingefurahi kuona wimbo wake unaimbwa hovyo hovyo na kuharibiwa radha yake”, anasema Hafsa, ambaye hivi sana anamalizia ngoma zake zingine tisa alizotunga mwenyewe, kabla ya kuvamia anga kwa mara ingine.
Hafsa anasema katika ukimya wake amekuwa akifanya utafiti na kujifunza kwa undani zaidi fani ya muziki, akipata mawaidha maridhawa toka kwa wanamuziki nguli ndani nan je ya nchi wakiwemo Muhidin Maalim Gurumo, Omar Mkali, Abdul Salvador na Lokassa ya Mbongo wa Congo aliyekutana na kufanya naye kazi alipokuwa ziarani Marekani hivi karibuni.
Msanii huyu wa kizazi kipya anasema ataitambulisha rasmi ngoma ya “NIMUOKOE NANI” katika tamasha la kumuenzi Mzee Gurumo lililopangwa kufanyika OKtoba 1, 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
“Natumaini wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye tamasha hilo name naahidi kuitendea haki ngoma ya “NIMUOKOE NANI” hivyo wasikose kuja kujionea wenyewe jinsi sie wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya kazi na wakubwa wetu wa kazi, anaongezea Hafsa ambaye pia anaandaa video yake pamoja na ya ngoma zake zingine mpya.
Mkongwe Abdul Salvador, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi wa  bendi ya TANCUT ALMASI YA Iringa iliyotamba na mtindo wake wa “FIMBO LUGODA”, anamtaja Hafsa kazinja mmoja wa wanamuziki wa kike waliojaaliwa sauti nzuri na kipaji cha hali ya juu hapa nchini.
“Kwa kuweza kuimba wimbo wa Mzee Gurumo na kupatia kisawasawa inadhihirisha kwamba Hafsa ni mwanamuziki aliyekomaa maana si mchezo kuimba nyimbo ya wakongwe kwa ufasaha kama alivyofanya Hafsa.
“Na hii inadhihirisha kwamba uwezekano wa kizazi kipya na cha zamani kufanya kazi pamoja ni mkubwa sana na sioni kwa nini isiwe hivyo”, anasema Salvador.
Omari Mkali, aliyetamba na bendi ya CHUCHU SOUNDS, chini ya marehemu Yusuf Chuchu, naye anamwelezea Hafsa Kazinja kama moja ya majembe ya muziki hapa nchini kwa upande wa kinamama, na kwamba anaweza kufika mbali endapo kama moto aliokuja nao upya atauendeleza.



Sunday, 15 September 2013

MAMIA WAUDHULIA DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU HAJATI ZANABIA ELIAS NASSIBU ILIYOFANYIKA KAMACHUMU BUSHAGARA

                                           Hii ni picha ya marehemu hajati zanabia elias nasibu
 Nyumbani kwa marehemu hajati zanabia ilipofanyika dua ya kumuombea kutimiza mwaka mmoja wa kifo chake
 hili ni kaburi la marehemu hajati zanabia elias nasibu ambae ni bibi yangu mimi(jamco) mzaa mama
                                                      mambo ya maandalizi ya pilau
                                                                         likiandaliwa pilau
                                                      ili pilau linoge sharti kachumbali iwepo
                                      mzee antidiua nae alikuwepo ndugu wa marehemu
 haruna goronga, salumu mawingu wakisalimiana bi leila elias nasibu ,binti mkubwa wa marehemu
bw majid kichwabuta akiwa na bw salamu


                                   bw hamidu akiwa na bw yusuf elias nasibu mtoto wa marehemu
                                                       bw bushira akiwa na bw yazid
 huyu bwana anaitwa mchunguzi, kwa wale wa kamachumu wanamfaamu kichwa chake kinajua mambo mengi sana
                                       mzee ahmad wa siku nyingi sana kamachumu,alieshika tama
                                                                    dua ikiombwa
                                             mic utaipenda na hasa inapopata mtaalamu
 bw salumu mawingu akitoa shukrani kwa niaba ya familia  ya marehemu alhaji elis nasibu
                                                           kaptan mwasa  akisalimia
                                          bw abdul, haruna na keptain mwasa nao walikuwepo
                                                                bw bingwa nae alikuwepo
 hapa shekhe aliwakumbusha wanadamu kuwa hakuna siku ngumu na ya shida kama siku ya kwanza umewekwa kaburini,amewataka waumini kumcha mwenyezi mungu, maana hapa duniani si lolote si chochote
                          shekhe Nuran akitoa mawaidha kwa walioudhulia dua ya kuwaombea marehemu
                                                                              wakati wa mlo
                                                                       tulikupenda sana bibi yetu