Thursday, 12 September 2013

MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA BIA SERENGETI BREWERIES TANZANIA BW STEPHEN GANNON ATEMBELEA WAKALA WA SERENGETI BREWERIES WA KAGERA NA GEITA, KAMPUNI YA ZACHWA INVESTMENT KUJIONEA UFANISI WA KAZI




                                 Mkurugenzi mkuu wa serengeti  breweries bw Stephen Gannon



mkurugenzi wa zachwa investment bw muganyizi wakala wa kagera na geita akiongea na mkurugenzi mkuu wa serengeti breweries bw stephen gannon nyumbani kwa bwana muganyizi



                                bw  muganyizi na mkewe,wakiwa na  bw stephen gannon

                                                             Ni katika hoteli ya victorius


mmoja wa wakurugenzi wa zachwa investment jane muganyizi akiongea na wageni waliokaribishwa chakula cha usiku  katika hotel ya victorius


mkurugenzi mkuu tanzania wa serengeti breweries akiongea na wateja na wadau mbalimbali wa serengeti





                                     naikubali kazi yenu........tutaendelea  kufanya kazi na nyie


        mkurugenzi wa zachwa investment bw muganyizi akielezea kinywaji kipya cha serengeti

si utani serengeti ni kiboko...

                                         wanasema waenga upele umepata mkunaji,




jamani sina mengi , kunywa bia za serengeti

                                                    chakula cha bukoba si mchezo.......



                                    wadau wa serengeti wakipata chakula victorius hotel bukoba



                                                                 enangaaaa...

                                                     mkurugenzi akanogewa .....

                                                            ukafika wakati wa muziki



                                                                        serengeti breweries si mchezo

NI MWAKA MMOJA SASA TANGU HAJATI ZANABIA ELIS NASIBU AFARIKI DUA YA KUMUOMBEA INAFANYIKA KAMACHUMU BUASHAGARA 13-9-2013 KUANZIA SAA SABA MCHANA

Ni mwaka mmoja sasa tangu uage dunia,tulikupenda sana  mzazi wetu na hakika  katika kipindi cha mwaka mmoja sasa pengo lako linaonekana na ni vigumu kuzibika, maana ulikuwa ni nguzo kubwa na msaada mkubwa katika familia, ndugu ,jamaa na marafiki wote,busara nma hekima zako  hakika  tunazikosa,mshikamano ulioujenga katika familia ,upendo na mapenzi makubwa tunayakosa, tulikupenda sana illa mungu amekupenda zaidi unakumbukwa na wanao wapenzi, laila elias nasibu, halima , afisa, seleman, yusuf na naziri, wajukuu wako wote, vitukuu, ndugu jamaa na marafiki,FAMILIA INAWAKARIBISHA KATIKA DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU TAREHE 13-9-2013 SIKU  YA IJUMAA KUANZIA SAA SABA MCHANA ITAKAYOFANYIKA KAMACHUMU BUSHAGARA NYUMBANI KWA MAREHEMU ALHAJI ELIAS NASIBU, KARIBUNI SANA

Wednesday, 11 September 2013

TANGAZO LA KUIBIWA GARI


SERENGETI FREIGHT
GARI LIMEIBIWA
MAKE: NISSAN NAVARA
MODEL: AVENTURA 
REG : AD07 MWK

TUNAWATANGAZIA NDUGU ZETU WATANZANIA WENZETU KUWA TUMEIBIWA HILI GARI KUTOKA KWENYE OFISI YETU HAPA LONDON 
TUNADHANI KUWA WEZI WA GARI HILI WATAKUWA WAMELISAFIRISHA KWENDA DAR AU ZANZIBAR 
TUNAOMBA MTU YEYOTE ATAKAE LIONA KAMA NI  BANDARINI AU HATA BARABARANI ATOE TAARIFA KITUO CHA POLISI CHA JIRANI AU ATUPIGIE MOJA KWA MOJA KWENYE NAMBA ZETU ZIFUATAZO

CHRIS LUKOSI +44 (0) 7903828119
TORNADO - DAR - 0713607116

ZAWADI YA SHS MILIONI KUMI (SHS 10,000,000) ITATOLEWA KWA ATAKAEFANIKISHA UPATIKANAJI WA HILI GARI

ASANTENI SANA 

CHRIS LUKOSI

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD,
EAST TILBURY, ESSEX, RM18 8RH

ASHA BARAKA NA BOMOABOMOA

 Mkurugenzi wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', ambaye pia ni Mjumbe wa Nec CCM, Asha Baraka, akiwaka wakati akizungumza  na mtandao huu jana jioni alipokuwa akisimamia zoezi la kuwazuia wabomoaji kutobomoa nyumba na vibanda vya wananchi katika eneo hilo la Hanansifu bila kufikia muafaka kwa mazungumzo na wahusika.

Zoezi hilo la kubomoa eneo hilo ili kujengwa barabara ya mtaa lilianza tangu mwezi wa tano mwaka huu, ambapo wenye nyumba zizizopo eneo hilo baada ya mazungumzo na wasimamizi wa zoezi hilo na Diwani na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, walikubaliana na kuwekewa alama eneo linalotakiwa kubomolewa ili kupisha upanuzi huo.

Baada ya alama hizo ulifanyika ubomoaji na kuchimba barabara hiyo kana kwamba zoezi la ujenzi lilikuwa likianza muda mfupi tu baada ya ubomoaji, lakini cha kushangaza watu wao baada ya kubomoa waliondoka zao na kuacha eneo hilo likiwa na madimbwi makubwa yaliyojaa maji na kusababisha eneo hilo kutopitika kwa wenye magari na waenda kwa miguu.

Aidha baada ya kumalizika kwa ubomoaji huo, wahusika wenye nyumba zao na fremu za maduka eneo hilo, walikaa kwa muda wa miezi miwili na walipohakikishiwa kuwa zoezi hilo limemalizika na hakuna ubomoaji utakaoongezeka, walianza kukarabati nyumba na fremu zao upya ili kuendelea na biashara.

Cha kushangaza ghfla watu hao walirejea tena jana na kuchora alama mpya kwa kutumia mkaa, na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo jambo lililowaacha hoi wananchi wa eneo hilo na wenye frem zao, kutokana na kutotolewa kwa taarifa wala watu hao kutokuwa na kiongozi hata mmoja wa Eneo hilo yaani Diwani au Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ambao walitakiwa kuwepo ili kutoa ufafanuzi wa tukio hilo.

Lakini cha kushangaza wakati wa zoezi hilo, hakuwepo Mwenyekiti wala Diwani, jambo lililowafanya wananchi kuhoji juu ya uhalali wa zoezi hilo.

Wakati wa zoezi hilo Asha Baraka, alimpigia simu Diwani, Abasi Tarimba, lakini naye alimjibu kuwa hajui lolote kama Diwani na kumtumia namba ya simu ya mtu mwingine ili azungumze naye, wakati yeye ndiye hasa alitakiwa kuwapo eneo hilo na kuwatetea wapiga kura wake.

Hata hivyo watu waliokuwapo eneo hilo walishangazwa na kitendo cha jamaa hao kuendelea kumoboa upande mmoja wa eneo hilo huku wakikwepa ukuta wa ghorofa lililopo eneo hilo ambalo ni jipya lililojengwa hivi karibuni kwa kukwepa gharama, wakati alama za awali zinaonyesha kuwa hata ukuta wa ghorofa hilo ulitakiwa kubomolewa.
 Katapila likiendelea kubomoa....
 Asha Baraka akisimama mbele ya Frem zake eneo hilo kuwazuia jamaa hao kuendelea na zoezi hilo hadi upatikane muafaka na wahusika kwanza.
 Asha Baraka, akionyesha alama ya pili iliyowekwa jana na kuanza kubomoa jana hiyo hiyo.....
 Wananchi wakimsikiliza Asha Baraka.....
 Sehemu ya madimbwi yaliyoachwa na wachimbaji hao mara ya kwanza ambayo kwa sasaa yameanza kukauka.
 Nyumba ya Asha Baraka (kushoto) inayotakiwa kubomolewa na (kulia) ndiyo Ghorofa lilalokwepwa ili kupindisha barabara hiyo jambo linalofanya kubomolewa kwa nyumba za upande mmoja.
 Asha Baraka, akionyesha alama za awali zilizowekwa kwa rangi nyekundu ambazo zinaonyesha kuwa hadi ukuta wa ghorofa unatakiwa kuondoka...
 Alama hiyo ipo kwenye kibanda hiki cha mkaa ambacho kipo sambamba na ghorofa hilo..
 Alama iliypchorwa kwa mkaa mara ya pili jana.......
Sehemu ya uhalibifu uliotokea jana wakati wa zoezi hilo.....katika moja ya fremu zilizopo eneo hilo...

Tuesday, 10 September 2013


*BODA BODA SI KWA ABIRIA TU BALI HATA MZIGO WA NYANYA

 Dereva wa bodaboda akisafirisha nyanya
Wafanyabiashara wa nyanya wakisubiri wateja. Huu ni msimu wa nyanya ambapo zao hilo limepungua bei huku kisado kikiuza hadi Sh. 1500.

*MATUKIO YA BARABARANI DAR ES SALAAM - ARUSHA

 Fuso lenye namba za usajili T 509 AGD, likiwa limeanguka na kumwaga mzigo wote wa Nyanya uliokuwa umebebwa na fuso hilo. Haikuweza kufahamika kwa haraka chanzo cha ajali hiyo.
 Mmoja wa wahusika akijaribu kuomba msaada kwa magari yaliyokuwa yakipita eneo hilo.
 Mafunzo wa Kampuni ya Strabag, wakiendelea na kazi ya upanuzi wa barabara ya Arusha inayoendelea kupanuliwa ambapo kwa sasa magari yamekuwa yakitumia muda mrefu kumaliza eneo hilo kwa kupita katika barabara vumbi iliyowekwa kwa dharula.
 Upanuzi wenyewe ni kama hivi
 Gari ndogo inayoelezwa kuwa iligongwa na basi la Happy Nations eneo la Mto Wami, likiwa limeegeshwa nje ya Kituo cha Polisi cha Wami.
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa mitaro katika barabara mpya ya mabasi ya Kaskazini, inayotokea Bagamoyo.
 Jamaa wakilinda mzigo wao nyuma ua Canter, kutoka Soko la Kariakoo kuelekea Tegeta.
 haikuweza kufahamika jamaa hawa walikuwa wakisafiri kwa staili hii kuwa walikuwa na matatizo ya kijamii au ndo tatizo la usafiri, hapa wakitokea bagamoyo kuelekea Chalinze katika barabara mpya....
 Ni baadhi ya wachezaji wa Taswa Fc, waliposhuka kupata chakula cha mchana maeneo ya Korogwe wakati wakielekea Mkoani Arusha kushiriki Bonanza linaloandaliwa na Taswa Arusha kila mwaka.
 Safari hiyo ilijumuisha timu zote mbili ya Taswa Fc na Taswa Queens....
 Wachezaji wakishuka garini kuelekea kupata msosi....
 Maeneo ya mbali na mijini hivi ndivyo vituo vya mafuta ambapo huuzwa kwa lita moja moja kama hivi...
Mafuta aina ya Petroli, yakiuzwa kwa staili hii jambo ambalo ni hatari....

*AJALI HAINA KINGA

 Baadhi ya abiria waliokuwa katika gari lililogongana na gari ndogo (pichani chini) wakilia baada ya kutokea ajali karubu kabisa na maeneo ya njia panda ya Kunduchi, wakati mabinti hao na wenzao wakiwa safarini kuelekea Bagamoyo kama kundi kuhudhuria Bonanza la familia, mwishoni mwa wiki iliyopita. 
Baadhi ya abiria waliokuwa katika Coaster hilo, na mashuhuda wakijadili alaji hiyo. Katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa zaidi ya magari kuumia.

*ANGALIA AKILI YA DEREVA HUYU v/s MNYAMA HUYU

 Hapa ilikuwa ni barabara mpya inayotokea Bagamoyo kuelekea mikoa ya Kaskazini inayochomokea njia panda ya Chalinze, ambapo Mnyama huyu alikuwa akikatiza barabara kuelekea upande wa pili wa barabara hiyo, huku (kushoto) ni Lori lililokuwa katika mwendo na (kulia) mwa Lori hilo ilikuwa ni Coaster iliyokuwa ikijaribu kulipita Lori hilo.

Wakati Coaster ikikaribia kumaliza bodi ya Lori ndipo Mnyama huyu akatokea upande wa pili akivuka huku akikimbia kwa mbwembwe akiruka ruka jambo lililowafanya abiria waliokuwa katika Coaster kumfurahia huku wakimsikitikia  kuwa huenda asingewahi kuvuka kabla ya kulambwa tairi na Lori.

Lakini wakati abiria hao wakifurahishwa na Mnyama huyu ambaye alikuwa mithili ya Nyani, ghafla Dereva wa Lori aliwashangaza watu baada ya kutumia bodi kubwa ya Lori lake lililokuwa na tera 'Eti' kumkatia denge mnyama huyo ili amkanyage na ndipo Lori hilo liliyumba na kutaka kuanguka huku likitoka nje ya Barabara huku mnyama huyo akikatiza kiulaini na kuondoka zake.

Sasa sijui kama Dereva huyu angeangusha gari angejieleza alikuwa akifanya nini, au angeelezeaje sababu za kuangusha gari. MADEREVA, UTULIVU, AKILI NA BUSARA MUWAPO BARABARANI NDIYO KITU CHA KWANZA.
Hapa Lori hilo likitoka nje ya Barabara kumkatia denege mnyama huyo, ambapo lilimkosa na kuyumba wakati likijitahidi kurudi barabarani na kutaka kusababisha ajali kwa kuigonga Coaster iliyokuwa pembeni yake.

*SALAAM ZA PONGEZI KUTOKA MMK MEDIA GROUP

MMK MEDIA GROUP SWAHILI TV, SWAHILI RADIO na DMK411
Tunatoa pongezi zetu za dhati kwa mwana habari mwenzetu ndugu Issa Michuzi na Blog yake ya www.issamichuzi.blogspot.com kwa kazi kubwa walioifanya na wanayoendelea kuifanya ya kuhabarisha jamii yetu kwa muda wa Miaka tisa (9) mfululizo bila kupumzika.

Blog ya Issa Michuzi imetimiza miaka 9 tangu kuanzishwa  tarehe 8 Septemba 2005 jijini Helsinki, Finland.  Kwanza kabisa; tunampa hongera Ndugu  Michuzi kwa kuandika historia kwa kuleta mapinduzi ya habari ndani nchini na nje ya Tanzania.

Pili; tumefurahishwa sana kwa kitendo cha Ndugu Michuzi kurudisha shukrani na fadhila kwa Baba wa Ma-blog Bwana Ndesanjo Macha kwa kumtambulisha, kumuingiza na kumfungulia blog ya jamii ya  www.issamichuzi.blogspot.com mnamo tarehe 8 Septemba 2005 jijini Helsinki, Finland. 
Tatu; Pongezi za kipekee zimuendee Ndugu Issa Michuzi kwa kazi kubwa ya kutuhabarisha usiku na mchana pamoja na majukumu yake ya  kikazi akilitumikia vyema Taifa letu la Tanzania katika Ofisi Kuu kuliko zote akiwa kama  Mwanahabari Mpiga Picha (Photo Journalist) mwajiriwa wa Serikali akifanya kazi chini ya  Kurugenzi ya Mawasiliano, Ofisi ya Rais Ikulu ya Tanzania.

Nne; Ni ukweli usiopingika kwamba Issa Michuzi ni mtu wa watu, anapenda watu na ucheshi wake umemletea mafanikio makubwa katika tasnia ya habari. Kwa upande mwingine Michuzi ameitumia vyema nafasi ya kipekee aliyopata kutuhabarisha kwa kutujuza mambo mbalimbali yanayoendelea ndani na nje ya nchi. Hakuna ubishi tukijiuliza swali ni wafanyakazi wangapi waliopo sasa hivi Serikalini katika nafasi kama ya  Michuzi, ama waliopita ambao wamefanya mapinduzi ya habari kama Michuzi? 
Ndugu msomaji, ukweli unabaki palepale Michuzi anastahili pongezi za kipekee kwa kuthubutu.

Mwisho kwa kumalizia napenda kuufahamisha Umma kwamba  Bwana Issa Michuzi amekuwa mfano wa kuigwa na jitihada zake na mazingira yake kikazi yamekuwa chanzo cha mafanikio na umaarufu mkubwa aliojizolea na kujijengea jina nchini na nje ya nchi. Hongera kwa jitihada na harakati zako.

Tunatambua pia kwa nafasi uliyonayo kikazi inakupa mlango wa kupata habari kabla ya vyombo vingine vya habari kupata,  na vilevile kwa kuwa mwajiriwa wa Serikali umejijengea heshima kwa taasisi, wizara na vyombo vingine vya Kiserikali kukuleletea habari zao moja kwa moja wewe kwanza kabla ya vyombo vingine, kitu ambacho kimefanya watu wengi tuwe tunasoma blog yako na kuipenda kitu ambacho ni kuzuri na cha kuigwa.

Mwisho tunakuomba ukaze mwendo na uendelee kutuhabarisha

Monday, 9 September 2013

ISLAMIC BANKING YA NBC KUPELEKA WATEJA WAWILI NA WENZA WAO HIJJA


 Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Kufuata Kanuni za Kiislamu (Islamic Banking), wa Benki ya NBC Tanzania, Yassir Masoud (katikati) akizungumza katika droo ya awamu ya pili  kupata washindi wawili waliojishindia safari wao na wenza wao inayolipiwa kila kitu na NBC kushiriki ibada ya Hija mjini Makka nchini Saudi Arabia baadae Mwezi ujao. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo, Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
 Meneja Uhusiano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Eddie Mhina akipiga simu kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya Islamic Banking ya benki hiyo ambayo washindi wawili na wenzao wao watalipiwa gharama zote kwenda Makka nchini Saudi Arabia kushiriki ibada ya Hijja baadae mwezi ujao. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo, Kaimu Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
 Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein (katikati) akihakiki majina ya washindi wa kampeni hiyo. Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata kanuni za Kiislamu wa NBC, Yassir Masoud na Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria hafla hiyo.
Kaimu Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akifurahi pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakati baadhi ya washindi wakielezea furaha yao baada ya kupigiwa simu na kujulishwa kujishindia safari ya kwenda hijja itakayolipiwa kila kitu na NBC. Kutoka kushoto ni Ofisa katika Idara ya Operesheni, Edesia Kahyarara, Meneja Masoko, Alina Maria Kimaryo, Meneja Uhusiano, Eddie Mhina na  Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.