Monday, 9 September 2013

KIWANDA CHA KWANZA CHA KUCHAMBUA TAKA CHAZINDULIWA GONGO LA MBOTO JIJINI DAR


IMG_5586
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimlaki mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa alipowasili kukagua kiwanda kipya na cha kwanza nchini Tanzania cha kuchambua taka (KIKUTA) kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar..
IMG_5606
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Gongo la Mboto mara baada ya kuwasili kiwanda cha KIKUTA.
IMG_5615
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa kuznugmza na wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto.
IMG_5644
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce Msenduki akisoma taarifa ya kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA) mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa alipotembelea kiwandani hapo kukagua juhudi zinazofanywa na Manispaa ya Ilala.
IMG_5586
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Gongo la Mboto Bw. Alphonce Msenduki akikabidhi taarifa ya kiwanda hicho kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa.
IMG_5654
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akizungumza na wakazi wa Gongo la Mboto wakati alipotembelea na kukagua kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA) kilichopo Gongo la Mboto jijini Dar.
Mh. Dkt. Huvisa amempongeza Diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni Meya wa Halamshauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwa jitihada zake za kuhamasisha usafi kwenye Manispaa yake na kuzitaka Manispaa zingine kuiga mfano wa Manispaa ya Ilala ambapo pia amewahamasisha wakazi wa Gongo la Mboto kutunza Mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na manadiliko ya tabianchi yanayopelekea ongezeko la Joto duniani.
IMG_5674
Pichani juu na chini ni Baadhi ya wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (hayupo pichani).
IMG_5638
IMG_5608
Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa wakati wa halfa hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gongo la Mboto Bw. Moshi Mwaluko.
IMG_5700
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) akielekea kukagua kiwanda hicho akiwa amembatana na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kushoto) pamoja na Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa (kulia).
IMG_5714
Mh. Dkt. Terezya Huvisa akiangalia maji ya michoro iliyopo katika kiwanda hicho inayohamasisha suala utunzaji wa Mazingira majumbani.
IMG_5725
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi kiwanda hapo namna wanavyotengeza Mbolea kwa kutumia taka zilizooza.
IMG_5736
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akingalia Mbolea iliyozalishwa kiwanda hapo tayari kwa matumizi.
IMG_5747
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akikagua kifaa kinachotumika kuchambulia taka kwa ajili ya kuzalishwa upya kiwandani hapo.
IMG_5780
Mratibu wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and Development Bi. Larissa Duma (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa (katikati) alipotembelea na kukagua kiwanda cha KIKUTA. Kushoto ni Diwani wa kata ya Gongo la Mboto na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
IMG_5808
Mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa kwenye picha ya pamoja na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha kuchambua taka (KIKUTA).
IMG_5823
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Terezya Huvisa akiagana na Mratibu wa Jamii na miradi kutoka Bremen Overseas Research and Development Bi. Larissa Duma.

Manispaa ya Ilala katika Kata ya Gongo la Mboto imezindua kiwanda cha kuchambua taka chenye uwezo wa kutengeneza Mbolea, Mboji na bidhaa mbalimbali zitokanazo na taka ngumu na nyepesi.
Kiwanda hicho awa kilijulikana kama kituo cha kutupia taka (KIKUTA) ambacho kilijengwa na mfadhili Bremen Overseas Research and Development kutoka Canada.
Kiwanda hicho cha kipekee kimetokana na juhudi za wakazi wa Gongo la Mboto na Kikundi cha Gongo la Mboto Youth Group wakisaidiana na viongozi wao na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
Kiwanda hicho kitatoa ajira kwa vijana ili kujikwamua kwenye lindi la umaskini.

WAHITIMU WA DARASA LA SABA NEW VISION YA IZIMBYA BUKOBA VIJIJINI WAAGWA

           wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi new vision ya izimbya wakitabasamu
                                             wanafunzi wa darasa la saba wakicheza kutikuti

                                               wanafunzi wakipokea vyeti vya kihitimu kwa mgeni rasmi
 kulia ni mkurugenzi wa shule ya msingi ya new vision na mkewe akitoa neno la shukrani kwa wazazi
                                  wanafunzi wanaohitimu katika muonekano wa kupendeza,shule hii ya msingi new vision ni ya bweni,ambayo iko izimbya na kitaaluma imekuwa ikifaulisha wanafunzi wote  na kiwilaya imekuwa ikiongoza kwa kipindi cha miaka mitatu,pia inapokea watoto wa chekechea
                          wazazi wakiwazawadia watoto wao na kuwapongeza kwa hatua hii
 bw Amosi rweyemamu akimzawadia na kumpongeza mmoja wa wanafunzi zaidi ya 60 wanaolipiwa karo na umoja wao ulioko spain, wamekuwa wakilipa karo kwa watoto yatima,watoto waliopoteza wazazi waliofariki kwa ukimwi nk.
 mama mzazi wa Amos rweyemamu akimpongeza mwanafunzi

 huyu mama akimpongeza mwanae ambae alitoa machozi, na kusema mwanae ameugua kwa kipindi kirufu na kusom kwa shida sana ,lakini anashukuru leo amefikia hatua hii, hivyo anakumbuka mengi ndo maana anatoa machozi,na mtoto nae alitoa machozi.
                                                                mgeni rasmi akitoa nasaha
                                                                 safari ndio imeanza....
                                                mama mzazi wa amos rweyemamu katika pozz
 Bw Amos rweyemamu yeye na wenzake wanaoishi spain wanalipa karo za zaidi ya wanafunzi 60 katika shule ya new vision izimbya
 wanafunzi wakipata chakula,shule hii iko kijijini kabisa ,pamoja na mazingira magumu ila wanafanya vizuri sana katika taaluma
kwa  elimu bora peleka mwanao  new vision pre & primary schooliliyoko izimbya bukoba vijijini

PICHA ZA MWANAMKE ALIEUWAWA KIKATILI


Mrembo Yusta Mkali, mkazi wa Kawe, Dar ambaye alikuwa mke wa mtu anadaiwa kuuawa kwa kutobolewa koromeo na mumewe, Musa Senkando na kusababisha simulizi ya kutoa machozi kisa kikielezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Polisi wa kituo cha Kawe wakiukagua mwili wa marehemu Yusta.
Mtuhumiwa wa mauaji, Musa Senkando.
Mwili wa marehemu Yusta ukipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Marehemu Yusta Mkali enzi za uhai wake.


Wakazi wa Kawe wakiwa na simanzi wakati mwili wa marehemu ukipelekwa hospitali.

“Huu ni unyama wa ajabu sana. Haya mapenzi ni ya kuyatazama sana. Ona sasa mwanaume amemuua mkewe. Inauma sana,” alisema mama Jack ambaye ni jirani wa familia hiyo.
Mtoto wa marehemu aitwaye Baraka Simon akiaga mwili wa mama yake kwa simanzi jana.
Ilikuwa ni simanzi na majonzi wakati wa kuaga mwili wa marehemu Yusta, jana katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kabla ya kuusafirisha kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi

WANAHABARI TUJITOKEZE KUMSAIDIA MWENZETU ZUBERI MUSSA- MPIGA PICHA WA MAGAZETI YA NEW HABARI ANAYESUMBULIWA NA UGONJWA WA AJABU


 Zuberi Mussa  katika mwonekano wa picha tofauti 
tofauti nje ya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mazinde.
Zuberi Mussa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi Dotto Mwaibale (kushoto), Mashaka Kibaya (kulia) wote wa Gazeti la Jambo Leo na Mashaka Mhando wa Gazeti la Majira mkoani Tanga, walipokwenda kumjulia hali kijjiini kwao.



Zuberi Mussa ambaye ni mpiga picha mkongwe katika vyombo mbalimbali vya habari nchini ambaye kwa sasa anafanyakazi Kampuni ya New Habari ni mgonjwa anayehitaji msaada wa hali na mali.

Kikubwa kinacho msumbua mwandishi mwenzetu huyu ni ugonjwa ambao bado haujafahamika ambapo kwa mtu anayemfahamu ni rahisi kumgundua kuwa ana matatizo ya kiafya kwani katika kila sentesi yake ya pili na ya tatu wakati wa kuongea naye hautaelewana naye kutokana na matamshi yake ambayo hayafahamiki yanayoonesha  kama mtu aliyechanganyikiwa.

Kutokana na kukosekana kwa fedha za kumsaidia katika matibabu hasa Hospitalini, Zuberi Mussa amelazimika kwenda kupata matibabu yake kwa waganga wa jadi.

Wakati Zuberi akiwa kijijini kwao Kata ya Mazinde wilayani Korogwe mkoani Tanga bila ya kuwa na msaada wowote mke wa mwenzetu huyo aitwaye Rehema Amir kwa kipindi cha mwaka mzima yupo hoi kitandani kutokana na maradhi ya kupooza yaliyompata mwanzoni mwa mwaka jana akiwa jijini Dar es Salaam, hawezi kufanya chochote ikiwa ni pamoja na kuongea hakika inaumiza na kusikitisha.

Ndugu wanahabari kila mmoja wetu kwa imani yake na utamaduni tulionao wa kusaidiana tujitokeze kumsaidia mwenzetu huyu ambaye anapita katika kipindi kigumu.

Binafsi nilipofika kumuona kwa mara ya kwanza wiki iliyopita nilishitushwa na hali aliyokuwa nayo ingawa kaka yake aitwaye Waziri Mussa anayemuuguza alidai kuwa alikuwa amepata nafuu.

Zuberi alifika katika eneo nililokuwepo akiwa katika hali ambayo si ya kawaida zaidi ya kusalimiana na kunitambua mengine yote nilioongea naye hatukuweza kuelewana. Kwa mtu yeyote atakayependa kumsaidia Zuberi pamoja na mke wake kipenzi  Rehema Amir anaweza kuwasiliana na Dotto Mwaibale kwa namba 0712-727062 ambaye atakuunganisha na kaka yake.

Ndugu wanahabari wenzangu  na mtu mmoja mmoja, Taasisi yoyote, shirika lolote, Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya, Wafanyabiashara, Makampuni mbalimbali na vyama vya michezo  hima tujitoe kimasomaso kumsaidia mpiga naji mwenzetu Zuberi Mussa na mke wake waondoke katika matibabu ya jadi wanayopata kwa waganga wa kienyeji badala yake wapelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi wa afya zao kwani kutoa ni moyo na si utajiri.

KINANA, NAPE KUWASILI SHINYANGA KESHO SAA TATU ASUBUHI

Sep 9, 2013
Ndugu Kinana
SHINYANGA, Tanzania
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana kesho Jumanne, ataanza ziara ya siku nne mkoani Shinyanga kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM na uhai wa Chama.

  akiwa mkoani Shinyanga Kinana atakagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika wilaya zote za mkoa huo sambamba na kutoa kadi kwa wanachama wapya wa CCM ambapo pia atafanya vikao vya ndani ikiwa ni moja ya mikakati ya uimarishaji wa chama mkoani humo.

Katibu wa CCM mkoani Shinyanga, Adam Ngalawa amesema leo kwamba Kinana na msafara wake akiwemo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye, wanatarajiwa kupokelewa kesho saa 3 asubuhi katika kata ya Isaka wilayani Kahama wakitokea Nzega mkoani Tabora.

Ngalawa alisema baada ya kupokelewa kwa Katibu Mkuu akiwa katika kata ya Isaka atasaini kitabu cha wageni na kisha atapokea taarifa ya utekelezaji wa kazi za CCM za wilaya ya Kahama na mkoa kwa ujumla pamoja na taarifa ya serikali ya mkoa.

Akiwa katika kata hiyo Kinana atagawa kadi za CCM kwa wanachama wapya na kisha atawasalimia wananchi kabla ya kuelekea katika kata ya Mwendakulima ambako atakagua miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya cha Mwendakulima.

Katibu mkuu huyo akiwa mjini Kahama atafanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya CCM kata ya Majengo, kufungua shina la wakereketwa la Mkombozi SACCOS Majengo pia atakuwa na kikao cha ndani na viongozi wa kata, matawi, mabalozi, wazee na madiwani wa CCM wilayani Kahama.

Kesho mchana Kinana atakuwa na mkutano wa hadhara katika eneo la uwanja wa CDT ambapo keshokutwa jumatano ataelekea wilaya ya Shinyanga ambako atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo katika wilaya hiyo na kushiriki katika ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo pia atakuwa na mkutano wa hadhara katika kijiji cha Salawe.

Pia katibu huyo ataendelea na ziara yake katika wilaya za Kishapu na Shinyanga manispaa ambako pia atakuwa na shughuli za kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama ilivyoainishwa ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

Kinana ataondoka mkoani Shinyanga Septemba 14, mwaka huu kwenda katika mkoa mpya wa Simiyu ambako pia atafanya shughuli za kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM na uimarishaji wa chama katika wilaya zote za mkoa huo.

Makamu wa Rais afungua maonesho ya nyaraka za kitaifa na kumbukumbu za Oman jijini dar leo


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye ufunguzi wa maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia nyaraka za aina kumbukumbu mbalimbali kwenye maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman mara baada ya kufungua maonesho hayo leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Hifadhi ya kumbukumbu za Kitaifa za Oman Dk.t Hemed Mohammed Al-Dhawyani kwenye ufunguzi wa maonesho ya nyaraka ya kitaifa na kumbukumbu za Oman yaliyofanyika leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa maonesho ya kumbukumbu za nyaraka ya kitaifa za Oman mara baada ya kufungua maonesho hayo leo Sept 09-2013 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam

Majeshi ya MONUSCO Yanayoongozwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Yalivyochakaza Ngome ya Kikundi cha Waasi cha M23


Mwanajeshi wa Jeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)MONUSCO yanayoongozwa na Wanajeshi Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)akiwa kwenye Mapigano ndani ya Kibati.
Kazi ni moja tu, nayo ni Kongo kuwa huru, vijana shupavu wanawajibika pichani ni Mwanajeshi wa Jeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)MONUSCO yanayoongozwa na Wanajeshi Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)akiwa kwenye Mapigano

Majeshi ya MONUSCO yanayoongozwa na Wanajeshi Kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ),yakidhibiti eneo la Kibati ilipokuwa ngome ya M23.  Picha Zote na Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)-Upanga