Wednesday, 4 September 2013

WAZEE WA YANGA WAJA JUU KUHUSU KATIBU MPYA WASEMA HANA NAFASI YANGA




Baraza la wazee wa YANGA limesema halimtambui katibu mpya wa YANGA aliyeletwa na kumuondoa  katibu aliyekuwepo RAWLENCE MWALUSAKO kwani viongozi waliomleta wamekiuka katiba ya YANGA.

IBRAHIM AKILIMALI ambaye ni katibu wa baraza la wazee amesema wamepata taarifa za kuondolewa kwa katibu wa YANGA wa zamani RAWLENCE MWALUSAKO jambo ambalo wamepinga vikali 


Baadhi ya wazee wa YANGA wamesema walikutana na katibu mpya klabuni katika mahojiano naye akashindwa kumtaja mtu aliyemleta kufanya kazi .


Baraza la wazee YANGA limesema halikatai kuletwa viongozi wapya bali uongozi wa YANGA ufuate taaratibu za katiba ya YANGA inavyotaka ikiwemo kutoa taarifa kwa kamati mbalimbali za YANGA ili zifahamu mabadiliko katika uongozi.
Wamesema katiba ya YANGA inataka kiongozi yoyote awe ni mwanachama halali wa YANGA na anafahamu taratibu za YANGA ndipo atafanya kazi

KWA MARA YA KWANZA TANZANIA YAPATA KIKAO RASMI EALA, KIKAO KIMOJA KUFANYIKA DODOMA AU DAR

IMG_6554
Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Mhe. Adam Kimbisa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo, Mh. Shy-Rose Bhanji, mbunge wa bunge hilo, Mh. Nderakindo Kessy na kulia ni Mhe. Makongoro Nyerere.
IMG_6512
Katibu wa wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mh. Shy-Rose Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhe. Nderakindo Kessy na Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Adam Kimbisa.
IMG_6549
Nasisitiza.....
IMG_6565
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania wakibadilisha mawazo baada ya mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania,Mh. Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti, Mh. Adam Kimbisa, Mh. Nderakindo Kessy na Mh. Makongoro Nyerere.
IMG_6570
Mbunge la Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania Mh. Makongoro Nyerere akipeana mkono na Katibu wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Shy-Rose Bhanji.
Na.Habari Mseto Blog.
Bunge la tatu EALA limeridhia Tanzania kupata kikao chake rasmi ambapo sasa kikao kitafanyika Dodoma na vikao vingine viwili kufanyika Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, mhe. Adam Kimbisa amesema hayo katika mkutano na wabunge watanzania EALA, na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo.
Mhe. Kimbisa amesema katika ratiba ya vikao vya Bunge la EALA, Tanzania pia imepata rasmi kikao kimoja ambapo sasa kitafanyika mjini Dodoma.
Vile vile amesema kikao hicho kinaweza kufanyika Dar es Salaama au Zanzibar.
Amefafanua kwamba, Bunge limeridhia vikao viwili vifanyike Arusha, kimoja kifanyike Tanzania sambamba na nchi zingine wanachama; Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kupata kikao kimoja kila nchi kwa mzunguko.
Amesema nchi ambayo itakosa kikao kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014, ndio itakuwa nchi ya kwanza kupata kikao cha mwaka ujao wa fedha.
Hata hivyo amesema, vikao vikao viwili vya Arusha vitakuwa ni vikao vya bajeti na ukaguzi wa mahesabu ambavyo ni vikao muhimu sana katika Bunge.
Mhe. Kimbisa amesema kikubwa wananchi wanachotakiwa kufahamu ni kuwa linapokuja suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha ni Makao Makuu na kwamba haiko Tanzania kwani nchi zote tano ni wadau wa Arusha.
Naye Katibu wa watanzania,Mh. Shy-Rose Bhanji amesema ni jambo la kujivunia kwamba Tanzania sasa itakuwa na kikao rasmi kwa njia ya mazungumzo. Hii ni hatua nzuri vile wananchi pia watapata mwamko wa masuala yanayojadiliwa Bungeni.
Hatua ya maridhiano hayo imefuatia mgoghoro ulioibuka miongoni mwa wabunge wa EALA kwamba vikao vya Bunge hilo vifanyike Arusha kwa mwaka mmoja wa fedha na si kwa mzunguko kama ilivyozoeleka kuanzia Bunge la pili.
Wabunge wengi isipokuwa watanzania walitaka vikao viendelee kwa mzunguko nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Arusha.
Vikao vya EALA hadi mwaka wa fedha June 2012/June 2013 vilikuwa vitano kwa mwaka. Vikao hivyo vimeongezeka kuwa sita. Vikao hufanyika kila baada ya takriban miezi miwili, kwa kipindi cha wiki mbili.

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MAKAMU WAKE DKT. BILAL WAWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI YA KAKA WA WAZIRI MSTAAFU MAOKOLA MAJOGO.


Tuesday, September 3, 2013

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mke wa Rais Mama salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo.
  Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mke wa Rais Mama salma Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, wakijumuika na waombolezaji wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akiwafariji wafiwa wakati alipofika kuaga mwili wa marehemu, Meinrad Diones Maokola, ambaye ni Kaka wa Waziri Mstaafu, Maokola Majogo, aliyefariki jana jijini Dar es Salaam. Shughuli ya kuagwa mwili wa marehemu ilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam leo.

Tuesday, 3 September 2013

JERRY MULO ATEMBELEA SHULE YA WASICHANA YA JOSIAH GIRL'S HIGH SCHOOL

Kwa siku chache mimi(Jamal kalumuna) nilizobahatika kuwa na mwandishi huyu Jerry Mulo nimeweza kuona utendaji kazi wake na umakini mkubwa kwa kile anachokifanya,lakini pia mimeshuhudia sehemu alizokuwa akifika jinsi watu walivyompa pongezi nyingi na wale waliokuwa hawjawahi kumuona ana kwa ana wanakuwa na shauku ya kumsalimia na kumpongeza kwa kazi zake ambazo amekuwa akifanya na kuonyeshwa katika vituo mbalimbali vya tv hapa nchini na nje ya nchi.Hali hii binafsi ilinifanya nijitahidi sana kuwa karibu na mtu huyu kwa nia ya kujifunza namna anavyofanya kazi zake,ndipo nikabahatika kutinga nae ghafla bini vuu katika shule ya sekondari ya  wasichana  josiah girl's yenye kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita iliyoko katika kata ya ijuganyondo manispaa ya bukoba mkoa wa kagera,Hapo ndio nikaweza kushuhudia utendaji wa Jerry Mulo,mpendwa msomaji nimekutana na waandishi wengi na hasa wale kwa kiasi fulani hujiona wako juu kuliko wenzao huyu ni tofauti,nimeshudia akiohi maswali  yake na wakati mwingine kushika camera mwenye  ili aweze kufanya kazi yake vizuri. lakini kikubwa  leo katika habari hii  ni kujua  namna kampuni ya yokama ilivyoamua kwa mapenzi ya dhati kumpa mtoto wa kike elimu bora , na kumkomboa mwanamke katika wimbi la ujinga na kumuendeleza ili hapo badae wapatikane wataalamu wengi wa kike katika nyanja tofauti katika taifa la Tanzania na duniani kwa ujumla, na ndio maana ipo sasa Josiah girl's high school,yenye kidato cha kwanza mpaka cha sita.
Jerry mulo akiwa ametinga ghafla katika ofisi ya mkuu wa shule ,Alvera kashushura na kuanza mazungumzo
kazi ikiendelea hapo ni mwalimu wa taaluma Aziaki wangwa akieleza swala zima la kumuelimisha mtoto wa kike
                                     wanafunzi wakiwa darasani,hawa ni kidato cha pili
                   josiah girl's wameona mbali zaidi katika teknologia, maana hujifunza hata kwa njia ya tv
                                                     baadhi ya walimu wakiwa na furaha
                                 wanafunzi wakiwa mahabara wakijifunza kwa vitendo
                      mwanamke anaweza,wanachangaya chemical, ni masomo ya sayansi
                      Jerry mulo akiwa katika harakati zake za kazi hapo josia girl's high school
            Josiah girl's high school asikwambie mtu , wameshaona mbali wapo kididital zaidi usipime
                            jerry mulo akiwa na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita
m,walimu akifundisha kwa njia ya tv, mitaala yote imeingizwa kwenye computer na mwalimu anafanya kazi zake kirahisi na kwa ufanisi mubwa, mlete mwanao wa kike josiah girl's kwa elimu bora
                                                              mambo ndo kama hivyo kwenye tv
wanapata chakula,jumapili  kama nyumbani kwa wengine ni zaidi ya nyumbani ,ni pilau, nyama, na kuku kidogo
                                                    hakusita kupata nao msosi jerry mulo
ndugu msomaji fuatilia jamco bukoba .blogspot.com,nilipata wasaa wa kumuuliza jerry mulo yale matukio yake ya hatari ya trafiki nk ,nilitaka kujiridhisha picha alikuwa akizipiga vipi,hana iyana akanieleza na kunipa mbinu ,kaani chonjo Jerry mulo wa bukoba anakuja
MJADALA wa Bunge jana jioni ulitawaliwa na kauli nzito baada ya wabunge kadhaa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutuhumiana kuhusika na ubadhirifu katika vyama vya ushirika nchini.

Hoja hiyo iliibuka wakati Bunge likijadili muswada wa sheria ya vyama vya ushirika wa mwaka 2013 uliowasilishwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Balozi Christopher Chiza.
Aliyekuwa wa kwanza kuwasha moto huo baada ya mapumziko ya mchana alikuwa mbunge wa Busega, Dk.Titus Kamati (CCM), ambaye alisema waziwazi kuwa wanasiasa ndio wezi wa vyama vya ushirika.
Dk. Kamani alihoji ni kwa nini serikali inapata kigugumizi kuwachukulia hatua wahusika na kusisitiza kuwa hapo kuna kulegalega kumaliza ufisadi katika ushirika.
“Wanasiasa hawa kwa nafasi zao wameingia kwenye ushirika na kufanya ufisadi lakini serikali inashindwa kuwachukulia hatua.
“Huku ni kulegalega na ndio maana hata tumeshindwa kuwataja wauza dawa za kulevya, waziri anaishia kusema tunayo orodha,” alisema.
Alihoji ni kwa nini sasa serikali isiige mfano wa China wa kuwafunga na hata ikibidi kuwanyonga watuhumiwa wa ufisadi wa vyama hivyo ikithibitika bila kujali nafasi zao kwenye siasa.
Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso (CCM), ndiye aliyefuata na kuchafua hali ya hewa kwa kumtuhumu Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku Nchini (TTB) kufanya ufisadi mkubwa ambao serikali inaujua lakini imeamua kuunyamazia.
Bila kumtaja kwa jina lakini alikuwa akimlenga mbunge mwenzake wa Namtumbo, Vita Kawawa, akisema kuwa anajilipa mshahara mara mbili ya ule uliopitishwa na serikali.
Alisema kuwa analipwa sh milioni mbili za mawasiliano na anachukua dola 1200 (zaidi ya sh milioni 1.8) kwa ajili nyumba badala ya sh 800,000 zilizoidhinishwa.
Mbunge huyo alisema mwenyekiti huyo anayajua mambo hayo na ndiye aliyeidhinisha.
“Nina uhakika na ninachozungumza, waziri nilishamletea taarifa juu ya jambo hili lakini amenyamaza, hivi hapa tunategemea ushirika utakuwa hai wakati mabosi wanautafuna?” alihoji.
Wakati mbunge huyo anaendelea kuzungumza, Kawawa akitaka kumpa taarifa juu ya jambo analolizungumza.
Kawawa alisema muda wake wa kuwa mwenyekiti kwenye bodi hiyo uliisha Juni 31 mwaka huu, hivyo ni vema mbunge mwenzake akatoa ushahidi wake juu ya tuhuma za watendaji wa bodi husika.
Baada ya Kawawa kumaliza, Kakosa aliendelea kuchangia ambapo alikataa taarifa hiyo kwa madai ana ushahidi wa kile kilichofanyika.
Mara baada ya Kakoso kumaliza kuchangia muswada huo, mbunge wa Kondoa Juma Nkamia alipewa fursa ya kutoa taarifa ambapo alisema tuhuma zilizotolewa na Kakoso dhidi ya Kawawa ni nzito sana na Bunge lipate fursa ya kuangalia jambo hilo pamoja na mhusika kutoa ushahidi.
Naibu Spika, Job Ndugai, alisema ofisi ya Bunge iko wazi kwa Kakoso kuwasilisha ushahidi wake juu ya kile alichosema.
Mara baada ya Ndugai kutoa ufafanuzi huo, alimpa nafasi mbunge wa Sikonge, Saidi Nkumba (CCM), ambaye alimtuhumu Kakoso kwa kushindwa kuliambia ukweli Bunge kuwa yeye ni Mwenyekiti wa Chama Kilele (APEX) ambacho kinapigiwa kelele kuwa kinawanyonya wakulima.
Alisema wakiwa Dar es Salaam kwenye vikao vya kamati za Bunge, Katibu wa Apex, aliitwa katika kamati kama mdau ambapo alipobanwa juu ya wizi unaofanyika kwenye chombo hicho alisema serikalini ikiiba kelele zinapigwa lakini APEX ikiiba kidogo kelele zinakuwa kubwa sana.
“Katibu wa Kakoso ndiye aliyetuambia hivyo. Huu ni wizi, sisi hatuwezi kukubaliana na jambo hilo, serikali haivumilii wizi, huyu Kakoso anasema APEX ni mkombozi lakini pale Tabora wamewaibia wananchi bilioni 16, hivi kweli hizi si fedha nyingi?
“Hii APEX ni lazima ifutwe, wenye tamaa ya kwenda kwenye ushirika ni vema waache siasa, na wenye ushirika ni vema wakabaki huko huko.”
Alibainisha kuwa wizi unaofanyika kwenye vyama vya ushirika unasababishwa na wanasiasa ambao wana kinga za kisiasa ndiyo maana wanaendelea kutafuna fedha za wananchi.
Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali, alisema wabunge wana taarifa za wizi wanatoa taarifa hapa bungeni lakini hakuna wanachokifanya.
“Yaani kila kukicha mnalea wizi halafu leo hii mnaanzisha tume za kuwanyonya wakulima, kule kwangu wakulima waliuza tumbaku, msianzishe vitu vya ajabu ajabu…, huu ni wizi mtu, msituletee wizi hapa kwa kubadilisha majina ya vitu,” alisema.
Tundu Lissu wa Singida Mashariki (CHADEMA) alisema sababu kubwa ya kuporomoka kwa ushirika ni serikali kuuingilia, kuudhibiti na kuuporomosha.
Alisema serikali ilianza kuvuruga mambo 1966 sheria za ushirika ilibadilishwa na msajili wa vyama vya ushirika alipewa mamlaka ambayo alianza kuyatumia vibaya ambapo mwaka 1976 alipigwa marufuku zikaja bodi za mazao.
Mwaka 1982 vilirejeshwa vyama vya ushirika lakini mamlaka yake yalikuwa yakitolewa na mrajis ambaye ni serikali.
Mbunge wa Nzenga, Andrew Kigwangalah, aliibua upya mzozo wa awali kwa kuanika nyaraka za ufisadi katika TTB kama ilivyokuwa imedokezwa awali na Kakoso.
Kingwangalah ambaye alidai kuwa hatarudi nyuma kuwataja mafisadi na wauza dawa za kulevya alisema kuwa kodi ya nyumba ya mwenyekiti wa bodi inalipiwa gahara tofauti na ile iliyoidhinishwa.
Alionyesha nyaraka kadhaa za malipo ya viongozi wa bodi hiyo na kisha kumvaa Nkumba akisema kuwa tatatizo la nchi hii si Apex bali ni rushwa, wizi, ubadhirifu halafu watu wanaona wizi wanaungalia badala ya kuchukua hatua.
“Waliobaki kwenye ushirika ni wezi watupu, wazalendo wameisha, wezi tunawajua lakini hatuwawajibishi wala kuwachukulia hatua.
“Nkumba ni msaidizi wa Kawawa katika bodi ya tumbaku anajua ukaguzi haujafanyika na ukifanyika wao hawatasalimika ndiyo maana wanaanza kuipiga vita Apex.
“Kuna watu wanatumiwa na kampuni za ubebari ambazo zilikuwa zikisafirisha tumbaku na kusambaza pembejeo, hawa sasa wanaona hatari za kampuni zao ndiyo maana zinawatumia wabunge ili APEX ifutwe, tuwe makini na wabunge waovu,” alisema.
Mzozo huo ulidumu huku Kawawa na Nkumba wakisimama kujitetea bila mafanikio hatua iliyomlazimu Naibu Spika wa Bunge kutoa nafasi kwa baadhi ya wabunge kuomba viongozi, lakini akaliahirisha Bunge hadi leo ambapo atatoa uamuzi wake.
Mapema asubuhi, wabunge walipendekeza wabadhirifu wa mali za ushirika walazimishwe kufidia hasara iliyotokea pamoja na kufilisiwa mali zao.
Pendekezo hilo limetolewa na Nkumba alipokuwa akisoma hotuba ya Mwenyekiti wa 
Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Peter Msolla.
Nkumba alisema ushirika umewakatisha tamaa wananchi kutokana na ubadhirifu wa viongozi wake hivyo ujio wa sheria hiyo utakuwa mkombozi.
Aliongeza kuwa watuhumiwa wa ubadhirifu wa ushirika wafikishwapo mahakamani mashauri yake yamekuwa hayathibitiki licha ya taarifa za fedha kuonyesha kuwa upotevu fedha upo; ni vema kuwepo na utaratibu wa kuwabana wahusika.
Nkumba alisema vyama vya ushirika vimekuwa vikikaguliwa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (Coasco) ambalo halifanyi kazi zake vizuri na kuitaka serikali kuweka utaratibu mzuri ikiwemo kuhusishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali.
Waziri wa Kilimo, Chiza alisema kuundwa kwa sheria hiyo litakuwa suluhisho la matatizo ya ushirika nchini.
Alisema serikali inalenga kuifuta sheria ya vyama vya ushirika namba 20 ya mwaka 2003 na inaamini sheria mpya itaimarisha, kuendeleza na kuufufua ushirika.
Chiza alisema sheria ya ushirika ya mwaka 2013 ina lengo la kutekeleza sera ya maendeleo ya ushirika ya mwaka 2002, inayovitaka  vyama vya ushirika imara, endelevu na vyenye kukidhi mahitaji ya wanachama kiuchumi chini ya mazingira ya soko huria.

Monday, 2 September 2013

MKUU WA MKOA WA KAGERA KANAL FABIAN MASSAWE AFUNGUA KIWANDA CHA KUTENGENEZA NGUO KATIKA KATA YA KIBETA MANISPAA YA BUKOBA

 Mkuu wa mkoa wa kagera akiongea na wageni waalikwa katika ufunguzi wa kiwanda cha kutengeneza nguo Endeavour group ltd kilichopo kata ya kibeta bukoba manispaa,mkuu wa mkoa amewataka wahaya wote wenye uwezo wa kuwekeza waje waitengeneze bukoba sasa,kanal massawe amesema duniani kote ukienda utamkuta muhaya, na wanauwezo mkubwa,sasa umefika wakati wa kuwekeza nyumbani,amewataka wawe na uchungu na bukoba,ambayo asilimia kubwa ya ya majengo yake yamechakaa,na nyumba nyingi mabati yamekuwa mekundu ,na hicho ni kielelezo tosha kuwa bukoba inapaswa kubadilika.
 kati ni mkurugenzi wa kiwanda akimtambulisha meneja wa kiwanda kwa mgeni rasmi kanal massawe
 mgeni rasmi akiangalia namna mashine za kushona nguo zinavyotumika ,na kufanya kazi kwa haraka zaidi na kwa muda mfupi
                                  picha ya pamoja mbele ya jengo la kiwanda cha kutengeneza nguo
 mwenye miwani mzee mashasi,mkuuwa chuo kikuu jokuko keshomshahara akiteta na mgeni rasm
 mkuu wa mkoa kagera kanal Fabian massawe akikata utepe kuzindua rasmi kiwanda cha kutengeneza nguo
                                     mkurugenzi wa kiwanda akitoa maelezo kwa mgeni rasmi
 Ndugu paskazia barongo, mmoja mwa wawekezaji bukoba maispaa akiwa na mdau wa maendeleo manispaa ya bukoba
                                mgeni rasmi akiangalia nguo mbalimbali zinazotengenezwa kiwandani hapo
 kiwnda hiki kinashona sare za shule,masuti, nguo za watoto ,wanawake na wanaume,sare za mashirika ,makampuni,mahotel, sare za viwandani nk
                                  wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi rasmi wa kiwanda

MASANJA MKANDAMIZAJI AFUNGUKA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA NA SERIKALI KUSHIKILIA PASSPORT YAKE.



Masanja Mkandamizaji afunguka alipolonga na Vijimambo kuhusu kudaiwa kuhusika na madawa ya kulevya na kuhusu kushikiliwa kwa Passport yake na Serikali, MSIKILIZE

Hii ndio Nyumba ya Ghorofa ya Masanja Mkandamizaji inayomhusisha na madawa ya kulevya

Sunday, 1 September 2013

RWANDA YAPELEKA WANAJESHI 1700 KUWASAIDIA WAASI WA M23 BAADA YA KUELEMEWA NA JWTZ ( MONUSCO).

KIKUNDI cha waasi cha M23 kinachopambana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kimeripotiwa kupigwa vibaya na kutikisa nguvu za kikundi hicho kutokana na baadhi ya wapiganaji wake kuripotiwa kupoteza maisha.
 
Mapigano baina ya M23 na Jeshi la Serikali ya DRC linalosaidiwa na Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), yameibuka upya ndani ya wiki hii.
 
Habari za kiintelijensia  zinasema kuwa, kutokana na shambulio hilo, Serikali ya Rwanda imelazimika kuingilia kati kusaidia waasi hao kwa kupeleka bataliani mbili zenye jumla ya askari 1,700 huko DRC, ili waweze kukabiliana na nguvu ya majeshi ya JWTZ, DRC, Monusco na Brigedi ya Majeshi ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa yenye mamlaka ya kujibu mapigo (FIB).

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Rwanda imepeleka bataliani hizo mbili zenye askari 850 kila moja saa 48 zilizopita na kwamba wamevuka mpaka kuingia DRC katika eneo la Kibumba, lakini wanashindwa kusonga mbele.
 
Habari zaidi zinasema sababu ya Rwanda kupeleka askari wake hao ni kusaidia M23 ambao walipigwa sana Agosti 23 na 27, mwaka huu katika eneo la vilima vya Kibati na  kuikimbia ngome yao.
 
“M23 walitandikwa sana Agosti 23 na 27 katika eneo la vilima vya Kibati, na kulazimika  kuikimbia ngome yao, ndio maana sasa hivi Rwanda imepeleka batalioni zao kuwapa nguvu, lakini wanashindwa kusonga mbele maana hawajielewi kwa sababu ya kipigo walichopata,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
 
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, eneo la Kibati ndilo eneo kubwa la M23 ambalo wamekuwa wakitumia kuhifadhi silaha zao za kivita, lakini wakati wa mapambano majeshi ya JWTZ , DRC, MUNUSCO na FIB yalisambaratisha kabisa ngome hiyo ya waasi.
 
FIB inaundwa na askari wengi wa Afrika Kusini na Tanzania. Habari zaidi zinasema kwa sasa majeshi ya DRC, Monusco na FIB yanawasubiri kwa hamu askari hao wa Rwanda kuingia uwanja wa vita ili kukabiliana nao kama walivyokabiliana na waasi wa M23.
 
“Taarifa tulizonazo hivi sasa Rwanda inajiuliza iwapo isonge mbele kupambana au irudi nyuma, ikifikiria pia kipigo walichopata M23,” kilisema chanzo kimoja cha habari. 

Inaelezwa kwamba, kutokana na kipigo walichopata M23 siku chache zilizopita kimepelekea Rwanda kujikuta ikikiri na kusema ukweli juzi kuwa inakisaidia kikundi hicho cha waasi.