Wednesday, 7 August 2013

MAGEREZA MSHINDI WA KWANZA WA JUMLA MAONESHO YA NANE



photo 745b0
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza, Mlasani Kimaro akinyanyua juu Kikombe cha Zawadi ya Mshindi wa kwanza wa jumla katika Maonesho ya Wakulima-Nane Nane baada ya kukabidhiwa na Mgeni rasmi Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Iddi katika Kilele cha sherehe za Maonesho ya Nane Nane Kitaifa, yaliyofanyika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma.(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

MANJI AITISHA MKUTANO MKUU WA DHARULA WA WANACHAMA WA YANGA KUJADILI KUHUSU DILI LA AZAM TV


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
1.   Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania Premier League (TPL) na Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha mechi za Ligi Kuu (Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016
2.   Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha kuwamkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani na Azam Media.
Kwa kuwa wawazi, Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na kueleza kuwa YANGAhaina tatizo na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu mechi zao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom Premier League katika Azam Television.
3.   Sote tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya ziada” inatumika kupotosha msimamo wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na kuidhalilisha Klabu ya YANGA hadharani.
Juu ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu zinazojionyesha wazi.
Inadhihirika wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama kuilazimisha YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.
Kwa kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.
Kwa kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti, 2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha mechi za YANGA.
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI WA YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WABUNGE WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na baadhi ya wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2013. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki,  Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2013. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki,  Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla
 

TIGO YAKABIDHI BAJAJI KWA WASHINDI SABA


 Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (kulia) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mshindi wa droo ya tatu wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Khalid Shabani katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Washindi wa  droo ya tatu ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ wakipozi mbele ya Bajaji zao walizokabidhiwa na kampuni ya simu ya Tigo katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam
 Mshindi wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ Bw. Sande Juma (kushoto) akipokea ufunguo wake wa Bajaji kwa furaha kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Washindi wa droo ya tatu wa promosheni ya Tigo ‘Miliki Biashara Yako’ (kutoka kushoto) Bw. Sande Juma, Tito Mkude  na Iddi Zonki wakikagua Bajaji walizokabidhiwa kutoka kwa kampuni hiyo ya simu katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
 Washindi wa promosheni ya Tigo 'Miliki Biashara Yako' wakijaribu kwa furaha moja ya Bajaji zilizokabidhiwa na kampuni ya simu ya Tigo katika hafla iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa wa Tigo, Bw. William Mpinga akihojiwa na Waandishi wa Habari katika hafla ya makabidhiano ya washindi wa promosheni 'Miliki Biashara Yako' iliyofanyika Soko la Nyuki, Tegeta jijini Dar es Salaam

KAGASHEKI CUP 2013: TIMU YA BILELE WAFANYA KWELI WAIFUNGA TIMU YA HAMUGEMBE BAO 2-1, MCHEZAJI KHALFAN RASHID NDIYE MUUAJI!!

Kikosi Cha timu ya Hamugembe kilichoanza pamoja na Kocha wao (kushoto)

Dakika ya kwanza(1) Mchezaji Jingo Suleiman anaipatia bao timu ya Bilele baada ya kuachia shuti kali lililomuacha kipa wa Hamugembe na hapa ni wachezaji wa Bilele wakimpongeza.
Wachezaji wa Bilele wakishangilia na mashabiki wao baada ya kufunga bao dakika ya kwanza.
 ***********************
Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya Bilele FC wenye maskani yao Bukoba Mjini ( Uswahili) leo imejikatia tiketi ya kucheza Nusu Fainali na kusonga mbele kwa kuifunga timu Hamugembe bao 2-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Timu ya Bilele ndio walianza kuandika bao lao dakika ya 1 bao lililofungwa na mchezaji mshambuliaji Jingo Suleiman na kuwafanya Hamugembe wasiamini macho yao kwa goli hilo la haraka. Timu ya Hamugembe pia ilikosa mkwaju wa penati uliodakwa na kipa Erick Nkwenkwe, penati iliyoleta utata kwa baadhi ya wachezaji wa Bilele na Mashabiki wao.

Dakika ya mwishoni mwa kipindi cha kwanza dakika ya 45 timu ya Hamugembe nao wakafanikiwa kusawazisha bao baada ya beki wa Bilele kujichanganya na kugawa pasi isiyo na macho kwa kipa wake na hatimaye mchezaji wa Hamugembe kutumia nafasi hiyo kusawazisha na kufanya 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kila timu ikiwa makini ili kutafuta bao la ushindi na hatimaye timu ya Bilele kufanya mashambulizi ya uhakika katika dakika za majeruhi dakika ya 90 mchezaji Khalfan Rashid Kitenge wa Bilele akachomoka na kuwaacha mabeki na kutupia nyavuni, Kwa ushindi huu Bilele wanajikatia tiketi ya kucheza Nusu fainali na timu iliyoshinda jana Makhirikhiri (Kitendaguro) kwenye Nusu Fainali wiki ijayo siku ya Jumanne tarehe 13.08.2013.

Wadau wakifuatoia mtanange Kidogo Bilele wafungwe bao hapa..Mchezaji wa Bilele akiendesha huku mchezaji wa Hamugembe akimkinga hapa hupiti!!
Kipa wa Bilele akiondoa mkwaju wa penati hapa.....Patashika uwanjani hapa wachezaji wa Bilele wakiwenka ngumu kwa wachezaji wa HamugembeMchezaji wa Bilele akiondosha mpira kwa kichwa hapa
Mashabiki
You might also like:

MZIBUA MITARO MAARUFU WA MAJI MACHAFU NA KAWAIDA MAREHEMU TUMAIN AKUTWA KAFARIKI LEO, MTARONI KASHAI MAENEO YA PEPSI

 Ni mwili wa marehemu Tumaini mzibua mitaro ya maji machafu kashai amekutwa kafariki katika mtaro wa kashai maeneo ya kiwanda cha pepsi zamani,chanzo cha kifo chake hakijafahamika
                                              umati wa watu waliokuja kushuhudia tukio la kusikitisha
                                    mwili wa marehemu kabla ya kutolewa kwenye mtaro
                                                  mwili wa marehemu ukitolewa mtaroni
                                                        mwili ukitolewa kwenye maji
                                        mwili ukipakiwa kupelekwa hospital kwa uchunguzi
eneo yalipomkuta mauti marehemu Tumain mzibua mitaro maarufu kashai,PICHA KWA HISANI YA DJ ANAS

Hatua iliyofikiwa katika kuanzisha moja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki




Mchumi Mwandamizi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Emmanuel Mbwambo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu hatua iliyofikiwa na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika majadiliano ya kuanzisha umoja wa fedha wakati wa mkutano na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. zamaradi Kawawa. (Picha: Frank Mvungi)

TAARIFA YA HATUA ILIYOFIKIWA NA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI KATIKA MAJADILIANO YA KUANZISHA UMOJA WA FEDHA


1.0       UTANGULIZI

Ibara ya 5(2) ya Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki inabainisha kuwa Umoja wa Fedha ni hatua ya tatu ya Mtangamano wa Afrika Mashariki. Madhumuni ya Umoja wa Fedha ni kujenga ukanda tulivu wa kifedha (monetary and financial stability zone) utakaoharakisha kusaidia ukuaji wa biashara na shughuli za kiuchumi ndani ya Jumuiya. Katika kufikia malengo haya ya Umoja wa Fedha Nchi Wanachama, ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki, hukubaliana yafuatayo:-

i. Kuongeza kiwango na kasi ya mtangamano wa masoko ya fedha na mitaji (deepen financial market integration);
ii. Kuhuisha sera za kibajeti za nchi Wanachama (harmonisation of national fiscal policies);
iii. Kuwa na utaratibu wa kuendesha shughuli za uchumi bila kukinzana na malengo ya Umoja wa Fedha;
iv. Kuunda Benki Kuu moja ya Jumuiya (EACB) itakayosimamia Sera moja ya fedha(single monetary policy) na sera moja ya viwango vya ubadilishanaji fedha (exchange rate policy); na
v. Kuanzisha sarafu moja ya Jumuiya;

2.0    HATUA ILIYOFIKIWA

Mchakato wa uundaji Umoja wa Fedha wa Afrika Mashariki ulianzishwa na Kikao cha 15 cha Baraza la 

t
 
 
Picture
Mwanasheria Mshauri wa Baraza la Ushindani (FCT) Bi. Hafsa Said(kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari sheria mbalimbali na kesi ambazo zimeshawahi kuendeshwa na baraza hilo, kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari, kulia ni Mchumi Mshauri wa Baraza hilo Bw. Nzinyangwa Mchany.
BARAZA LA USHINDANI (FAIR COMPETITION TRIBUNAL – FCT)

MADA KUHUSU BARAZA LA USHINDANI ILIYOWASILISHWA KWA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 6 AGOSTI 2013, KATIKA UKUMBI WA HABARI MAELEZO, DAR ES SALAAM

Utangulizi

Ndugu Waandishi wa Habari, mada yetu inahusu Baraza la Ushindani. Katika mada hii tunatarajia kuliezea Baraza la Ushindani kuwa ni chombo cha namna gani, majukumu yake na uwezo wake kisheria. Hivyo, ili kuweza kuwapa maelezo yatakayoweza kuwasidia kuandika makala zenu vizuri mada hii imejengwa katika sehemu tatu kuu kama ifuatavyo:
  1. Chimbuko la Baraza la Ushindani;
  2.  Baraza la Ushindani ni nini
  3. Majukumu na Uwezo wa Baraza.

Chimbuko la Baraza la Ushindani

Bila shaka mtakumbuka kwamba katika jitihada za kuboresha na kuimarisha uchumi mwaka 1986, Serikali ya Tanzania iliamua kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa uchumi kutoka kwenye mfumo wa uchumi hodhi (planned economy) na kufuata mfumo wa uchumi wa soko (Market Economy). Kwa kifupi katika Mfumo wa uendeshaji wa uchumi hodhi maamuzi yote makubwa yanayohusisha uendeshaji wa uchumi hufanywa na Serikali, wakati katika mfumo wa uchumi wa soko, maamuzi yote makubwa hufanywa kwa kutegemea mwelekeo na nguvu ya soko.   Aidha, mfumo wa uchumi wa soko unashirikisha kwa kiasi kikubwa sekta binafsi. Katika mfumo huu huduma na bidhaa sokoni hutolewa na kuuzwa kwa ushindani. Uzoefu duniani umeonesha kuwa bila kuwa na usimamizi mzuri wa ushindani sokoni migongano na mivutano ya kimasilahi 


ERICK KIMASHA ANASEMA TUMEONA YA FUTARI, TUSUBIRI YA KWARESMA

Tumeona ya Futari, Tusisubiri ya Kwaresma!

Ukistaajabu ya Musa, utayaona ya Firauni! Nilidhani kuwaona wanasiasa wanageuka waongoza Ibada ndiyo ingekuwa mwisho wa kustaajabu kwangu maishani. La hasha kumbe ndo bado kabisa vituko ndo viko arif!

Toka nizaliwe sijapa kuona tukio la kiibada lililogeuka kuwa msimu wa maonyesho ya kidunia kama Ramadhani ya mwaka huu. Sote tumemuona Rais wetu mkarimu wakiwafuturisha watu wake wa nguvu hususani wasanii, tumeona mabenki, makampuni ya simu na makampuni mengine yakifuturisha wateja wao, tumesikia Manispaa zikifuturisha, tumeona wabunge wengi tu wakitoa vitu vya kufuturisha katika majimbo yao, tusimsahau Mama Salma naye hakubaki nyuma. Wote hawa hawafuturu na walengwa ikabaki kuwa ibada yao ya sirini bali huakikisha pia uwepo wa vyombo vya habari kama sehemu kuu ya ibada yao. Na leo tunasoma habari za Edward Lowassa kufuturu Tanga. Nimevutiwa na Mtiririko huu wa jinsi matukio ya Kiibada yalivyogeuka majukwaa ya kisiasa na taratibu Wanasiasa wanavyozidi kujichukulia kiti kwenye mimbari na altare huku Wachungaji, Mashehe na Mapadri wakigeuka kuwa waumini na walei wakati waumini na walei wao wakichukua jukumu jipya ndani ya makanisa na msikiti kama washangiliaji. Nani ataliokoa kanisa la Mungu na wanyanganyi? Mtume gani atarudi kuzikomboa Masjid za mwenyezi Mungu?

Naamini katika matendo ya sadaka za kiibada lakini siamini katika show-off za namna ya ufuturishaji unavyofanywa. Naamini sadaka ya kweli ni ile mtu anayotoa moyoni si kwa ajili ya kuufamisha umma anafanya nini bali kwa ajili ya kumfurahisha muumba wake. Sote tumeona jinsi ufuturishaji ulivyogeuka kuwa sehemu ya CSR ya Makampuni na majukwaa ya kisiasa. Mwanzo miaka ya nyuma tulizoea makampuni ya simu ndiyo yalikuwa yanatumia ufuturishaji lakini sasa tumeona na wanasiasa wamevamia kwa kasi ya ajabu mlango huu. Kama mwenendo huu unahusiana na harakati za mwaka 2015, basi natabiri mwakani kuna wanasiasa na vyama vya siasa vitafuturisha mwezi mzima! Tutainajisi futari na itageuka chanzo cha kututenganisha. Wapo wataoanza kusema “mie nafuturu msikiti wa chama Fulani” na wengine watakuwa wanashiriki “futari ya mgombea fulani”

Tumebomoa misingi ya nchi, kila uchao tunavunja miiko ya vyama, tunahimiza na kutekeleza itikadi za kibaguzi, na baada ya kuharibu huko kote sasa tumevamia kuivunja misingi ya ibada za Mwenyezi Mungu?! Tutafakari upya tujirudi mapema. Tuwaambie hapana wanasiasa uchwara wanaotusababishia maisha magumu na njaa ili watuhadae kwa futari la msimu. Tutumie hekima na busara kuwakosoa viongozi wetu wa dini kwa kukumbatia ukengeufu wa namna hii kujongea patakatifu. Tusipofanya hivyo sasa, natarajia msimu ujao itakuwa zamu ya matukio haya haya kudurufiwa katika Kwaresma. Na ndipo katika madhehebu yote, tukio hili la ibada ya toba litakapokuwa limegeuka rasmi kuwa mateka na jukwaa la wanasiasa. Tumeona ya Futari, Tusisubiri ya Kwaresma kuchukua hatua!

Ni mtazamo wa Erick Kimasha, msomaji na mchangiaji wa hii Blog.