Tuesday, 6 August 2013

TAMASHA LA IDD MOSI DAR LIVE: WASANII, MABONDIA WALONGA NA WANAHABARI

Tuesday, August 6, 2013

Meneja wa Matukio wa Dar Live, Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu burudani mbalimbali zitakazokuwepo Dar Live sikukuu ya Idd Mosi.
Mwanamuziki H - Baba akitamba mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kuwa atafunika mbovu siku hiyo.
Mratibu wa mapambano ya ndondi, Abdallah Yasin 'Ustaadh' (kulia) akiongea na wanahabari. Kushoto ni Abdallah Mrisho.
Mwanamuziki Ali Kiba (kulia) akipeana 'hi' na Ustaadh wakati wa mkutano huo.
Bondia Francis Miyeyusho akitunisha misuli. Bondia huyu atapigana na Mzambia Darius Lupupa.
 
Bondia Chupaki Chipindi atakayezipiga na Ramadhan Kido.
 
 Ramadhan Kido atakayepambana na Chupaki Chipindi siku hiyo.
 
Mabondia wa kike Ester Kimbe (kushoto) na Irene Kimaro wakijaribu kuzipiga.
Mabondia Francis Miyeyusho (kulia) na Ramadhan Kido (kushoto) wakifuatilia mkutano huo.
Chupaki Chipindi kutoka mkoani Iringa akiwa kwenye pozi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
 
Bondia Ester katika pozi.
 
Bondia Irene naye akiwa kwenye picha ya pozi.
 
H - Baba katika pozi la kusimama.
 
Ester ndani ya gloves.
WASANII wa muziki watakaopanda katika jukwaa la kisasa la Dar Live sikukuu ya Idd Mosi pamoja na mabondia leo wamelonga na wanahabari kwenye mkutano uliowakutanisha ambao umefanyika katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza Afrikasana jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo wasanii wametambiana kila mmoja akitamba kuwa atamfunika mwenzake. Vilevile mabondia nao wametunishiana misuli hali inayoonyesha kuwa kutakuwa na bonge la burudani katika sikukuu hiyo ya Idd Mosi.
Katika sikukuu hiyo wasanii Ali Kiba, H-Baba, Chegge, Temba, Dogo Aslay, Bi. Cheka na Bendi ya Mapacha Watatu watashusha bonge la burudani na kuwapa raha mashabiki watakaohudhuria shoo hiyo. Kwa Upande wa masumbwi bondia Francis Miyeyusho atazipiga na Darius Lupupa kutoka nchini Zambia, Chupaki Chipindi atapigana na Ramadhan Kido. Vilevile mabondia wa kike Ester Kimbe na Irene Kimaro wataonyeshana moto siku hiyo.

KAGASHEKI CUP 2013: ROBO FAINALI, LIVE MATCH- KITENDAGURO 2 VS MIEMBENI 0

Waamuzi wa mtanange huu kati ya Kitendaguro na Miembeni ambao ndiyo umefungua raundi hii ya pili ya Robo fainali Kagasheki Cup 2013.
Wachezaji wakisalimiana kabla ya mtanange kuanza
Wachezaji wakisalimiana na waamuzi hapa kulia ni wachezaji wa Kitendaguro a.k.a Makhirikhiri

Kikosi kilichoanza cha Miembeni

Kikosi Cha Makhirikhiri( Kitendaguro)

Monday, 5 August 2013

ADITHI YA PUNDA NA MKULIMA!


Siku moja punda wa mkulima alianguka ndani ya kisima. Mnyama huyo alipiga kelele kinyonge kwa masaa kadhaa wakati mkulima akijaribu kufikiri nini cha kufanya.
Hatimaye, aliamua kwakuwa punda wake alikuwa mzee, na pia kisima hicho kilihitaji kufunikwa juu, Akaona hapakuwa na haja ya kumtoa
 Akaita majirani zake wote waje kumsaidia. Wao wote wakachukua makoleo na kuanza kuchota taka kwa koleo na kuzitupia ndani ya kisima.
 Mara ya kwanza, punda aligundua nini kilikuwa kinatokea akapiga kelele kwa nguvu. Basi, ikawashanganza wale watu punda aliponyamaza ghafla!
Baada ya kutupa taka kadhaa kwenye hicho kisima. Huyo mkulima alishangazwa na kile alichokiona. Kwamba kila koleo la taka lililorushwa juu ya mgongo wa punda, punda alikuwa akifanya kitu cha kushangaza. Alikuwa akijitikisa ili taka zimwagike chini huku akipiga hatua moja kuja juu.

Kadri mkulima na majirani walivyoendelea kutupa uchafu kwa koleo juu ya punda yule, alizidi kutikisa mgongo wake na kupiga hatua moja kuja juu. Muda mfupi baadae, kila mtu alishangaa jinsi punda alivyozidi kutokeza ndani ya kisima na kuja juu.

FUNZO:
Maisha yatakutupia kila aina ya uchafu. Ili utoke nje ya kisima wahitaji kujitikisa na kuchukua hatua moja juu. Kila tatizo ulilonalo, ni jiwe la kukuwezesha kukanyaga na kupiga hatua kuja juu. Tunaweza kutoka nje ya kisima kirefu kwa kuongeza bidii ya kupiga hatua moja kuja juu bila kuacha na kutokata tamaa kamwe. Tikisa itikisa uchafu mbali na kuchukua hatua kuja juu.
Kumbuka kanuni 5 rahisi ili uwe na furaha:
1. Weka huru moyo wako mbali na chuki - Samehe.

2. Weka huru akili yako mbali na wasiwasi - Wengi hushindwa kabisa kipengele hiki.

3.Tosheka / rizika na ulichonacho.

4. Toa zaidi.

5. Tarajia vichache kutoka kwa watu lakini zaidi kutoka kwako mwenyewe.
Asante Avit Kapinga kwa kututumia ujumbe huu.

RAIS KIKWETE NA MARAIS WASTAAFU MZEE MWINYI NA MZEE MKAPA WAALIKWA FUTARI KWA KATIBU MKUU KIONGOZI

Monday, August 5, 2013

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya nne Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakati wa futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa pili kushoto) nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
 Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefua akimshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya nne Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwa kuhudhuruia  futari aliyoaiandaa nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
 Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Alhad akiongoza dua kwa waalikwa waliohudhuyruia  futari aliyoaiandaa nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya nne Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya  futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya nne Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya  futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjmani William Mkapa na Rais wa Awamu ya nne Alhaj Ali Hassan Mwinyi baada ya  futari iliyoandaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es salaam Jumapili

Sunday, 4 August 2013

WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA SHULE YA SEKONDARI ST.SOSTHENES YA IZIMBYA KABALE BUKOBA VIJIJINI WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO WATEMBELEA EQUATOR NCHINI UGANDA

 Wanafunzi  wa shule ya sekondari St. Sosthenes wakiwa katika picha ya pamoja Equator,mwalimu mkuu wa shule hiyo ndugu Mujungu Johnston amesema wamekuwa wakiwafundisha watoto darasani, lakini wanapenda ili watoto waelewe vizuri wanawapeleka watoto kwenye maeneo husika ili waweze kuelewa zaidi kile wanachojifunza darasani, aliendelea kusema wataendelea kufanya hivyo kila wakati japo ni gharama ila wanajari wanafunzi kujifunza na kuelewa
                                                                             wanafunzi wakiwa maeneo ya equator 
                                         mwalimu mkuu aliekaa akiwa na walimu wenzake
                                          walimu wakifurahia study tour yao na wanafunzi
                                                                 walimu wa kike wakifurahia
                                          wanafunzi wakiwa wanafurahia ziara yao ya mafunzo
                               mwalimu mkuu akieleza nia  na madhumuni ya ziara ya mafunzo
          watu mbalimbali hupenda kupiga picha wanapofika eneo hilo linaroigawa dunia katikati
 wanafunzi wa kidato cha kwanza wa St. SOSTHENES,shule inayomilikiwa na kanisa la Authodox Tanzania, shule hii ipo Izimya kabale bukoba vijijini
     mwalimu mkuu akiwaeleza wanafunzi historia kwa ufupi kuhusu watawala wa nchi ya uganda
                                               wanafunzi wakimsikiliza mwalimu mkuu
                                                                              walimu
                                                            walimu na wanafunzi
jamcobukoba.blogspot.com tutawaletea matukio popote pale tupigie simu 0754-757157

Friday, 2 August 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA KIONGOZI WA TAASISI YA IYF YA KOREA KUSINI NA UJUMBE WAKE

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Mchungaji Ock Soo Park pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na ujumbe wa IYF Ikulu jijini Dar es salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadili chapisho la kitabu na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Mchungaji Ock Soo Park aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo. Kushoto ni mkaliman
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Kiongozi wa taasisi ya International Youth Foundation (IYF) ya Korea Kusini Ock Soo Park Ikulu jijini Dar es salaam

BAADA YA ROSE NDAUKA KUHUSISHWA KATIKA FUMANIZI...!! HAYA NDIYO MANENO YA MCHUMBA WAKE ROSE KUHUSU SAKATA HILO

Friday, August 2, 2013



BAADA ya msanii wa filamu nchini Rose Ndauka kuripotiwa kufumaniwa akiingia gesti na msanii chipukizi wa muziki wa bongo fleva Nassoro Ayoub 'Dogo Nasry' huku akiwa amevaa baibui kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, mumewake mtaarajiwa Maliki Bandawe 'Chiwaman' amjia juu msanii huyo kwa madai ya kumchafua mpenzi wake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Chiwaman aliweka wazi kuwa msanii huyo Nasry ambaye alimuomba Rose aweze kushiriki kwenye video yake, walishindwa kufikia maamuzi kutokana na kiwango cha malipo kuwa madogo, na badala yake msanii huyo alimuomba wapige picha kama ukumbusho.

Alisema kuwa kitendo hicho cha kupiga picha na msanii huyo wakati wapo katika mazungumzo ya awali ya kukubaliana malipo ndizo picha alizotumia msanii huyo na kudai kuwa alikuwa naye nyumba ya wageni kitendo ambacho si cha kweli.

"Hawa wasanii wachanga wanatafuta umaarufu vibaya kwa kuwachafua watu, ilikuwa amemuomba Rose ashiriki kwenye video yake na ndipo walipokutana kwa ajili ya mazungumzo hayo na alikuwa na mdogo wangu sasa hapo masuala ya gesti yametokea wapi" alisema Maliki.

Aliongezea kuwa "kama nilikuwa sijui hicho kitu na kwa jinsi mambo yalivyokuwa ningeweza kumuacha mchumba wangu ninayempenda kwa dhati, ila msanii huyo alichokifanya siyo jambo sahihi, kwani alimuomba apige naye picha na Rose alikubali huku bila kujua nia yake ".

Maliki alisema kuwa huyo msanii anatafuta umaarufu kwa kuchafua majina ya watu wengine, kitu ambacho hakina mashiko kwenye jamii.