Tuesday, 11 June 2013

ASKOFU MKUU WA AUTHODOX JIMBO KUU TAKATIFU LA MWANZA JERONYMOS MUZEEYI AWAASA WANAFUNZI WA KITUO CHA MUJUNGU ACADEMIC CENTRE KUSOMA KWA BIDII



 Askofu mkuu Jeronymos Muzeeyi jimbo kuu takatifu la mwanza amewaasa wanafunzi  wa kituo cha mujungu academic centre kilichoko kata ya kagondo kusoma kwa bidii,ili elimu watakayoipata hapo iweze kuwasaidia katika maisha yao,wanafunzi zaidi ya tisini kutoka katika shule mbalimbali za sekondari ambazo zimefunga wapo hapo shuleni wakiendelea na masoma katika kipindi chote cha likizo,kituo hiki kinafundisha masoma ya sayansi,arts na kilimo


           wanafunzi wa kituo cha mujungu academic centre wakimsikiliza  askofu mkuu



baadhi ya madarasa ya kituo



                                                   askofu akiendesha ibada rasmi ya kuzindua kituo






                                                                 wanafunzi wakiimba wimbo


                                   askofu mkuu alitoa zawadi ya vitabu ili wanafunzi wajifunze




askofu pia alitoa zawadi ya madaftari na kalamu kwa wanafunzi wote,na kulia ni mkuu wa kituo johnstone richard mujungu






                                             kituo hiki wapo wanafunzi wa bweni na wanafunzi wa kutwa
                                     wanafunzi wakipokea zawadi ya dafrari na kalamu kutoka kwa askofu






                                                               someni vitabu...



                                            baba askofu tunaomba utuzindulie

                             baba askofu akizindua rasmi majengo ya kituo cha mujungu academic centre











 mmiliki wa libeneke la jamcobukoba.blogspot.com akiwa katika picha ya pomoja na askofu na mkuu wa kituo akifurahi sana








                                             ni tank kubwa la maji linalojengwa kituoni hapo



Hatimaye Wilfred Rwakatare Aachiwa kwa Dhamana, Mwenzake Aendelea Kusota....

Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Rwakatare
HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam, imemwachilia kwa dhamana Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Rwakatare mara baada ya kutimiza masharti ya dhamana iliyofunguliwa leo.
Miongoni mwa masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama na Rwakatare kuyatimiza yote na wadhamini wake ni pamoja na kuwa na wadhamini wawili ambao wamesaini bondi ya sh milioni 10 na yeye mwenyewe kujidhamini.
Masharti mengine ya dhamana hiyo ambayo ametimiza ni pamoja na Rwakatare kukabidhi mahakamani hati ya kusafiria na kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila taarifa. Hata hivyo mshtakiwa mwenzake Ludovick Rweikiza ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo na kurejeshwa maabusu.
Rwakatare na mstakiwa mwenzake, Rweikiza wanashtakiwa kwa makosa kadhaa yakiwemo ya kupanga njama za kumteka Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, kwa nia ya kumdhuru hali kadhalika kupanga mikakati ya kutenda vitendo vya kigaidi.
Taarifa ya awali chini kabla ya kuachiliwa
Dhamana ya Wilfred Rwakatare Wazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam, imefungua dhamana ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Rwakatare pamoja na mstakiwa mwenzake, Ludovick Josepha Rweikiza.
Miongoni mwa masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama ni pamoja na washtakiwa wote kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya sh milioni 10 kila mmoja na washtakiwa wenyewe kujidhamini. Masharti mengine ya dhamana hiyo ni pamoja na washtakiwa kukabidhi mahakamani hati za kusafiria na kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila taarifa.
Kwa uamuzi huo wa mahakama uliotolewa mapema leo, sasa dhamana ipo wazi na kinachosubiriwa ni washtakiwa kutimiza masharti ya dhamana kabla ya kuachiliwa. Rwakatare na mstakiwa mwenzake, Rweikiza wanashtakiwa kwa makosa kadhaa yakiwemo ya kupanga njama za kumteka Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, kwa nia ya kumdhuru hali kadhalika kupanga mikakati ya kutenda vitendo vya kigaidi.

REDD'S MISS KAGERA 2013 NI 15-06-2013 JUMAMOSI LINA'S NIGHT CLUB




 NI MSANII MICHAEL ROSS KUTOKA NCHINI UGANDA ATATOA BURUDANI
            TIKETI ZINAPATIKANA KASIBANTE REDIO,KATA TIKETI YAKO MAPEMA

Monday, 10 June 2013

HALI YA AFYA YA MANDELA SIO NZURI.


Rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, angali katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa. Mandela amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.

"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''

Maombi yakekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.

Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.


Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.

Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.

Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.


 Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona.


Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.


Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.


Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999.


Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela.

Habari na bbc swahili
Dunia nzima inaungana kumuombea Mandela apone hata leo kumekuwepo na misa maalum ya kumuombea apone huko Afrika ya kusini.
Hatuta penda kumkosea Mungu hata akimuita tunaamini muda wake utakuwa umefika.Mandela atakumbukwa kwa Ushujaa wake na bara hili la Afrika na dunia kwa ujumla.
Viva Mandela!!

RAISI KIKWETE AMPA MKONO WA POLE KHADIJA OMARY KOPA MJINI BAGAMOYO. Rais Dk. Jakaya Kikwete akimfariji Msanii wa taarabu Hadija Kopa nyumbani kwake mjini Bagamoyo jana kufuatia kifo cha Mumewe Marehemu Jaffari Ali Yusuf aliyefariki na kuzikwa majuzi. Rais Dk. Jakaya Kikwete akiwafariji wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wa msanii maarufu wa taarabu na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa CCM, Hadija Kopa kufuatia kifo cha mumewe Jaffari Ali Yusuf kilichotokea wiki iliyopita na kuzikwa jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi na (kulia) ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa CCM, Ridhwani Kikwete. Picha na Freddy Maro - IKULU

RAISI KIKWETE AMPA MKONO WA POLE KHADIJA OMARY KOPA MJINI BAGAMOYO.


Rais Dk. Jakaya Kikwete akimfariji Msanii wa taarabu Hadija Kopa nyumbani kwake mjini Bagamoyo jana kufuatia kifo cha Mumewe Marehemu Jaffari Ali Yusuf aliyefariki na kuzikwa majuzi.
Rais Dk. Jakaya Kikwete akiwafariji wanafamilia, ndugu jamaa na marafiki wa msanii maarufu wa taarabu na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa CCM,  Hadija Kopa kufuatia kifo cha mumewe Jaffari Ali Yusuf kilichotokea wiki iliyopita na kuzikwa jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo  Ahmed Kipozi na (kulia) ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa CCM, Ridhwani Kikwete. Picha na Freddy Maro - IKULU

Sunday, 9 June 2013

KWA HALI ISIYO YA KAWAIDA MWANAMKE AJIKUTA SEHEMU ZAKE ZA SIRI HAZIPO BAADA YA KUMUIBIA MWANAUME ALIEKUWA NAE GESTI

 Mama huyu akiwa hajielewi kwa kile kilichompata,baada ya kula uroda na mwanaume katika nyumba ya wageni ya super star hamugembe alitoweka na pesa za mwanaume huyo ambae inasemekana ni mkazi wa kigoma,baada ya muda mama huyu alijikuta hana sehemu zake za siri

 mama alipoteza sehemu zake za siri kwa mujibu wa maelezo yake anamtafuta mwanaume ambae inasemekana ni mkazi wa kigoma amrudishie sehemu zake za siri
 umati mkubwa wa watu walifurika maeneo ya stand kuu bukoba kushuhudia tukio la aina yake

                                                duniani kuna majanga na hili janga

                                               masikini mama wa watu hana tena sehemu zake nyeti

 umati mkubwa uliokuja kumshuhudia mama aliepoteza sehemu zake za siri,baada ya kumuibia mwanaume
                                      umati ulikuja kumuona mama alipoteza sehemu zake za siri

 baada ya umati kuwa mkubwa police walifika maeneo ya tukio na kumchukua huyo mama,tunafanya jitihada za kumpata msemaji wa jeshi la police,na ikibidi taarifa rasmi ya daktari
                                                             ni stand kuu bukoba leo
                                                                msomaji kuna mengi ya kujifunza hapa

                                    panda mama tukifika huko tutajua zipo au zimetoweka...
                                                            majanga jamani ......       
                                          mama alipoteza sehemu za siri akipelekwa polisi

MAMBO MENGI KATIKA UTAMADUNI WA MUHAYA HAYAFANYIKA KAMA ZAMANI KUTOKANA NA HALI YA MAISHA KUBADIRIKA


Enzi za mababu zetu,nyumba nyingi maeneo ya vijijini bukoba ilikuwa ni jambo la kawaida kukuta (OBWATO) mtumbwi wa kutengeneza pombe ya kienyeji orubisi kwa maana kila wiki ilikuwa ni kawaida kwenda kwa wazee tofautitofauti na kukuta wametengeneza pombe hiyo ya kienyeji, rubis inatengenezwa kwa ndizi mbivu,zinachangaywa na mtama. Miaka ya sabini wahaya chakula chao kikuu ilikuwa ni ndizi, ugari mtu alikula kwa kupenda na kwa nadra sana,na mtu alipokula ugari wengi walimshangaa na kumuona mtu mwenye dhiki hivi..,yote hiyo ilisababishwa na neema ya mashamba mazuri yenye rutuba na ndizi nyingi,zilikuwepo ndizi aina ya embile ndizo zilitumika kwa ajili ya kutengeneza pombe,aina ya ndizi hiyo ilikuwa ni marufuku kwa matumizi ya chakula, lakini mambo hubadilika leo migomba maeneo mengi hamna tena,mingi imeshambuliwa na magonjwa na wengine wametoa kabisa migomba na kuendelea na kilimo cha kutegemea msimu kama mahindi nk,hali hiyo imesababisha mambo mengi ya asili ya muhaya kupotea kutokana na hali ya maisha na kiuchumi kubadilika,vitu kama obwato ni nadra sana kukuta watu bado wanatengeneza pombe za kienyeji,maana hata hizi ndizi za pombe watu wanakula na hazipatikani tena,wenye migomba mizuri na wachache sana anbao wanauwezo wa kugharamia mashamba.

Anaonekana mtu akichota pombe kuweka kwenye dumu

Maeneo mengi bukoba miaka ya sabini walitumia kuni kupikia chakula,kizazi hiki hata vijijini wanatumia majko ya mkaa,gesi na umeme kupikia

Na nyama ya bukoba ni tofauti na maeneo mengine ,maana ng'ombe muda wote wanakula majani fresh

Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa maeneo mengi wanapanda migomba ya kisasa kwendana na hali halisi ya udongo

Aina ya ndizi hii hujulikana zaidi kwa jina la mutwishe

Wenye uwezo kifedha na mbolea ndio wanaweza kuandaa mashamba ya migomba

Wa mama wamekaa kwenye nyasi wakizungumza,
Watu hukaa kwenye nyasi na kuendelea na mazungumzo kama kawaida

Endelea kuangalia jamcobukoba.blogspot