BENDI ya muziki wa dansi ya Malaika yenye masikani yake jijini Dar es salaam, Ilipagawisha wakazi wa Mkoa wa Kagera Vilivyo kwenye ziara yao katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Ziara hii baada ya kumaliza hapa Mjini Bukoba wanaelekea Jijini Mwanza, Jiji la Miamba ya Mawe (Rock City) ambapo bendi ya Malaika itatoa burudani ya uhakika ndani ya Villa Park Resort ambapo Bela ambaye hujiita Rais wa Vijana atafanya makubwa tarehe 31, Mei 2014 siku ya Jumamosi kiingilio kikiwa ni Tsh:10,000/ = tu.
Wakazi wa Mwanza zamu yenu sasa hiyo! Hakuna kukosaaa!!
Waimbaji wa Band ya Malaika wakikamua vilivyo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Lina's Club uliopo Bukoba Mjini.
Dadaz wakifuatilia kwa karibu sana Burudani kutoka kwa Malaika Band kutoka jijini Dar es salaam
Marafiki: Bw. Mutensa na rafiki yake Ticha wa Leo leo wakipeana neno
....peupe na wazi wazi ....chezea Malaika Band wewe!! Dada Maua akiwa kwenye kasi mbaya!! 120!
Kazi ipo kweli kweli!!!
No comments:
Post a Comment