Thursday, 23 June 2016

HARAMBEE YA OKOA MAISHA YA WAANDISHI WA HABARI KUFANYIKA JUMAMOSI JUNI 25 MKOANI DODOMA


Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari,Peter Nyanje akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar kuhusiana na maandalizi ya harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. Pichani shoto ni Mratibu wa Kampeni hiyo Grace Nackson na kulia ni Mratibu kutok Kampuni ya Midia Assistant,Dickson Matikila pamoja na Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulika kwa jina la kisanii Inspekta Haroun.PICHA NA MICHUZI JR.
Mratibu wa Kampeni ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, Grace Nackson akitoa ufafanuzi zaidi kuhusiana na harambee hiyo kwa waandishi wa Habari waliotaka kufahamu zaidi kuhusiana na harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016.Mratibu huyo ameeleza kuwa Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Inspekta Haroun akifafanua jambo kuhusiana na ushiriki wao kama sehemu ya wasanii watakaoshiriki siku hiyo mjini Dodoma.
Mkutano ukiendelea kuhusiana na harambe hiyo.

======  ======  ======  ======
Kamati ya Maandalizi ya Okoa Maisha ya waandishi wa habari, imeandaa harambee maalumu ya kuosha magari yaani Media Car wash for health, litakalofanyika Mjini Dodoma, Uwanja wa Jamhuri, siku nzima ya Jumamosi June 25, 2016. 

Lengo la harambee hiyo ni kukusanya fedha zitakazotumika kuwakatia Bima ya Afya waandishi wa habari takribani 1000 hapa nchini. Kamati ya Maandalizi ya harambee inajumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari chini ya Uenyekiti wa Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda, inaomba ushirikiano wakaazi wa Dodoma pamoja na Wabunge. Mtakumbuka kwamba kamati hii ilifanya tukio kama hili viwanja vya Leaders, Jijini Dar es Salaam July 4, 2015, ambapo zaidi ya 30m/-, zilichangishwa.

Fedha hizo zilisaidia gharama za matibabu ya waandishi watatu waliokuwa mahututi wakati huo, mmoja wao akiumwa kansa. Lengo la mwaka huu limebadilika ambapo tumekusudia kuhakikisha kuwa wengi wao wanakatiwa bima ya afya, ili kujikinga na kadhia ya kuchangiwa fedha pale wanapofikwa na maradhi. Aidha, kwenye changizo hili tutakuwa na kadi maamlum za kuomba michango ya mfuko huo, ambazo tutazigawa kwa Wabunge kupitia ofisi ya Bunge. Tutaomba ushirikiano mzuri kutoka kwa Wabunge na wakazi wa Mji wa Dodoma ili kufanikisha zoezi hili. 

Pia tumeandika barua kwa Spika tukimwomba awajulishe Wabunge ili wajitokeze kwa wingi kwenye zoezi hili. Waratibu wa Harambee ile ambayo ni Kampuni ya Media Assistant, imefanya utaratibu wa kumleta Miss Tanzania Ms Lilian Kamazima pamoja na wasanii wa Bongo Movies na Bongo Fleva kuja kushiriki zoezi hilo. 

Wasanii hao ni kundi la Weusi ambalo linajumuisha John Simon Makini a.k.a Joh Makini, Nickson Simon a.k.a Nikki wa Pili na George Sixtus Mdemu a.k.a G Nako, wenye asili ya Arusha na wanafanya shughuli zao za kimuziki Jijini Dar es Salaam pamoja na Haruna Kahena a.k.a Inspekta Haruni. Wasanii wa Bongo Movies ni pamoja na Aunt Ezekiel, Kajala Masanja, Ray Kigosi na Jacob Stephen a.k.a JB. Na pia kutoka Orijino Komedi tumepewa mwakilishi Isaya Mwakilasa ambaye zaidi anajulikana kwa jina la Wakuvanga na maarufu zaidi kama Mama Bele. Asanteni kwa Kunisikiliza Judicate Shoo, Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Harambee

Wednesday, 22 June 2016

MACHINGA JIJINI MWANZA WAKUTANA KUAMUA HATIMA YAO.

Mgeni Rasmi, Dkt.Kissui Steven Kissui ambae ni Mwenyekiti wa Shindano la Uwezeshaji Kiuchumi na Ajira Tanzania, akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.
Na BMG

Mkutano huo ambao uliandaliwa na Shirika la Machinga Mkoa wa Mwanza SHIUMA, ulilenga Machinga kujadiliana na wadau wengine wa Uwekezaji ikiwemo taasisi za kifedha, juu ya Kurasimisha biashara zao na kuwekwa kwenye mifumo rasmi ya Kibiashara na Kijamii.
Machinga wamesema changamoto kubwa zinazowakabiri ni Ukosefu wa Mitaji ya Biashara, Maeneo ya Kufanyia Biashara pamoja na Ukosefu wa Elimu Biashara. Wamesema wanataka nao watambulike na taasisi za kifedha ili wapate fursa ya kukopesheka ili kukuza mitaji yao.
Mgeni Rasmi, Dkt.Kissui Steven Kissui ambae ni Mwenyekiti wa Shindano la Uwezeshaji Kiuchumi na Ajira Tanzania, akifungua Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.
Katibu wa Shirika la Machinga Mkoa wa Mweanza SHIUMA, Venatus Anatory, akizungumza katika Mkutano wa Wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) Jijini Mwanza uliofanyika hii leo.
Mmoja wa Machinga akizungumza katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo
Mmoja wa Machinga akizungumza katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo
Mmoja wa Machinga akizungumza katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo
Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanja (katikati), akiwa na wadau wengine katika Mkutano wa Machinga Jijini Mwanza uliofanyika hii leo
Machinga Jijini Mwanza
Machinga Jijini Mwanza
Machinga Jijini Mwanza wakinyoosha mikono juu ikiwa ni ishara ya kukubaliana kwa pamoja na hoja yakurasimisha biashara zao, Kupata maeneo rasmi ya Kufanyia biashara katikati ya Jiji pamoja na Kutambulika katika taasisi za kifedha ili waweze kukopesheka na kupatiwa elimu ya kibiashara.

Sunday, 19 June 2016

MK BOTTLES CO.LTD WAANZA KUZALISHA SODA, KIWANDA CHA MAJI ASILIA BUKOBA.

 MK BOTTLES kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa kilichopo Manispaa ya Bukoba kata ya Kashai ,baada ya maji yake ya julikanoyo kwa jina la Asilia kukubalika kwa kasi kwa wanywaji kutokana na ubora wa hali yajuu, sasa wameanza uzalishaji wa soda zenye radha tofauti kwa watumiaji, Mtendaji mkuu wa kiwanda hicho Georgia George wakati akiongea na jamcobukoba.blogspot.com amesema anamshukuru mungu kwanza kwa mafanikio makubwa  ya kuweza kuzalisha maji ya kunywa na kukubalika kwa wanywaji mkoani kagera na mikoa mingi nchini Tanzania, amesema pamoja na  hayo sasa wameamua kuanza uzalishaji wa soda ili kuweza kukidhi maombi na mahitaji ya watumiaji.(katika picha Bi Georgia George akiwa kiwandani ).
 Kutoka maktaba picha ya soda zinazozalishwa.
 Maji Asilia.
 hapa kazi tu.
 Mitambo .

HONGERA SAULO NA LILIAN KUFUNGA NDOA.

 Katika picha ni maharusi Bw saulo na Bi Lilian wakiwa na wapambe wao katika ufukwe wa ziwa maeneop ya Bukoba club darajani Bukoba.