Monday, 15 February 2016

RAIS DK. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA MABALOZI WAPYA WATATU, MAKAMISHNA WANNE WA POLISI NA KAIMU MKURUGENZI MKUU NIDA




Rais Dk. John Magufuli amewateua, Dk. Asha-Rose Migiro, Mathias Chikawe na Dk. Ramadhani Dau kuwa Mabalozi wa Tanzania katika Nchi za Nje.

Kadhalika, Rais Dk. Magufuli akiwateua wanne kuwa Makamishna wa Polisi na mmoja akimteua kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) 

Ifuatayo ni Taarifa ya Ikulu, Kama ilivyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa, baada ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue kutangaza uteuzi huo, leo, Ikulu mjii Dar es Salaam.



WAWILI WASIMAMISHWA TBC



 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amewasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio wa TBC Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi wa shirika hilo Bi. Edna Rajab na kuagiza kufumuliwa kwa Idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha.

Thursday, 11 February 2016

MWENYEKITI WA BUKOBA VETERAN SEIF MKUDE AWAASA WANAWAKE KUPENDA MICHEZO.

Mwenyekiti wa Bukoba veteran Bw Seif Mkude amewataka wanawake kupenda michezo mbalimbali kwa ajili ya afya zao na kuburudika,Bw Mkude aliyasema hayo hivi karibuni kwewnye sherehe ya kuaga na kukaribisha mwaka mpya iliyoandaliwa na wanawake mbalimbali wapenda michezo wa Manispaa ya Bukoba, Mgeni rasmi Bw Mkude aliwaomba wanawake wajiunge na Bukoba veteran ili waweze kujifunza na kujua mengi kuhusiana na michezo, sherehe hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kiroyera beach.
Wachezaji wa timu ya mpira wa pete katika ubora wao.
Kulia ni Bi Zaitun akiwa na BI Rebecca wapenda michezo.
Mwenyekiti wa sherehe Bi Zaitun akieleza umuhimu wa kukutana katika siku  hii ya sherehe.
Kocha Nora, ni mwalimu wa muda mrefu sana katika mpira wa pete mkoa wa Kagera.
Watu wakaburudika.
Mchezaji maarufu katika mpira wa wavu.
Ikakatwa keki.
Mgeni rasmi akimlisha keki Katibu wa chaneta Mwl Revina.
Shampeen ikafunguliwa.
Cheereess
Kushoto ni mchezaji mkongwe