Friday, 25 April 2014

MWILI WA MAREHEMU DATUS BUBERWA NYAMWIHURA WAWASILI KIJIJINI KWAO MBALE BUKOBA NA KUZIKWA 26-4-2014 JUMAMOSI


 Ni vilio na majonzi makubwa  vyote kwa pamoja vilitawala katika kijiji cha Mbale Bukoba  baada ya mwili wa marehemu Datus Nyamwihura kuwasili kutokea jijini Dar es salaam
 Mzee Masabara na wanae wakiwa maeneo ya Rwamishenye Bukoba wakisubiri Gari linalokuja na mwili wa marehemu
 Mwili wa marehemu ukiwasili Bukoba mjini
 Bw Rahimu nae alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakisubiri mwili wa marehemu maeneo ya Rwamishenye
 Hapa ndio nyumbani kwao na marehemu
 Wakazi wa kijiji cha Mbale
 Poleni jamani, Dada Passy Kazimoto akiwapa pole wanafamilia
 Machunguuu
 Ndugu , jamaa na marafiki wakipokea mwili kijijini
 Ni majonzi na simanzi
 Fransics Mutungi akaongoza misa ya shukrani kwa kufikisha mwili salama
 Mzee Damwel Ruangisa akimpa pole Bw Chichi kaka wa marehemu
 Murungi Kichwabuta nae akitoa pole
 Wazee waliokuja na mwili
 Wakipata chakula cha usiku kilichoandaliwa na Mama Shamila
Bw Chichi akiwa na swaiba wake,ambae alifika muda mchache baada ya kuwasili kijijni

Thursday, 24 April 2014

KUTOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MMOJA AANGUKA KWA PRESHA MJENGONI DODOMA


 Wauguzi na Waganga wa Zahanati ya Bunge mjini Dodoma wakitoa msaada wa huduma ya kwanza na kufanya maandalizi ya kumpeleka Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ziana Mohamed Haji katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo baada ya kupata matatizo ya  mshutuko.
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambapo pia ni Ndugu na Jamaa wa Mjumbe wa Bunge hilo Ziana Mohamed Haji wakijadiliana na watendaji wa Bunge hilo jinsi ya kumsaidia baada ya kupata matatizo ya mshutuko leo mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambapo pia ni Ndugu na Jamaa wa Mjumbe wa Bunge hilo Ziana Mohamed Haji wakijadiliana na watendaji wa Bunge hilo jinsi ya kumsaidia baada ya kupata matatizo ya mshutuko leo mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano kwa ajili ya kuendelea kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba Mpya leo mjini Dodoma.
 Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano kwa ajili ya kuendelea kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba Mpya leo mjini Dodoma.
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Esther Juma (kushoto) na Catherine Saruni (kulia) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma mara baada ya mapumziko ya kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba Mpya.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Saada Mkuya Salum akichangia maoni yake leo mjini Dodoma kuhusu Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba mpya.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mizengo Pinda (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Watendaji wa Bunge na Wajumbe wenzake Nassoro Salim (kulia),Haji Omar Heri(wa tatu kulia), Mohamed Aboud Mohamed(wa pili kushoto) , Dkt. Tereza Huvisa(kushoto) na Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Yahaya Hamis Hamad(wa tatu kushoto) leo mjini Dodoma wakati wa mapumziko mafupi ya kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba mpya. Picha na Ofisi ya Bunge Maalum la Katiba

Wednesday, 23 April 2014

NEWS ALERT!!!MAKAMPUNI MBALIMBALI KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA ELIMU NCHINI

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau  wa Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya washiriki wa mkutano wa wadau wa TEHAMA kutoka nchi za Bonde la Ufa wakimsikiliza Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (hayupo pichani) akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.


Kauli hiyo imemtolewa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa wadau Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutoka nchi za ukanda wa Bonde la ufa leo jijini Dar es salaam.
“Nawasihi wajasiriamali katika mambo ya TEHAMA ndani ya nchi washirikiane na wenzao wa nje ya nchi ili waweze kujijengea uwezo wa kukuza uchumi wa nchi yetu” alisema Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa aliwasihi washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania inawakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza katika TEHAMA ili kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma ya mawasiliano katika maeneo yote nchini hadi vijijini.
Aidha, Prof. Mbarawa alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya TEHAMA ni pamoja na ukosefu wa nishati ya umeme vijijini, kumudu gharama za uendeshaji, ukosefu wa vifaa vya sekta hiyo na usalama wa taarifa mbalimbali katika mitandao.
Kwa upande wake Waziri wa Mawasiliano, Habari na Uhusiano wa Bunge kutoka Burundi, Tharcisse Nkezabahizi alisema kuwa TEHAMA ni moja ya Nyanja muhimu inayotumiwa katika nchi yake ikiwemo elimu na huduma za afya ambapo ni muhimu kwa nchi za bonde la ufa kutumia teknolojia hiyo ili kukuza uchumi wan chi husika.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Digital Network Oy nchini Finland, Cipa Ojala alisema kuwa mkutano huo umekuja wakati mwafaka ambapo nchi nyingi zinatumia fursa iliyopo ili vyombo vya habari ikiwemo televisheni kuhama kutoka analogia kwenda dijiti.
Tanzania mpaka sasa imekuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika kutekeleza hatua ya kuhama kutoka mfumo wa analogia kwenda dijiti mbapo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu takribani mikoa yote itakuwa imezima mitambo ya analojia kwenda dijiti.
Nchi zinazoshiriki katika mkutano huo ni Burundi, Rwanda, Somaliland, Zambia, Sudani Kusini ikiwemo Tanzania ambayo imekuwa mwenyeji wa mkutano huo kwa mara ya pili mfululizo pamoja na wadau wengine katika sekta hiyo. 

KIKOSI CHA TAIFA STARS WAKIWA KATIKA UZI MPYA WA MAZOEZI

  Katika hali ya kukiweka kikosi cha timu ya Taifa stars sawa,picha kwa hisani ya Pelegrinius Rutayuga Mshauri wa ufundi TFF