Wednesday, 15 January 2014

SHOGA AWEKA HISTORIA BONGO!!! NI ANTI ASU...BAADA YA KUOKOKA HIVI NDIVYO ALIVYOFANYA

KATIKA tukio linalochukuliwa kama ni la kihistoria kuwahi kutokea katika miaka ya karibuni, shoga wa Jijini Dar es Salaam, Amos Hamis, maarufu kama Anti Asu, aliyeokoka Agosti mwaka jana, ametangaza nia ya kutaka kuoa katika Kanisa la TAG, Magomeni wiki iliyopita.


Anti Asu enzi hizo akiwa shoga katika pozi....

Amosi alimvalisha pete ya uchumba, Astrida Samatha baada ya kukamilisha taratibu zote za mila na desturi za ukweni na hatimaye kupewa ruksa ya kumuoa.

Mara baada ya misa ya pili kumalizika katika kanisa hilo, Amos alimvisha pete mchumba wake huyo na kusababisha nderemo na vifijo kutoka kwa waumini wa kanisa hilo, ambao waliahidi kuchangia baadhi ya gharama wakati wa harusi yao.


Anti Asu enzi hizo baada ya kuokoka kanisani...

Akizungumzia suala hilo, Amosi ambaye ni maarufu sana jijini Dar es Salaam enzi zake akijishughulisha na mapenzi ya jinsia moja, alisema:

"Siamini na wala sikuwahi kufikiria kama nitakuja kuwa na familia yangu, namshukuru sana baba mchungaji, kwani nina imani hata hao wanaoendelea na ushoga ipo siku watarejea kwa Bwana."


Anti Asu akimvisha pete mchumba'ke hivi karibuni kanisani

Amos alisema alijikuta akitamani kuwa na mwanamke baada ya kuokoka lakini hakuwa na mawazo hayo kipindi alipokuwa shoga.


Anti Asu baada ya kufunga ndoa kanisani wakiwa katika pozi yeye na mchumba'ke
Astrida, mwanamke aliye tayari kuolewa na Amos, alisema Mungu ameagiza upendo wa dhati ukiwemo ule wa roho, hasa kwa watu kama hawa na siyo vizuri kuwatenga.

"Tumeagizwa upendo ule wa roho, mimi naona ni sawa kwa kuwa na yeye ni mtu kama mimi na anahitaji upendo wa dhati na ninaahidi kumpenda," alisema Astrida.

MCHUNGAJI ANENA
Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo, Dustan Kanamba, alisema Agosti, mwaka jana, Amos aliamua kuachana rasmi na ushoga na kuokoka, ndipo yeye na mke wake, walipoamua kumchukua na kuwa sehemu ya familia.

"Mimi na mke wangu tulishauriana na kumchukua ili awe mmoja kati ya familia yetu, japo kabla ya kuokoka alikuwa hajisikii kuwa na mwanamke lakini hali ilibadilika pale alipookoka na kujiona anahitaji kuwa na mwanamke kwani kwa kipindi cha miaka 29, Amos hakuwahi kumjua mwanamke," alisema mchungaji.

WAUMINI WAMPONGEZA
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wamempongeza Amos kwa hatua aliyofikia na kuahidi kumpa sapoti katika ndoa yake inayotarajiwa kufungwa hivi karibuni, huku wakitaja baadhi ya vitu watakavyomuwezesha kama kumshonea suti ya kufungia ndoa na vinginevyo.

Amos aliachana na mambo ya ushoga Agosti, mwaka jana baada ya kuokoka na kufanyiwa maombi na mchungaji kiongozi wa kanisa la T.A.G, Magomeni Mikumi jijini Dar.

RC KAGERA ANAFICHA NINI?

MKUU wa Mkoa (RC) wa Kagera, Kanali mstaafu Fabiani Massawe, anafanya mbinu za kutaka kupindisha ukweli kuhusu tuhuma zinazomkabili Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani.
Manispaa hiyo imekumbwa na mgogoro mkubwa kati ya madiwani na meya huyo, vikao vya madiwani havikutani kwa zaidi ya mwaka. Suluhu imeshindikana hadi kufikia hatua ya kuletwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, ili akague miradi inayolalamikiwa.
Wakati ripoti ya CAG ikisubiriwa iseme kilichobainika, mkuu wa mkoa anajaribu kutumia njia za panya kutaka kumaliza mgogoro huo kwa mbinu za kijanja.
Huku akielewa wazi kwamba madiwani wamechaguliwa na wananchi na hivyo wanawajibika kwao, Massawe anaamua kuitisha kikao alichokiita cha usuluhishi ili kuwashawishi wakubali kuketi na ‘mtuhumiwa’ kupitisha bajeti ya 2014/2015.
Massawe anajificha kwenye migongo ya viongozi wa dini, Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini, Sheikh wa Wilaya ya Bukoba, Haruna Kichwabuta na wazee maarufu ili wamsaidie kuwalainisha madiwani, lakini anagonga mwamba.
Madiwani hao wanane wa CCM wanaompinga meya pamoja na wale saba wa upinzani, wanamshangaa Massawe na viongozi wake wa usuluhishi kuwa walikuwa wapi mwaka mzima wakati mgogoro huo ukiendelea.
Wanahoji kwanini asubiri hadi ripoti ya CAG inakaribia kuletwa mezani ndipo anazunguka kuwalainisha ili wapitishe bajeti upesi, tena kwa vitisho na ubabe kwamba watakaogoma kuhudhuria watafukuzwa udiwani.
Tunahoji kwa Massawe tukitaka kufahamu hasa analenga kuficha nini katika mgogoro huo wa Bukoba. Kwanini awe na haraka wakati ripoti ya CAG yenye ukweli wote iko tayari?
Kama naye sio sehemu ya ufisadi huo, ni kwanini asingoje CAG aiwasilishe ripoti ili isomwe na mchawi wa maendeleo ya Bukoba ajulikane kama ni madiwani au meya na viongozi wa serikali?
Mgororo wa Bukoba haukuanza juzi wala jana, viongozi wa dini pamoja na hao wazee wanaojaribu kutumiwa na Massawe, lazima watiliwe shaka kwamba walikuwa wapi tangu viongozi wote wa juu wa CCM akiwemo Rais Jakaya Kikwete wanashindwa kuutatua hadi kuomba CAG awatafutie ukweli?
Sasa kama ukweli huo uko tayari, kwanini Masaswe anajaribu kuzunguka mlango wa nyuma ili wananchi wasijue CAG alibaini nini? Katika jitihadi hizi za udalali wa kujaribu kumkinga Meya Amani, mkuu wa mkoa ana maslahi gani?
Kwa kitendo alichokifanya Massawe juzi, ni wazi kuwa amewadharau viongozi wa CCM na mkuu wake, yaani Rais Kikwete kwa kuingilia suala ambalo uamuzi wake ulikwishapelekwa kwenye ngazi nyingine.
Massawe ameletwa kuiongoza Kagera kama mteule na ataiacha wakati wowote mteule wake atakapoamua vinginevyo, sasa ni kwanini hawapi nafasi wawakilishi halali wa wananchi (madiwani) wakatimiza majukumu yao kwa kuzingatia utaratibu unaofaa?

CCM WAMSHITAKI MASSAWE KWA JK

CCM wamshtaki Massawe kwa JK
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Fabian MassaweCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimemshtaki kwa Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Fabian Massawe, kikidai kuwa ndiye chanzo cha mgogoro kati ya Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani na madiwani.
Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Massawe kujitumbukiza katika mgogoro huo, akidai anasuluhisha pande hizo mbili kwa kutumia viongozi wa dini na wazee maarufu, huku akitambua kwamba ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, iliyochunguza tuhuma za ufisadi haijatolewa.
Tanzania Daima Jumatano limedokezwa na kigogo mmoja wa makao makuu ya CCM, kwamba hatua hiyo ya Massawe imeleta shaka ya kwamba kuna jambo anataka lisijulikane katika ripoti ya CAG itakayokabidhiwa hivi karibuni.
“Huyu mkuu wa mkoa tumebaini ndiye chimbuko la matatizo yote ya Bukoba kwa namna anavyojaribu kumlinda mtuhumiwa. Yaani amefikia hatua ya kutaka kuonyesha umma kuwa mgogoro huo unasababishwa na imani za kidini.
“Chama kilikwishaamua kupitia Kamati Kuu, tukaomba serikali imwagize CAG afanye ukaguzi wa miradi ya kifisadi anayodaiwa kuitekeleza meya, sasa ripoti haijatolewa halafu yeye anaitisha vikao kuwababaisha madiwani,” alisema.
Kiongozi huyo ambaye alizungumza kwa sharti la kuhifadhiwa jina lake, alisema kuwa tayari wameagiza chama Mkoa wa Kagera kiwapatie muhtasari wa kikao hicho alichokifanya Massawe kwa ajili ya uamuzi zaidi.
“Huyu mtu ni tatizo na kwa jinsi inavyoonyesha, ripoti ya CAG imemkaanga meya, ndiyo maana Massawe anahaha kumnasua. Sisi tumeamua kumshtaki kwa rais ambaye ndiye mteuzi wake ili achukue hatua zaidi maana anavuruga chama,” kilisema chanzo hicho.
Juzi, Massawe aliitisha kikao na madiwani hao wanaompinga meya wakiwemo nane wa CCM na saba wa upinzani, mbele ya Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini, Sheikh wa Wilaya ya Bukoba, Haruna Kichwabuta na wazee maarufu kwa kile alichodai ni kuwapatanisha na meya ili vikao vya baraza viweze kufanyika wapitishe bajeti ya mwaka 2014/15.
Kati ya madiwani hao 15, saba wa CHADEMA na CUF hawakuhudhuria kikao hicho wakidai kutokitambua huku sita wa CCM waliingia na kuondoka bila muafaka kupatikana.
Amani aliingia kwenye mgogoro na madiwani wake wanane wa CCM pamoja na mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na wenzao saba wa CHADEMA na CUF wakitaka kumwondoa kutokana na tuhuma za kuendesha miradi ya kifisadi.
Baada ya mgogoro huo kuwa mkubwa na CCM ngazi ya taifa kushindwa kuumaliza, hatimaye Kamati Kuu ya chama hicho ilimwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kupitia Wizara ya Tamisemi kufanya ukaguzi maalumu wa tuhuma hizo kupitia CAG.
Oktoba 10, mwaka jana, CAG alianza ukaguzi huo na tayari amekamilisha ripoti yake akisubiri kuikabidhi, lakini kumekuwa na juhudi za makusudi za kutaka kupotosha taarifa hiyo ili isiwasilishwe kwa madiwani.
Wakizungumza na gazeti hili kwa simu juzi kutoka mjini Bukoba, baadhi ya madiwani hao walieleza kushangazwa na kitendo hicho cha Massawe ilihali wanasubiri ripoti ya CAG.
“Sisi tumemuuliza mkuu wa mkoa, wakati mgogoro huo ukiendelea hadi leo ambapo vikao havifanyiki, hao viongozi wa dini na wazee walikuwa wapi kutafuta muafaka hadi wangoje CAG amalize ukaguzi na ripoti inakaribia kutolewa ndipo waje kutusuluhisha?
“Kwanza kama tungekubali huo mtego wao, wananchi wetu wangetushangaa na kamwe wasingetuelewa kuona kile tulichokipigania kinakaribia kutolewa hadharani kujua ukweli halafu tunageuka,” alisema mmoja wao.
Massawe inadaiwa kuwa alijaribu kuwasihi madiwani hao akidai kuwa ripoti ya CAG haipo, na kwamba kama itakuwepo huenda ikachelewa kwa muda wa miezi miwili, na hivyo kuwataka waingie kwenye vikao vya baraza kupitisha bajeti.
Kwamba baada ya suluhu hiyo kukwama, Massawe aliahidi kutumia mabavu ya kumwagiza mkurugenzi wa halmashauri aitishe kikao cha Baraza la Madiwani akitishia kuwa diwani ambaye hatahudhuria atachukuliwa hatua za kuwajibishwa.
Waliohudhuria kikao cha juzi kutoka CCM ni Alexander Ngalinda wa Kata ya Buhembe ambaye pia ni Naibu Meya, Yusuf Ngaiza (Kashai) ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya, Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo), Richard Gaspar (Miembeni) na Murungi Kichwabuta wa Viti Maalumu.
Balozi Kagasheki na Dauda Kalumuna wa Kata ya Ijuganyondo hawakuweza kuhudhuria kikao hicho kutokana na kuwa katika majukumu yao mengine.
Miradi iliyokuwa inalalamikiwa ni upimaji wa viwanja 5,000 unaodaiwa mkopo wake wa sh bilioni 2.9 kutoka Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) haukufuata taratibu, na wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.
Upo pia ujenzi wa soko ambapo meya anadaiwa kusitisha malipo ya ushuru na kutaka kuwaondoa wafanyabiashara bila kufuata utaratibu.
Anatuhumiwa pia kukopa sh milioni 200 kutoka Benki ya Uwekezaji (TIB) bila kibali cha Baraza la Madiwani. Vile vile alitoa taarifa kwenye kikao cha baraza hilo kuwa TIB iliwapa ruzuku ya sh milioni 90, lakini hakueleza misingi yake.
Upo pia mradi wa kuosha magari ambao unadaiwa kutumia kiasi cha sh milioni 297 zinazotiliwa shaka. Ameshindwa pia kutoa mchanganuo wa mapato na matumizi ya mradi wa kiasi cha sh milioni 134, za ujenzi wa kituo cha mabasi.

Tuesday, 14 January 2014

MAREHEMU ALINDA( MTOTO WA JENI MMILIKI WA MTK BAR) KUZIKWA 15-1-2014 IZIMBYA

 Hii ni picha ya marehemu Alinda aliefariki 13-1-2014   katika hospital ya kagondo akiwa na umri wa miaka 15, alikuwa anaingia kidato cha tatu katika shule ya sekondari Zakia Meghiji iliyoko chato, na tarehe anafariki ndio ilikuwa siku yake ya kurudi shule, Bwana ametwaa jina lako lihimiliwe
                                     Jeni amepoteza mwanae wa kwanza
 Lily Tigo akiwa na Bety msibani
 Maua Daftari busy na simu msibani ,pembeni chui na London
 Bi Zamda
 Bw Wilson Mchunguzi akiwa msibani
 Majirani wakiwa msibani
 Kushoto ni mtoto pekee wa Jeni alibaki
 Kulia  ni Jeni aliefiwa na mwanae aliekuwa na umri wa miaka 15
 Swaiba mkubwa wa Jeni(mfiwa) Bi Pelina
                                    MC Baraka akiwasili eneo la msiba na Bw Yugin Kabendera
 Azizi Kachwamba
                                                          Msibani maisha yakiendelea
                                         Mmmmm jamani kazi ya mungu haina makosa
Moses Nyama msanii wa kakau Band(kushoto)akiwa na msanii Bk Sande(kulia) wakiwa eneo la msiba

RC AMTUMIA KILAINI KUMNASUA MEYA BUKOBA

Kanali mstaafu Fabian Massawe na  Meya wa  Bukoba, Anatory AmaniMKUU wa Mkoa (RC) wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, amekimbilia kwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini, Sheikh wa Wilaya, Haruna Kichwabuta na wazee maarufu ili wamsaidie kumnasua Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani, asing’olewe na madiwani.
Hatua hiyo inakuja wakati ambapo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Uttouh, akitarajiwa kuwasilisha ripoti ya ukaguzi wa miradi ya kifisadi katika manispaa hiyo wakati wowote.
Amani aliingia kwenye mgogoro na madiwani wake wakiwemo wanane wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki na wenzao saba wa CHADEMA na CUF wakitaka kumwondoa kutokana na tuhuma za kuendesha miradi ya kifisadi.
Baada ya mgogoro huo kuwa mkubwa na CCM ngazi ya taifa kushindwa kuumaliza, hatimaye Kamati Kuu ya chama hicho ilimwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kupitia Wizara ya Tamisemi kufanya ukaguzi maalumu wa tuhuma hizo kupitia kwa CAG.
Oktoba 10, mwaka jana, CAG alianza ukaguzi huo na tayari amekamilisha ripoti yake akisubiri kuikabidhi, lakini kumekuwa na juhudi za makusudi za kutaka kuipotosha taarifa hiyo ili isiwasilishwe kwa madiwani.
Mkuu wa Mkoa ambaye amekuwa mtetezi mkubwa wa Meya Amani, jana aliitisha kikao cha dharura kati yake na madiwani wanane wa CCM wanaompinga Amani na kuwalainisha waondoe tofauti zao ili Baraza la Madiwani lianze vikao vyake.
Wakizungumza na gazeti hili kwa simu jana kutoka mjini Bukoba, baadhi ya madiwani hao walieleza kushangazwa na kitendo hicho cha Massawe ilhali wanasubiri ripoti ya CAG iwasilishwe ili wajue kile kilichobainishwa kwenye uchunguzi.
“Sisi tumemuuliza mkuu wa mkoa, wakati mgogoro huo ukiendelea hadi leo ambapo vikao havifanyiki, hao viongozi wa dini na wazee walikuwa wapi kutafuta muafaka hadi wangoje CAG amalize ukaguzi na ripoti inakaribia kutolewa ndipo waje kutusuluhisha?
“Kwanza, kama tungekubali huo mtego wao wananchi wetu wangetushangaa na kamwe wasingetuelewa kuona kile tulichokipigania kinakaribia kutolewa hadharani kujua ukweli halafu tunageuka,” alisema mmoja wao.
Tanzania Daima lilidokezwa kuwa Massawe alijaribu kuwasihi madiwani hao bila mafanikio akidai kuwa ripoti ya CAG haipo na kwamba kama itakuwepo huenda ikachelewa kwa muda wa miezi miwili, hivyo kuwataka waingie kwenye vikao vya baraza kupitisha bajeti.
“Baada ya kuona tumeshikilia msimamo wetu, Massawe alitumia ubabe kumwagiza Katibu Tawala aitishe vikao hivyo kwa nguvu ili tutakao kaidi tuchukuliwe hatua za kinidhamu za kuwajibishwa.
“Sasa tumemtaka atueleze kama yeye yuko juu ya Rais Jakaya Kikwete, maana baada ya yeye kushindwa kumaliza mgogoro wetu ndipo kupitia kwa Waziri Mkuu alimwagiza CAG aje kukagua. Sisi tumemwambia kwamba tunataka ripoti zote ile ya Abbas Kandoro na CAG na si vinginevyo,” alisema diwani mwingine.
Kikao cha jana kilihudhuriwa na Alexander Ngalinda wa Kata ya (Buhembe), ambaye pia ni Naibu Meya, Yusuf Ngaiza (Kashai), ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya, Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga), Robert Katunzi (Hamugembe), Samwel Ruhangisa (Kitendagulo), Richard Gaspar (Miembeni) na Murungi Kichwabuta wa Viti Maalumu.
Balozi Kagasheki na Dauda Kalumuna (Ijuganyondo) hawakuweza kuhudhuria kikao hicho kutokana na kuwa katika majukumu  mengine.
Miradi iliyokuwa inalalamikiwa ni upimaji wa viwanja 5,000 unaodaiwa mkopo wake wa sh bilioni 2.9 kutoka Mfuko wa Dhama ya Uwekezaji (UTT) haukufuata taratibu, na wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.
Ipo pia ujenzi wa soko ambapo meya anadaiwa kusitisha malipo ya ushuru na kutaka kuwaondoa wafanyabiashara bila kufuata utaratibu.
Anatuhumiwa pia kukopa sh milioni 200 kutoka Benki ya Uwekezaji (TIB) bila kibali cha Baraza la Madiwani. Vile vile alitoa taarifa kwenye kikao cha baraza hilo kuwa TIB iliwapa ruzuku ya sh milioni 90, lakini hakueleza misingi yake.
Upo pia mradi wa kuosha magari ambao unadaiwa kutumia kiasi cha sh milioni 297 zinazotiliwa shaka. Ameshindwa pia kutoa mchanganuo wa mapato na matumizi ya mradi kiasi cha sh milioni 134, za ujenzi wa kituo cha mabasi.

Sunday, 12 January 2014

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAFANA


 Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia wananchi wa Zanzibar wakati akiingia kwenye uwanja wa Amani  na gari la wazi kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi.


 Sehemu ya Umati uliofurika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akikagua vikosi vya gwaride kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Amani.

 Wakina mama hawakuwa nyuma kwenye maandamano ya mika 50 ya Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.



 Kikosi cha Mbwa kikiingia uwanjani tayari kuonyesha umati wa watu jinsi Mbwa wenye mafunzo wanavyoweza kufanya kazi zao vizuri.
 Askari wakionyesha jinsi askari waliokuwa chini ya mkoloni walivyokuwa wanafanya mambo yao ikiwa kila amri kutoka kwa lugha ya kiingereza.
 Kikosi cha Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana na maadui bila kutumia silaha za moto kwenye uwanja wa Amani wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

 Sehemu ya Jukwaa kuu la uwanja wa Amani likiwa limefurika wakati wa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi.