Tuesday, 25 August 2015

MATUKIO YA KUWASILI KWA MWILI WA MAREHEMU LAMBERT NDIWAITA KUTOKEA NAIROBI .

Ilikuwa ni majonzi, vilio na simanzi pale mwili wa marehemu Lambert Ndiwaita ulipowasili katika viwanja vya kanisa la Kilutheri usharika wa Kashura Bukoba.
Jamaa mbalimbali waliofika kanisani kupokea mwili wa marehemu.
Gari maalumu kutoka nchini Uganda lililoleta mwili wa marehemu, ni moja ya kampuni inayofanya shughuli ya kuzika.
Kushoto ni mjane wa marehemu akisadiwa kushuka kwenye gari.

Mama mzazi wa marehemu(katikati) akisaidiwa.
Picha ya marehemu
Mchungaji wa usharika wa Kashura akiendesha ibada.
Mwili ukawasili nyumbani kwa marehemu Kishasha Bukoba mjini kabla ya kupelekwa kijijini kwao Maruku kwa mazishi.
Ni matukio,ilibidi asaidiwe.
Mwili wa marehemu ukipelekwa kijijini kwao Maruku kwa ajiri ya mazishi.Endelea kufuatili shughuli ya mazishi.

Monday, 24 August 2015

TANGAZO LA KIFO,BURIANI ENG LAMBERT NDIWAITA

Familia ya marehemu Eng. Lambert Ndiwaita wa Nairobi Kenya inasikitika kutangaza kifo cha Eng. Lambert Ndiwaita(pichani) kilitokea tarehe 20.8.2015 katika hospital ya Nairobi, Kenya, Marehemu Eng. Lambert Ndiwaita alikuwa ni mtaalam wa viwanja vya ndege kwenye shirika la viwanja vya ndege vya Kimataifa,chini ya  Umoja wa Mataifa (International Civil Aviation Organisation - ICAO) chini ya Umoja wa Mataifa.  Mwili wa Marehemu utasafirishwa kwenda nyumbani kwake Bukoba, Tanzania na mazishi  yatafanyika jumanne tarehe 25-08-2015 kijijini kwake Maruku Bukoba. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana  lihimidiwe, Amina.

Sunday, 23 August 2015

NI ZAIDI YA MAFURIKO JANGWANI,MTAISOMA NAMBA,CCM MBELE KWA MBELE


 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Jangwani.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 -2020
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye uzinduzi wa kampeni uliofanyika viwanja vya Jangwani.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan wakionyesha Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020  katikati ni Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye aliwakabidhi ilani hiyo kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM Jangwani.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikweteakizungumza baada ya kukabidhi ilani kwa mgombea wa CCM
 Umati wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM Jangwani.


  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Jangwani.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es salaam waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam.


 Hii ndio CCM
 TOT wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jijini Dar es Salaam.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia) akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwenye uzinduzi wa kampeni za CCM jijini Dar es Salaam.
 Wasanii wa bongo wakiwa jukwaani.