Meneja mkuu wa KCU Vedasto Ngaiza akiwakaribisha wajumbe wa mkutano mkuu wa mizania na kumkaribisha mwenyekiti wa bodi kufungua mkutano.
Mwenyekiti wa bodi ya KCU (1990 LTD) Bw John Binunshu akifungua mkutano
Makamu mwenyekiti wa bodi ya KCU Bw Ngalinda akisalimiana na wajumbe
Mjumbe wa bodi mama Muhazi akisalimia wajumbe wa mkutano
Bw Frank mjumbe wa mkutano mkuu kutokea chama cha msingi Maruku
Mjumbe akichangia baadhi ya maswala muhimu
Mjumbe kutokea Ibwera Bw Sadru Nyangasa akichangia maswala ya kuimarisha ushirika
Mkaguzi wa mahesabu kutoka Coasco akisoma mahesabu ya mizania yaliyokaguliwa na Coasco
Wanahabari wakifuatilia kwa umakini
Muonekano wa mkao katika ukumbi wa Bukoba Coop zamani uliitwa ukumbi wa Yasira Hotel
Watendaji wa KCU
Bw Kanjagaire wa kwanza kulia meneja kitengo cha kuuza kahawa nje kilichoko Moshi
Wajumbe wakipata chakula baada ya mkutano mkuu wa Mizani
Wednesday, 30 April 2014
KWA WALE WENYE MWALIKO WA BIRTHDAY PARTY YA KARNE YA MALKIA WA BW SIMBA MAWENYA
Bw Abdulrahim Simba Mawenya anapenda kuwakaribisha wageni wote mliopata mwaliko wa sherehe ya kuzaliwa ya malkia wake Raazizi mpenzi mke wake Bi Rukia Mawenya tarehe 2-5-2014 katika ukumbi wa Lina's ndani ya paa jipya kuanzia saa 1.00 jioni.KAULI MBIU NI KUPENDEZA, KULA, KUNYWA NA KUCHEZA. Karibuni sana.
Tuesday, 29 April 2014
IBADA YA MISA YA KUMALIZA MATANGA YA MAREHEMU DATUS BUBERWA NYAMWIHURA
Baba Paroko akinukuu mistari kwenye biblia
Baba Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba Methodius Kilain ni miongoni mwa wageni walioshiriki ibada
Kwaya
Wageni mbalimbali walioudhuria ibaya ya kumaliza matanga
ENEO LA KABURI LA MAREHEMU DATUS
Busara na hekima zimejaa kwa baba Askofu Kilaini
Dada wa marehemu
Jamcoblogspot,com inaiombea familia kuwa na subira katika hiki kipindi kigumu cha kumpoteza mpendwa wenu.Datus Buberwa Nyamwihura.
Baba Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba Methodius Kilain ni miongoni mwa wageni walioshiriki ibada
Kwaya
Wageni mbalimbali walioudhuria ibaya ya kumaliza matanga
ENEO LA KABURI LA MAREHEMU DATUS
Busara na hekima zimejaa kwa baba Askofu Kilaini
MAMA SALMA AZINDUA CHANJO YA KUZUIA MAAMBUKIZO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 9-16
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Leonidas Gama akimpokea Mke wa Rais Mama
Salma Kikwete kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro tarehe
28.4.2014. Mama Salma alikwenda Moshi kuzindua rasmi chanjo ya kuzuia
maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wa umri wa
miaka 9 hadi 16.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma
Kikwete akisalimiana na Mwakilishi wa Shirika la kuhudumia watoto,
UNICEF, hapa nchini Dkt. Sudha Sharma, mara baada ya kuwasili kwenye
uwanja wa Mandela uliopo katika eneo la Pasua katika Manispaa ya Moshi
kwa kulikofanyika uzinduzi rasmi ya chanjo ya saratani ya shingo ya
kizazi kwa wasichana.
Maandamano
ya vikundi mbalimbali kutoka katika Mkoa wa Kilimanjaro wakipita mbale
ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe ya uzinduzi wa
chanjo kwenye uwanja wa Mandela huko Pasua mjini Moshi tarehe 28.4.2014.
Mamia
ya watu waliohudhuria sharehe za uzinduzi wa chanjo ya kuzuia
maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana wakifuatilia
kwa makini hotuba ya Mgeni rasmi, Mama Salma Kikwete katika sherehe
hiyo.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi na wanafunzi
waliohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa chanjo ya kuzuia saratani ya
shingo ya kizazi kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 16 huko Pasua,
Moshi tarehe 28.4.2014.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi kwa
wasichana kwenye sherehe iliyofanyika huko Pasua, Moshi Mjini tarehe
28.4.2014. Wengine katika picha (kushoto kwenda kulia) ni Ndugu Leonidas
Gama, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Rufaro Chatora, Mwakilishi wa
Shirika la Afya Duniani hapa nchini, Dkt Kebwe Stephen Kebwe, Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Neema Rusibamayila, Mkurugenzi
wa Kinga kutoka Wizara ya Afya, Mama Salma na wa Kwanza kulia ni
Mwakilishin wa Shirika la Kuhudumia watoto (UNICEF) hapa nchini Dkt.
Sudha Sharma.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza naza mtoto Salma Abillah mara
baada ya kupata chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi na baadaye
kumkabidhi kadi yake ambayo anatakiwa kurudi tarehe 28.10.2014 kwa
ajili ya kupata chanjo ya pili.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete anaonekana akitoa chanjo ya matone kuzuia
ugonjwa wa polio kwa mtoto Ahmad, miezi 10, aliyefika kwenye sherehe ya
uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi
kwa wasichana huko Pasua, Moshi
Subscribe to:
Posts (Atom)