JAMCO BLOG BUKOBA

Tuesday, 15 April 2014

MAANDALIZI YA REDD'S MISS KAGERA YAANZA,KUFANYIKA MAPEMA MWEZI WA SABA,WAREMBO KUCHUANA KWANZA MAWILAYANI.

Mratibu wa mashindano ya urembo mkoa wa kagera ndugu Jamal Kalumuna akiongea na vyombo vya habari amesema kampuni ya Lweru Entertainment  ndio yenye dhamana ya  kuandaa na kusimamia mashindano ya  urembo  Redd's Miss Kagera  2014. Ndugu Jamal amesema baada ya sikukuu ya Pasaka utaanza mchakato wa kuwapata  washiriki wa  urembo katika baadhi ya Wilaya za Mkoa wa Kagera. Mratibu amezidi kueleza kuwa kwa mwaka huu wamejipanga vizuri kuhakikisha  wanapata warembo wenye sifa na uwezo wa kuuwakirisha Mkoa wa Kagera katika mashindano ya Kanda ya ziwa na Kitaifa,Mashindano ya kumpata malkia wa urembo Mkoa wa Kagera atapatikana mapema mwezi wa  saba na  mshindi wa pili na wa tatu watakaoshiriki mashindao ya kanda ya ziwa.  Pia ameyaomba  Makampuni, Taasisi, Mashirika na watu binafsi kutumia nafasi hii kudhamini na kutangaza shughuri  na biashara zao.
 Bw Haruna mmoja wa wanakamati wa maandalizi
 Picha kutoka maktaba
 Picha kutoka maktaba
 Ni moja ya Warembo waliowahi kushiriki Redd's Miss Kagera miaka ya nyuma
 Kamati
jamco blog at 02:22
Share

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version

About Me

jamco blog
View my complete profile
Powered by Blogger.